Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa
miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la
Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.
Marehemu
Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira
safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na
wema katika familia.
Kikwete
ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha
mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika
katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria
mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja
marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.
0 comments:
Post a Comment