Ndege ya Shirika la EgyptAir la Misri ina ya Airbus A320 iliyotoweka kwenye rada
Ndege ya Shirika la EgyptAir la Misri ina ya Airbus A320 ikitokea
jijini Paris, Ufaransa kwenda Cairo, Misri imetoweka kwenye rada ikiwa
na watu 69.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika hilo, Airbus A320
ilitoweka katika maeneo ya mashariki ya Bahari ya Mediterranean,
kilomita 16 kabla ya kufika katika anga la Misri.
Maofisa wanaosimamia safari za ndege wanasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria 59 na wahudumu 10.
Hakuna dalili zozote za kuwepo kwa hali mbaya ya anga zilizoripotiwa
na nchi ya Misri imetuma ndege za kivita kuisaka ndege hiyo kwa
ushirikiano na utawala wa Ugiriki.
0 comments:
Post a Comment