Wanaume wawili wanaosema kuwa
maafisa wa polisi wa Kenya waliwalazimisha kufanyiwa ukaguzi wa tupu ya
nyuma ili kubaini kwamba walishiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia
moja wameanzisha kesi mahakamani wakitaka ukaguzi huo kuwa ukiukaji wa
katiba.
Wanasema kuwa walilazimishwa kufanyiwa ukaguzi wa magonjwa
ya virusi vya ukimwi na Hepatitis kufuatia kukamatwa kwao mnamo mwezi
Februari 2015 baada ya kushukiwa kwamba wanashiriki katika ngono ya
mapenzi ya jinsia moja.
Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja kushiriki ngono ni kinyume na sheria nchini Kenya na adhabu ya makosa hayo ni miaka 14 jela.Mahakama ya Mombasa imewapatia mawakili wa serikali wiki moja kutoa jibu.
Chini
ya sheria ya kimataifa ,ukaguzi wa lazima katika tupu ya nyuma ni
kitendo cha kikatili,unyama na ni sawa na mateso kulingana na kundi la
haki za kibinaadamu Human rights Watch.
0 comments:
Post a Comment