Showing posts with label kimataifa. Show all posts
Showing posts with label kimataifa. Show all posts

Friday, May 20, 2016

Update Ajali EgyptAir: Waliokuwa Zamu Paris Wabanwa

Zoezi la kutafuta mabaki ya ndege ya Misri iliyopotea hapo jana, leo limeingia siku ya pili ambapo tayari serikali ya Misri imesema ndege hiyo inawezekana ikawa imetunguliwa na magaidi na sio tatizo la kiufundi.

Nayo serikali ya Ufaransa inasema inajaribu kuchunguza iwapo taratibu za usalama hazikufuatwa huko mjini Paris. Maafisa usalama waliokuwa zamu wakati ndege hiyo Egypt air ilipopaa kuelekea Cairo wameanza kuhojiwa.

Ndege hiyo iliyokuwa na abiria sitini na sita ilipotea ilipokuwa njiani kutokea Ufaransa kuelekea mji mkuu wa Misri Cairo.
Wataalamu wa masuala ya usalama wanasema kama kulikuwa bomu kwenye ndege hiyo ingetua mara kwa mara.

Kabla ya kufika Paris ufaransa ndege hiyo ilitua katika miji ya Cairo, Tunis na Eritrea. Usalama katika uwanja wa ndege umeimarishwa tangu tukio la ugaidi lililotokea mwaka jana.

Nayo Serikali ya Misri imesema ndege hiyo ina uwezekano mkubwa kuwa ilitunguliwa na magaidi na si tatizo la kiufundi.
Maafisa usalama na ufundi kutoka Ufaransa wamekwenda Cairo nchini Misri kusaidiana na mamlaka ya nchi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

Bado kumekuwa na sintofahamu kuhusu eneo la mwisho ndege hiyo MS804 ilipopotelea takriban nusu saa kabla ya kutua.

Zoezi la kuitafuta ndege hiyo na mabaki yake bado linaendelea karibu na kisiwa cha Ugiriki cha Karpathos.

Tayari uchunguzi umeanza ambapo ulinzi mkali umeimarishwa katika uwanja wa ndege Charles de galles huko Paris Ufaransa.
Share:

Picha: John Legend Afurahia Kuwa Baba

Maisha huwa ni mazuri pindi unapokipata kitu unachokitaka.Kwa sasa maisha ya John Legend na mkewe, Chrissy Teigen yanaonekana kuwa na furaha zaidi tangu walipofanikiwa kupata mtoto wa kike, Luna Simone mwezi uliopita. Wawili hao wameonekana kwenye mitaa ya New York City wakizunguka huku John Legend akiwa amembeba Luna.


Share:

Thursday, May 19, 2016

Mabaki ya Ndege ya EgyptAir Yapatikana


Duru za kampuni ya ndege ya EGYPTAIR zimesema kuwa wizara ya usafiri wa anga nchini humo imepokea barua rasmi kutoka kwa wizara ya maswala ya kigeni nchini Misri inayothibitisha kupatikana kwa mabaki ya ndege iliotoweka ya MS 804 karibu na kisiwa cha Karpathos.

Hivyobasi kampuni hiyo imetuma salamu za rambi rambi kwa familia za abiria na wafanyikazi waliokuwa wakiabiri ndege hiyo.

Tayari familia za abiria hao pamoja na wafanyikazi wameelezewa kuhusu tukio hilo jipya.
Kwa sasa kundi la wachunguzi wa Misri wakishirikiana na wenzao wa Ugiriki wanaendelea kutafuta mabaki mengine ya ndege hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa imepaa kutoka uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle, Paris ikiwa na raia 15 wa Ufaransa.

Ndege hiyo pia ilikuwa na raia 30 wa Misri, raia 2 wa Iraq na raia mmoja mmoja kutoka Uingereza, Canada, Ubelgiji, Kuwait, Saudi Arabia, Algeria, Sudan, Chad na Ureno.

Awali rais wa Ufaransa Francois Hollande alikuwa amesema kuwa ndege hiyo ilianguka.
Share:

Staa wa filamu za James Bond apiga teke fuko la hela

Muigizaji raia wa Uingereza, Daniel Craig ayelikuwa akicheza filamu za James Bond amekataa ofa ya £68 milioni kutoka kwenye kampuni ya MGM Studio iliyomtaka acheze filamu mbili za 007.

Taarifa zinasema kuwa kwa sasa Tom Hiddleston ndiye anategemewa kuwa James Bond anayefuata baada ya Daniel Craig (48) kupiga chini ofa hiyo.

Mpaka sasa Daniel Craig ameshacheza filamu nne ndani ya miaka 11 na amefanikiwa kuingiza kiasi cha £38 milioni na kumzidi mwigizaji wa mwanzo aliyekuwa anacheza filamu hizo, Pierce Brosnan.

Aidha mtu wa karibu wa Daniel Craig amesema, “He had told people after shooting that this would be his final outing, but the film company still felt he could come around after Spectre if he was offered a money deal.”
Share:

Ndege ya Misri Yatoweka Kwenye Rada na Abiria 69

Ndege ya Shirika la EgyptAir la Misri ina ya Airbus A320 iliyotoweka kwenye rada
 
Ndege ya Shirika la EgyptAir la Misri ina ya Airbus A320 ikitokea jijini Paris, Ufaransa kwenda Cairo, Misri imetoweka kwenye rada ikiwa na watu 69.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika hilo, Airbus A320 ilitoweka katika maeneo ya mashariki ya Bahari ya Mediterranean, kilomita 16 kabla ya kufika katika anga la Misri.

Maofisa wanaosimamia safari za ndege wanasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria 59 na wahudumu 10.
Hakuna dalili zozote za kuwepo kwa hali mbaya ya anga zilizoripotiwa na nchi ya Misri imetuma ndege za kivita kuisaka ndege hiyo kwa ushirikiano na utawala wa Ugiriki.
Share:

Wednesday, May 18, 2016

Trump: Sitaelewana Kabisa na Waziri Mkuu wa Uingereza Nikiingia Madarakani

Mgombea anaewania urais nchini Marekani Donald Trump ameonya kuwa hatakuwa na uhusiano mzuri na waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron Ikiwa atakuwa rais wa Marekani.

Mwezi Disemba, Bwana Cameron alimtaja Trump kama mtu mwenye “ubaguzi, mjinga, na mwenye makosa” kufuatia kauli yake kwamba ataweka marufuku ya muda ya kuingia Marekani dhidi ya waislam.

Bwana Cameron amekataa kufuta kauli zake dhidi ya Bilionea Trump , ambae anatarajiwa kuwa mgombea wa urais wa Marekani kupitia chama cha Republican katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Akizungumza katika kituo cha televisheni cha Uingereza ITV kwa mara ya kwanza mbele ya umma tangu akosolewe Bwana Trump, alisema yeye si mjinga ama mbaguzi stupid bali ni”muunganishi”.

Kuhusu kauli za Bwana Cameron, Bwana Trump alisema : “yaelekea hatutakuwa na uhusiano mzuri sana, nani anajua.
“natumai kuwa na uhusiano mwema na yeye, lakini inaonekana ni kama hataki kutatua tatizo.”

Donald Trump pia alimkemea Meya wa London , Sadiq Khan, kwa kumuita “mjinga”.
Alielezea kauli yake kama kosa na isiyokua na ya heshima, huku akimtaka Bwana Khan afanyiwe vipimo vya uwezo wa akili yake (IQ).
Share:

Monday, May 16, 2016

Atiwa Mbaroni Kwa Kudandia Helkopta

Polisi wa Kenya wanamshikilia mtu mmoja mjini Bungoma baada ya kuning’inia kwenye helikopta iliyoubeba mwili wa aliyekuwa mfanyabiashara Jacob Juma.

Mtu huyo, Saleh Wanjala ambaye hakutoa sababu za kufanya hivyo, alishikiliwa na polisi huku akipata matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa Bungoma.

Wanjala alionekana akining’inia kwenye helikopta iliyobeba mwili wa mfanyabiashara huyo wakati ikipaa kutoka kwenye Uwanja wa Posta mjini Bungoma baada ya wananchi kutoa heshima za mwisho.

Wanjala aliamua kuidandia helikopta hiyo wakati ikiondoka kupeleka mwili wa Juma nyumbani kwake katika Kijiji cha Mungore.

Akisimulia mkasa huo, Wanjala alisema alikuwa karibu na helikopta hiyo wakati ikianza kupaa na kwamba aliumia baada ya mguu wake kukwama.

“Nilikuwa nimeketi chini ya helikopta na wakati ilipokuwa inaanza kupaa, mguu wangu ulikwama hapo ikabidi nijishikilie vizuri ili nisianguke,” alisema Wanjala.

Rubani wa helikopta hiyo alilazimika kumpeleka hadi uwanja wa ndege wa Bungoma mita 700 kutoka kwenye uwanja huo lakini Wanjala aliamua kuruka na kuumia vibaya miguu na mikono. Muuguzi wa Hospitali ya Bungoma, Leah Atsewa alisema bado wanamfanyia uchunguzi. 
 
Share:

Friday, May 13, 2016

Mwanamke mkongwe zaidi duniani afariki New York

 Bi Jones alizaliwa mwaka 1899 

Mwanamke aliyetambuliwa kuwa mkongwe zaidi duniani amefariki dunia alipo kuwa akitibiwa jijini New York, Marekani, madaktari wamesema.

 Susannah Mushatt Jones, amefariki akiwa na umri wa miaka 116.Alizaliwa eneo la mashambani jimbo la Alabama mwaka 1899, na amekuwa akiugua kwa siku kadha.

Morano sasa ndiye mwanamke mzee zaidi duniani 

Mwanamke Mwitaliano, Emma Morano, ambaye ni mdogo wa umri wa Bi Jones kwa miezi kadha, sasa ndiye anayetambuliwa kuwa mwanamke mkongwe zaidi duniani.

Anaaminika kuwa mtu pekee duniani aliyezaliwa karne ya 19 ambaye bado yuko hai.

Source: BBC
Share:

Thursday, May 12, 2016

Rais Yoweri Museveni Aapishwa Rasmi Kuwa Rais wa Uganda

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameapishwa Rasmi kuwa Rais wa nchi hiyo katika viwanja vya Kololo nchini humo na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Afrika akiwamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutoka Tanzania.
Share:

Video: Mpinzani wa Museveni, Dr Kiiza Besigye Akamatwa Baada ya Kujiapisha Kuwa Rais

Mpinzani mkuu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye ambaye amekuwa akipinga ushindi wa Rais huyo, amekamatwa na polisi wa nchi hiyo baada ya jana kujiapisha kuwa Rais ikiwa ni siku moja tu (leo) kabla ya Museven kuapishwa.

Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa vizuizi  vya polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''.

Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya juu''.

Video hiyo ilisambazwa kwa kasi  kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliopita akiwaacha kwa mbali wapinzani wake wakuu, Kizza Besigye na Amama Mbabazi.

Kadhalika, Mahakama Kuu nchini humo ilihalalisha ushindi wa Museveni baada ya kutupilia mbali shauri la pingamizi la ushindi huo lililowasilishwa na Amama Mbabazi.
Share:

Picha: 2Face Apewa Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu Nchini Nigeria

Msanii wa Nigeria, 2Face amekuwa msanii wa kwanza wa nchi hiyo kupewa shahada ya heshima na chuo kikuu cha Igbinedion, Okada.

Shahada hiyo ya heshima kwa 2Face alikabidhiwa ikiwa imeambatana na sherehe za kusherekea miaka 17 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.

Aliyekuwa Gavana wa jimbo la Edo, Chief Lucky Igbinedion ambaye ni makamu wa chuo hicho alihudhuria kwenye sherehe hizo akiwa sambamba na Prof. Sir. Victor Uwaifo na mchekeshaji maarufu wa nchi hiyo Maleke.


Share:

Wednesday, May 11, 2016

Mwanamke wa miaka 72 ajifungua mtoto India


Mwanamke wa umri wa miaka 72 amejifungua mtoto wa kiume katika hospitali moja nchini India.

Mwanamke huyo alipachikwa mimba kupitia njia ya kitaalamu ya IVF ambapo yai la mwanamke hutolewa kutoka kwenye ovari, kutungishwa mbegu ya kiume na kisha kurejeshwa kwenye mji wa mimba. Yai hilo linaweza kutolewa kwa mwanamke mwingine.

Njia hiyo hutumiwa kuwawezesha wanawake tasa kupata watoto.Daljinder Kaur alijifungua mtoto wake baada ya kupokea matibabu kwa miaka miwili katika hospitali iliyoko jimbo la Haryana.

Matabibu walifanikiwa kumtungisha mimba kupitia IVF mara yao ya tatu.Mumewe Kaur ana umri wa miaka 79.

Kisa hicho kimezua mjadala mkali kuhusu kutumiwa kwa teknolojia hiyo ya IVF na umri ambao wanawake wanaweza kuruhusiwa kuitumia kupata watoto.

Dkt Kanad Nayar, katibu mkuu wa chama cha upachikaji mimba nchini India anasema sheria ya kuamua umri wa juu ambao mwanamke anaweza kuruhusiwa kutumia teknolojia hiyo itatungwa karibuni.

Umri huo utakuwa karibu miaka 55.Daktari huyo anasema jambo la kuzingatiwa zaidi ni uwezo wa mwanamke kumlea mtoto hadi akomae.

"Ukimzaa mtoto lazima uweze kumlea mtoto kwa karibu miaka 20 hivi. Huwezi kujifungua mtoto kisha uwaache watu wengine wakimlea,” amesema Dkt Nayar.

Ni mara ya pili kwa mwanamke mkongwe kujifungua mtoto India. Awali, mwanamke wa miaka 70 alijaliwa mtoto nchini humo.

Lakini mwanamke huyo alifariki miaka miwili baadaye na sasa mtoto huyo anatuzwa na jamaa zake.

Credit: BBC
Share:

Tuesday, May 10, 2016

Picha: Mfahamu binti wa Van Damme, Bianca,anapiga mkono kama baba yake

Bianca, binti wa Van Damme

Mtoto wa nyoka naye ni nyoka vile vile. Uzuri wa Bianca Van Varenberg, 25, usikulaghai ukadhani ni binti wa kuchezea tu. Atakupa mkong’oto hadi usahau njia uliyopitia.

Ni mtoto wa muigizaji mkongwe wa movie za mapigano, Jean Claude Van Damme.

Anajulikana zaidi kikazi kama Bianca Bree. Miaka mitano iliyopita alionekana kwenye uzinduzi wa filamu ya baba yake lakini akawa kimya tena, hadi sasa.


Mwaka 2012 alisema angependa atoke kinyake bila kutumia jina la baba yake ndio maana hajaliweka kwenye majina yake.

 Yeye pia anapenda kuja kuwa muigizaji wa filamu.
Share:

Picha:Mama afichua pacha wake watano Aliojifungua Ndani ya Dakika 2

Mama mmoja raia wa Australia ametoa picha za mapacha watano aliowazaa mwezi Januari.

Kim Tucci wa miaka 26 alichukua dakika mbili tu kujifungua wanawe hao, wasichana wanne na mvulana mmoja.Wote walitungwa kawaida na hakutumia matibabu yeyote ya uzazi.


Madaktari 50 walimsaidia mama huyo kujifungua kwa njia ya upasuaji, na wanawe wote wako salama.Wanasayansi wanasema ni mama mmoja kati ya milioni 55 wenye nafasi ya kuzaa mapacha watano.


Bi Tucci alipata umaarufu sana wakati alipoweka taarifa za mimba yake katika ukurasa wake wa Facebook.Kampuni ya kunasa picha ya Erin Elizabeth imesaidia sana kunadi safari ya Bi Tucci wakati wa ujauzito wake.


Mama huyo ameelezea changamoto alizokumbana nazo akisema kuwa kuna kipindi alihisi kama anapoteza maisha.Ameongeza kusema kuwa madaktari walimshauri kuwaokoa watoto wawili na kumtaka kuwatoa wengine kutokana na sababu za kiafya.Hata hivyo yeye aliamua kubeba mimba yake hadi mwisho.


Bi Tucci na mumewe bwana Vaughn wana watoto watano,wanne wasichana na mvulana mmoja.Wameanza kuchangisha pesa ili kununua gari kubwa ambalo litaweza kutosha familia hiyo kubwa.
Share:

Monday, May 9, 2016

Bush Asema Hatampigia Kura Donald Trump

Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Jeb Bush amesema hatampigia kura Donald Trump katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini humo Novemba mwaka huu.

Bush alisema kuwa Trump hana tabia wala mienendo ya kuwa Rais wa Marekani.

‘‘Marais wa Marekani wanasifa zao na wanakubalika kwa watu, lakini huyu jamaa hana sifa hata moja ndiyo maana kila siku namkana na kusema hafai kabisa kuwa rais wa nchi hii, ’’alisema Bush

Jeb ni mojawapo wa wanachama mashuhuri wa Republican kutanganza hadharani kuwa hatampigia kura Trump kwa sababu ya kampeni yake ya kiburi ambayo imegawanya Chama cha Republican.

Juzi Spika wa Bunge, Paul Ryan alisema hatamuunga mkono mfanyabiashara huyo tajiri ingawa atakutana naye wiki ijayo.

Hata hivyo, Trump aliungwa mkono na mgombea urais wa zamani wa nchi hiyo, Bob Dole aliyeshindwa katika uchaguzi na Bill Clinton wa Chama cha Democratic mwaka 1996.

Wiki iliyopita Seneta wa Texas, Ted Cruz alijitoa katika kinyang’anyiro cha kuwania uteuzi wa kugombea urais kwa Republican baada ya kushindwa katika uchaguzi wa awali dhidi ya mpinzani wake huyo.

Cruz aliwaambia wafuasi wake katika mji wa Indianapolis kwamba: “ Njia hii kuelekea ushindi imefungwa” na kusema kuwa wapiga kura wamechagua njia nyingine.

Alitoa shukrani kwa wafuasi wake wote. Trump alipata ushindi mkubwa Indiana huku Cruz akishika nafasi ya pili na gavana wa Ohio John Kasich akiwa katika nafasi ya tatu.

Trump alisema huo ni ushindi mkubwa kwake na kumpongeza Cruz akimuita yeye na wagombea wengine 15 waliokuwa wanagombea uteuzi wa Republican kuwa ni werevu na wenye nguvu.Alitoa wito wa kuwa na umoja ndani ya chama hicho.

Kwa upande wa Democratic seneta wa Vermond, Bernie Sanders ameshinda katika jimbo la Indiana dhidi ya Hillary Clinton

Wagombea hao wawili walibadilishana ushindi kabla ya Sanders kuibuka mshindi kwa asilimia saba ya kura. Hata baada ya ushindi huo wa Sanders katika jimbo la Indiana, Hillary anaongoza katika idadi ya wajumbe ikionyesha kwa mahesabu ni vigumu kwa Sanders kuteuliwa kuwa mgombea wa Democratic
Share:

Sunday, May 8, 2016

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Ahudhuria Mazishi ya Lucy Kibaki nchini Kenya

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.

 
Marehemu Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema katika familia.

Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.
Share:

Saturday, May 7, 2016

Hasira Za Ugomvi Wa Kimapenzi Zamalizikia Kwenye Range Rover Revere

Picha za gari lililokuwa na ujumbe wa kukasirisha uliochorowa katika gari hilo zimesambazwa mara elfu katika mtandao wa Twitter.



Gari hilo jeupe aina ya Range Rover Revere lenye bei ya Kuanzia pauni 75,000 lilionekana limeegeshwa karibu na Harrods magharibi mwa London na kuchorwa ujumbe wa kukasirisha kwa kile kilichoonekana kuwa mpenzi aliyedanganywa.


Gari hilo liliandikwa 'cheater' katika pande zote mbili za gari huku maneno ''Hope she was worth it'' yakiandikwa katika madirisha ya gari hilo.Klo ambaye alipiga picha za gari hilo alisema kuwa alimuona mwanamke mmoja akilichora gari hilo,alikuwa kama amechanganyikiwa.


'Hakuna mtu aliyejaribu kumzuia.Baadaye aliondoka.Maneno ''Its Over'' pia yaliandikwa kwenye gari hilo ikielezea kuisha kwa uhusiano wowote'. 

Share:

Thursday, May 5, 2016

Video: Mwanamke Aokolewa Akiwa Hai Kwenye Vifusi Nairobi Siku 6 Baada ya Jumba Kuporomoka


Mwanamke ametolewa akiwa hai kutoka kwenye vifusi siku sita baada ya jumba kuporomoka katika mtaa wa Huruma, Nairobi.Amepelekwa hospitalini.

Juhudi za uokoaji bado zinaendelea.Mwandishi wa BBC Anthony Irungu alishuhudia mwanamke huyo akitolewa kwenye vifusi.

Share:

P Diddy Aongoza Orodha ya Forbes ya Wana Hip Hop Watano Wenye Mkwanja zaidi


Forbes wametoa orodha mpya ya wasanii wa hip hop wenye fedha zaidi, The Forbes Five.
Diddy ameongoza orodha hiyo mwaka huu kwa kuwa na utajiri ufikao dola milioni 750. Nafasi ya pili imekamatwa na Dr Dre mwenye dola milioni 710 huku Jay Z akifuatia kwa dola milioni 610.
Mwanzilishi wa Cash Money, Birdman amefuatia katika nafasi ya nne akiwa na dola milioni 110. Drake amechukua nafasi ya 50 Cent na kukamata nafasi ya tano kwa utajiri wa dola milioni 60.
Share:

Wapenzi wa Jinsia moja wapinga ukaguzi wa Nyeti Zao

Wanaume wawili wanaosema kuwa maafisa wa polisi wa Kenya waliwalazimisha kufanyiwa ukaguzi wa tupu ya nyuma ili kubaini kwamba walishiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja wameanzisha kesi mahakamani wakitaka ukaguzi huo kuwa ukiukaji wa katiba.

Wanasema kuwa walilazimishwa kufanyiwa ukaguzi wa magonjwa ya virusi vya ukimwi na Hepatitis kufuatia kukamatwa kwao mnamo mwezi Februari 2015 baada ya kushukiwa kwamba wanashiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja.

Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja kushiriki ngono ni kinyume na sheria nchini Kenya na adhabu ya makosa hayo ni miaka 14 jela.Mahakama ya Mombasa imewapatia mawakili wa serikali wiki moja kutoa jibu.

Chini ya sheria ya kimataifa ,ukaguzi wa lazima katika tupu ya nyuma ni kitendo cha kikatili,unyama na ni sawa na mateso kulingana na kundi la haki za kibinaadamu Human rights Watch.
Share:

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger