Zoezi la kutafuta mabaki ya ndege ya
Misri iliyopotea hapo jana, leo limeingia siku ya pili ambapo tayari
serikali ya Misri imesema ndege hiyo inawezekana ikawa imetunguliwa na
magaidi na sio tatizo la kiufundi.
Nayo serikali ya Ufaransa
inasema inajaribu kuchunguza iwapo taratibu za usalama hazikufuatwa huko
mjini Paris. Maafisa usalama waliokuwa zamu wakati ndege hiyo Egypt air
ilipopaa kuelekea Cairo wameanza kuhojiwa.
Ndege hiyo iliyokuwa na abiria sitini na sita ilipotea ilipokuwa njiani kutokea Ufaransa kuelekea mji mkuu wa Misri Cairo.
Wataalamu wa masuala ya usalama wanasema kama kulikuwa bomu kwenye ndege hiyo ingetua mara kwa mara.
Kabla
ya kufika Paris ufaransa ndege hiyo ilitua katika miji ya Cairo, Tunis
na Eritrea. Usalama katika uwanja wa ndege umeimarishwa tangu tukio la
ugaidi lililotokea mwaka jana.
Nayo Serikali ya Misri imesema ndege hiyo ina uwezekano mkubwa kuwa ilitunguliwa na magaidi na si tatizo la kiufundi.
Maafisa
usalama na ufundi kutoka Ufaransa wamekwenda Cairo nchini Misri
kusaidiana na mamlaka ya nchi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi.
Bado kumekuwa na sintofahamu kuhusu eneo la mwisho ndege hiyo MS804 ilipopotelea takriban nusu saa kabla ya kutua.
Zoezi la kuitafuta ndege hiyo na mabaki yake bado linaendelea karibu na kisiwa cha Ugiriki cha Karpathos.
Tayari uchunguzi umeanza ambapo ulinzi mkali umeimarishwa katika uwanja wa ndege Charles de galles huko Paris Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment