Showing posts with label dini. Show all posts
Showing posts with label dini. Show all posts

Monday, May 9, 2016

Picha: Rais Magufuli Alivyoshiriki Ibada Ya Jumapili Ya Kupaa Kwa Bwana Katika Parokia Ya Toleo La Bwana Jimbo La Arusha Mjini Jana

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 08 Mei, 2016 aliungana na waumini wa Parokia ya Toleo la Bwana iliyopo katika Jimbo Katoliki la Arusha kusali ibada ya Jumapili, ambapo katika salamu zake amewaomba watanzania kuendelea kuiombea nchi yao ili kazi anayoifanya ya kukabiliana na matatizo yanayowakabili watanzania wanyonge ifanyike kwa mafanikio.

Dkt. Magufuli amesema hayo alipokaribishwa na Mwenyekiti wa Parokia hiyo Bw. Philemon Mushi kuwasalimu waumini wa kanisa hilo, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Jumapili ya kupaa kwa Bwana.

"Niko pamoja na nyinyi ndugu zangu watanzania na wana Arusha wote, napenda kuwaahidi tena sitawaangusha, nitasimama mbele kuwatetea masikini, siku zote nitakuwa upande wenu, siku zote nitatembea na nyinyi, nasema kwa dhati kabisa na nataka muamini hilo kwamba sitawaangusha" amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa na waumini walioshiriki ibada hiyo.

Rais Magufuli amewahakikishia watanzania wote kuwa atahakikisha ahadi zote alizoziahidi anazitekeleza na amewaomba watanzania wote kuungana na kushikamana ili kufanikisha juhudi za kuijenga Tanzania bora.

"Ninajua kuongoza ni kazi kubwa, ninajua kuongoza Taifa lililo masikini kama Tanzania inahitaji mkono wa Mungu, kwa hiyo niwaombe sana ndugu zangu Wakristo na watanzania kwa ujumla, muendelee kuliombea Taifa hili, kuniombea mimi, na pia kujiombea sisi wote ili amani tuliyonayo katika nchi yetu iendelee kudumu katika maisha yote.

"lakini siku zote katika matendo yetu kila tunapofanya tumtangulize Mungu kwa sababu Mungu ndio kila kitu, lakini tutambue kwamba siku moja tutakufa, kwa hiyo ni vyema katika matendo yetu tutakapokuwa hapa duniani tujitahidi sana kufanya matendo mazuri kwa ajili ya watu na hasa watu wanyonge, ambao kwa kweli watanzania waliowanyonge wanapata shida sana" Amebainisha Rais Magufuli.

Pia Dkt. Magufuli amewasihi watanzania wote kuachana na ushabiki wa vyama vya siasa na badala yake waungane katika ujenzi wa Taifa na kukabiliana na kero zinazowaumiza
 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha Mei 8, 2016
 
Sehemu ya waumini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akiwsalimia  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha  Mei 8, 2016.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea zawadi ya Rozari kutoka kwa Padri Kiongozi  Peter Pinto Sio Germin Longio  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha Mei 8, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea zawadi ya Biblia Takatifu kutoka kwa Padri Kiongozi Peter Pinto Sio Germin Longio  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha Mei 8, 2016
 





Share:

Tuesday, May 3, 2016

Mary Msigwa: Wasanii chipukizi hatuthaminiwi


MWIMBAJI chipukizi katika muziki wa Injili nchini, Mary Msigwa, amelalamikia wasanii wenye majina makubwa katika muziki huo kutowathamini, vyombo vya habari na wadau wa muziki huo pindi wanapotaka msaada kwa ajili ya kukuza muziki wao.

Msigwa alilalama kwamba nyimbo za wasanii chipukizi hazipewi nafasi ya kuchezwa kwenye redio na runinga mbalimbali bila sababu za msingi.

Mary alisema changamoto nyingine zinazowakabili waimbaji wachanga ni kukosa fedha kwa ajili ya kurekodia, kushindwa kujitangaza kiasi kwamba wanashindwa kutambulika kwa jamii.

“Wasanii chipukizi hatuthaminiwi na hii imesababisha baadhi ya wenzetu kushindwa kuendelea na huduma hii kwani hata kama ukifanikiwa kurekodi kwa kujibana shida inakuwa kwa watangazaji wa redio na televisheni ambao huwa hawazipi nafasi nyimbo zetu na hii inasababisha tushindwe kufahamika kwenye jamii,” alisema mwimbaji huyo.
Share:

Kanisa Katoliki Lachomwa Moto Karagwe

Picha si ya tukio halisi
Watu wasiofahamika wamechoma moto Kanisa Katoliki Kigango cha Nyarwele, Parokia ya Kimiza, Jimbo la Kayanga wilayani Karagwe, Mkoa wa Kagera.

Katika tukio hilo la jana usiku, mali zote zilizokuwamo ndani ambazo thamani yake haijajulikana ziliteketea.

Shuhuda wa tukio hilo, Paulina Nkuba (67) alisema alifika eneo la tukio asubuhi baada ya kupewa taarifa na mjukuu wake anayesoma Shule ya Msingi Kimiza.

Alisema baada ya kufika katika eneo la tukio alipiga yowe kuomba msaada na alipoona watu hawatokei, alitoa taarifa kwa uongozi wa kitongoji ndipo waliwajulisha wananchi na kuanza kukusanyika. 
Paroko wa Parokia ya Kimiza, Padre Fortunatus Bijura alisema kitendo hicho ni cha kuhuzunisha na kusisitiza hawataacha kusali kwa kuwa hata chini ya mti watafanya ibada.

Askofu wa jimbo hilo, Almachius Vicent Rweyongeza aliwataka waumini wasilipize kisasi hata kama wakimjua aliyechoma kanisa hilo.

Mwenyekiti wa kamati ya kanisa hilo, Sabas Kafuba alivitaja baadhi ya vitu vilivyoteketea kuwa ni jengo, nyaraka, meza, viti, kinanda na jenereta.

Akizungumza na wananchi, ofisa upelelezi wa Wilaya ya Karagwe aliyejitambulisha kwa jina la Masoud aliwataka kuunda vikundi vya ulinzi na kutoa taarifa za kukomesha uhalifu huo.
Share:

Tuesday, October 15, 2013

SIKUKUU YA EID-EL-HAJJ NI OKTOBA 16, 2013 - BAKWATA....


Share:

Friday, October 11, 2013

TAHADHARI: UAMSHO WAPANGA KUFANYA UGAIDI KWA VIONGOZI WA DINI NA SERIKALI KABLA SIKUKUU YA Eid El Haj.


Waraka wenye vitisho ukiwa na nembo ya Jumuiya ya Uamsho na mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) umesambazwa visiwani Zanzibar, ukidaiwa kutishia kufanyika kwa shambulio dhidi ya viongozi wa dini na Serikali kabla ya Sikukuu ya Eid El Haj.
 


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam amethibitisha kupata nakala ya waraka huo wenye maneno makali na vitisho kwa usalama wa watu na amani ya nchi. Kamanda Mkadam alisema,Polisi imefanikiwa kuupata waraka huo baada ya tukio hilo kuripotiwa na baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini Visiwani humo.
 


Hata hivyo, alisema,tayari makachero wa Polisi wako kazini na ametoa wito kwa viongozi wa dini na wananchi kuondoa hofu kwa vile vyombo hivyo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kukabiliana na tukio lolote la kihalifu.
 


Aliwasihi wananchi kuendelea na jitihada za kuwafichua wahalifu na watu wanaowatilia shaka dhidi ya amani visiwani hapa.
 


“Hatua tulizochukua ni pamoja na kuwataka viongozi wa dini kuanzisha kamati za ulinzi mbali na kuwapatia huduma za ulinzi kama njia ya kukabiliana na matukio mbalimbali,”alisema Kamanda Mkadam.
 
Waraka huo unadaiwa kuainisha vitendo vya hujuma kuwa vitazidi hadi pale Zanzibar itakapofanikiwa kurejesha kile kilichoitwa Uhuru wake.

Source:Gazeti la Mwananchi
Share:

Tuesday, May 28, 2013

DHAMBI YA UASHERATI YAZIDI KULITAFUNA KANISA KATOLIKI, MWEKITI WA KANISA ANOGEWA NA PENZI LA 'NYUMBA NDOGO' NA KUAMUA KUMHONGA GHOROFA.... !!

HALI ya hewa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Tabata, jijini Dar es Salaam  si shwari hata kidogo kufuatia baadhi ya waumini kumtuhumu Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji, Faustin Mchanuzi kwamba ana ‘nyumba ndogo’ anayoitembelea kila mara hivyo aachie ngazi kwa sababu kitendo hicho ni uzinzi, Uwazi linakupa hatua kwa hatua.
Kutokana na hali hiyo, waumini hao wanadaiwa kuweka msimamo wao kwamba endapo kiongozi huyo hataondolewa, wapo tayari kulihama kanisa hilo



KWA NINI KANISA LITIKISIKE?
Siku za karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya baadhi ya viongozi wa kanisa hilo kudaiwa kushiriki vitendo vinavyotafsiriwa kuwa ni vya uzinzi.
Hivi karibuni Padri Urbanus Ngowi wa Jimbo la Moshi alidaiwa kufumaniwa na mke wa mtu aliyejulikana kwa jina moja la kijamii la Mama P.
Mbali na Padri Ngowi kunaswa na mwanamke huyo na picha zake kutolewa kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda Toleo la 313 la Aprili –Mei 5, 2013, pia Padri Celestine John Nyaumba wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Homboro Dodoma anadaiwa kumjeruhi mwanamke aliyezaa naye, Selestina Anania Kibena licha ya kwamba sheria za kanisa hilo haziruhusu mapadri kuzaa wala kuoa.

TURUDI KWA MCHANUZI
Mchanuzi, licha ya kudaiwa kuwa na nyumba ndogo pia waumini hao wamedai amekwenda mbele zaidi kwa kuamua kumjengea mwanamke huyo nyumba ya ghorofa Tabata Kinyerezi, Dar.

PAROKO AINGILIA KATI
Madai hayo yalivuma kiasi kwamba, paroko wa parokia hiyo, Cyprian Kagaba (pichani) aliamua kuingilia kati kwa kuitisha vikao kwa nyakati tofauti na wajumbe wa Kigango cha Kimanga na Jumuiya Kuu ya Mtakatifu Martin ili kujua nini tatizo au kiini cha kuwepo kwa madai hayo mazito.

WAUMINI WAMUITA KADINALI PENGO
Licha ya kutopatikana kwa suluhu kupitia vikao vilivyoitishwa na Paroko Kagaba, baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamemuomba Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo kufika kanisani hapo ili kuweka mambo sawa.
Waumini hao wamedai kwamba pamoja na paroko wa kanisa hilo kuingilia kati kwa kuitisha vikao lakini bado hali si shwari wakisisitiza mwenyekiti huyo ang’oke.
“Suala hili la mwenyekiti limeleta mgawanyiko mkubwa ndani ya kanisa hali inayohatarisha usalama na kurudisha nyuma maendeleo ya kanisa,” alisema mmoja wa waumini wa kanisa hilo huku akiomba jina lake lisiandikwe gazetini.

WASIWASI FEDHA ZA KANISA KUJENGA GHOROFA Waumini hao waliendelea kudai kwamba wana wasiwasi kwamba fedha alizotumia mwenyekiti huyo kumjengea ghorofa mwanamke huyo, zinaweza kuwa za kanisa kwa vile hakuna taarifa yoyote inayotolewa kwa waumini au wajumbe wa kanisa hilo kuhusu matumizi ya fedha.
Ilibainika kuwa chanzo cha kuzuka kwa madai hayo ya kuwepo kwa nyumba ndogo ni matumizi hayo ya fedha ambapo mwenyekiti huyo anasimamia.
Waumini hao waliendelea kudai kuwa matumizi mabaya ya fedha yalisababisha baadhi ya viongozi kujiuzulu akiwemo aliyekuwa katibu, Perpetua Mashele ambaye alimwandikia barua Paroko Kagaba juu ya dhumuni la kuachia ngazi.
Barua hiyo (nakala tunayo) iliandikwa Aprili 10, mwaka huu ikieleza kwamba shughuli aliyokuwa akipaswa kuifanya kikatiba ameporwa na kufanywa na viongozi wachache kwa manufaa yao binafsi.
Katika barua hiyo, aliyekuwa mweka hazina ambaye pia alijiuzulu, katika kipindi chake cha uongozi wa miaka mitatu hakuwahi kwenda benki kushughulikia fedha za kanisa hilo zaidi ya mwenyekiti huyo.

UWAZI LAMSAKA MWENYEKITI
Baada ya kusikia madai hayo yote wiki iliyopita, Uwazi lilimtafuta Mchanuzi ili kusikia kutoka kwake kuhusu madai hayo ambapo kwa upande wake alikiri kuwepo kwa manenomaneno hayo.
Alisema wapo watu wachache wanaovumisha kwamba ana nyumba ndogo na taarifa hizo wamezieneza kila sehemu hadi kwa paroko wa parokia hiyo, akimaanisha Cyprian Kagaba.
Aliendelea kusema kwamba mwanamke anayedaiwa ni  nyumba ndogo yake alikuwa mke wake wa pili wa ndoa tangu mwaka 1993 lakini waliachana mwaka 2003 yeye alipojiunga na kanisa hilo.
Alisema kwa sasa amebaki na mke mmoja wa ndoa aliyemuoa mwaka 1970, hivyo aliyemuacha si mke wake tena.

KUHUSU MADAI YA KWENDA KWA NYUMBA NDOGO KILA MARA
Mwenyekiti huyo aliweka wazi kwamba ni kweli amekuwa akienda nyumbani kwa mwanamke huyo kwa sababu ya kuwaona watoto watatu aliozaa naye na si kukutana naye kimwili.
“Watu hao wanaonipiga vita wamewahi kunitegea hadi mwanamke ili nifumaniwe naye gesti lakini hawakufanikiwa. Hili suala la nyumba ndogo limeshafika hadi kwa Pengo wala si suala geni kwangu,” alisema mwenyekiti huyo.

VIPI KUHUSU KUMJENGEA GHOROFA?
“Si kumjengea, bali nilimuongezea kiasi cha fedha alizolipwa kama fidia na serikali wakati anahamishwa pale Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere ili kupisha upanuzi wa uwanja huo na nilifanya hivyo kwa sababu ana watoto wangu, ubaya uko wapi jamani? Mimi nilimuongeza fedha kidogo lakini nyingine zilikuwa za kwake.”
Kuhusu matumizi mabaya ya fedha, mwenyekiti huyo alisema si ya kweli kwa vile kila kitu kinajulikana kwa paroko na watu wengine wanaostahili kujua.

PAROKO KAGABA HUYU HAPA
Kwa upande wake, Paroko Kagaba alikiri kuwepo kwa uvumi kuwa mwenyekiti huyo ana nyumba ndogo. Akasema alishafanya uchunguzi na kugundua kuwa ni yule mwanamke aliyeachana naye wakati anajiunga na kanisa hilo.
Aliendelea kusema kwamba kwa upande wa fedha zipo salama na amekuwa akiwaita wajumbe wenye madai hayo na kuongea nao ili wawe kitu kimoja na waondokane na uvumi.
“Hivi karibuni tulikutana mapadri wanne wa kanisa hili la Tabata kujadili mambo hayo yaliyokuwa yakikua kwa kasi, niliwaambia lazima waumini waachane na uvumi,” alisema paroko huyo.

AONAVYO MHARIRI
Kwa mujibu wa imani ya Kikristo, mwanaume anatakiwa kuoa mke mmoja tu, hivyo Mchanuzi ili awe muumini safi wa kanisa hilo aliamua kufuata sheria za imani hiyo kwa nia njema kabisa kwa kumuacha mke wa pili licha ya kuzaa naye watoto watatu. Ni maamuzi magumu lakini sahihi.
Share:

Friday, May 24, 2013

AIBU: MCHUNGAJI ATEMBEZWA UCHI HADI KANISANI KWAKE BAADA YA MKEWE KUMFUMANIA NA MWANAKWAYA LIVE..!!

Mtumishi mmoja wa Mungu amejikuta akipata aibu ya mwaka si tu mbele za Mungu bali hata kwa mkewe pamoja na mashuhuda wengine baada ya mkewe kumfumania ‘live’ kitandani akifanya mapenzi na mwana kwaya wa kanisa lake huko Kisumu nchini Kenya.
 
Habari zilizoripotiwa na mtandao wa Kenyan-Post zinasema msichana huyo mweye miaka 23 amekuwa na mahusiano ya muda mrefu na pasta huyo kabla hawajabambwa.
 
Kisa hiki ni kama movie ambazo tumezoea kuziona zenye story line ambayo unaweza kutabiri mwisho wake.


 Kwa mujibu wa mtandao huo, ile ‘siku ya 40’ mke wa pasta huyo alikuwa anatarajia kusafiri kwenda nyumbani kwao kusalimia wazazi wake hivyo mumewe alimsindikiza mpaka kituo cha basi, lakini alionekana kuwa mtu mwenye haraka na kumwambia mkewe kuwa siku hiyo ana mkutano muhimu hivyo anapaswa kuwahi. Baada ya kumfikisha kituoni aligeuza gari kwa haraka na kuondoka.


Huku nyuma mke wa pasta kwa bahati mbaya (upande wa pasta) na bahati nzuri (upande wake) aligundua kuwa amesahau zawadi aliyokuwa amemnunulia mama yake mzazi ambaye ndio anaenda kumsalimia hivyo ikabidi airudie nyumbani kisha asafiri na basi litakalokuwa linafuata.
 
Alipofika nyumbani anapoishi na mumewe alishangaa kukuta mlango haujafungwa kwa nje na huku anakumbuka walipoondoka waliufunga hivyo akahisi huenda wamevamiwa mchana kweupe, alipojaribu kuusukuma ulikuwa umefungwa kwa ndani ndipo alipoomba msaada wa majirani wakavunja kitasa na kuingia ndani.
 
Mama huyo alipigwa na butwaa kwa kile alichokikuta ndani baada ya kumkuta msichana anayemfahamu kuwa kiongozi wa kwaya ya kanisani la mumewe wakiwa uchi wa mnyama katika kitanda chake na mumewe.

Maamuzi aliyochukua ni kuwavamia kitandani na kuzitupa nje kupitia dirishani nguo zao wote lakini kwa bahati mbaya msichana aliyemfumania alifanikiwa kukimbia na kumuacha pasta mwenyewe. 
 
Huwa wanasema hasira ni hasara na maamuzi ya hasira hugeuka majuto baadae, baada ya mmbaya wake kukimbia aliamua kumvuta mumewe (pasta) akisaidiwa na watu wengine  akiwa uchi wa mnyama na kumtembeza mbele ya umati wa watu mpaka katika kanisa analotoa huduma pasta huyo kwa lengo la kufichua mabaya yake.
 
Bahati nzuri alijitokeza mwanaume mmoja aliempatia shati lake ili ajisitiri.
Share:

Tuesday, May 21, 2013

"WAKRISTO MSIACHE KUSALI KWA KUOGOPA UGAIDI"....ASKOFU PENGO

Askofu wa Kanisa Katoliki,Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka waumini wa kanisa hilo kutoogopa kifo badala yake waendelee kwenda makanisani licha ya kuwapo kwa vitisho vya kushambuliwa.
Pengo alisema hayo jana katika Kanisa la Mtakatifu Joseph alipokuwa akitoa sakramenti ya kipaimara na aliwataka wasiwe na hofu lakini waendelee kumwamini Yesu Kristo kama Mwana wa Mungu.
“Tuendelee kwenda makanisani,kamwe tusiogope kuuawa,tuwe na imani kwamba Yesu Kristo ndiye mlinzi wetu na ndiye atuongozaye,”alisema Pengo.
Kardinali Pengo alisema hata kama vyombo vya dola vitakuwa vimeshindwa kuwalinda,waumini kamwe wasiache kwenda makanisani kwa ajili ya kuabudu.
Pengo aliwataka waumini hao kutolipiza kisasi kutokana na mauaji yaliyotokea hivi karibuni mkoani Arusha kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya Yesu Kristo.
“Wakristo kulipa kisasi ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya kikristo na sheria za nchi,” alionya Pengo.

Kauli hiyo imekuja baada ya watu watatu kuuawa kwa bomu na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa hivi karibuni katika Kanisa Katoliki,Parokia ya Joseph Mfanyakazi,Olasiti nje kidogo ya jiji la Arusha.
Mauaji hayo yalitanguliwa na kuuawa kwa Padri Evarist Mushi aliyeuawa Februari 17 wakati akielekea katika Kanisa la Mtakatifu Theresia,Zanzibar kuendesha misa.
Pia Desemba 25 mwaka jana,Padri Ambrose Mkenda alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi watu wasiojulikana wakati akisubiri kufunguliwa geti nyumbani kwake Zanzibar.
Pengo aliwataka waumini wote kuendelea kusali kwa imani yao na kwamba matatizo yanayojitokeza yasiwakatishe tamaa.
Alisema hata katika mafundisho, kuna mambo mengi ambayo yalifanywa na baadhi ya watu ili kumkatisha tamaa Yesu Kristo asitimize malengo yake lakini baadaye alishinda.
“Vivyo hivyo waumini yanayojitokeza hivi sasa yasitukatishe tamaa tuendelee na utaratibu wetu wa siku zote na tutashinda,”alisema Pengo.
Share:

Monday, May 20, 2013

WATU 15 WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUCHOMA KANISA TANGA....!!

POLISI inawashikilia watuhumiwa 15, wanaodaiwa kuchoma moto Kanisa la Bethania lililoko eneo la Donge katika Mkoa wa Tanga, Ijumaa iliyopita usiku.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe, alisema watuhumiwa hao walikamatwa usiku huo huo katika maeneo tofauti ya mji wa Tanga.
Massawe alisema polisi inawahoji watuhumiwa waliokamatwa, ili kubaini wahusika halisi wa tukio hilo, kabla ya kuwafikisha mahakamani.
Kwa mujibu wa Kamanda Massawe, Polisi pia inachunguza tukio jingine la kutaka kuchoma moto Kanisa la Miracle Revival, lililoko katika mji wa Makorola.
Usiku wa kuamkia juzi, watu wasiojulikana walijaribu na kuchoma moto makanisa mawili, banda moja la kuoneshea picha za video na banda la pombe za kienyeji, na kusababisha hofu ya uhalifu dhidi ya dini ya Kikristo kuenea miongoni mwa wakazi mkoani hapa.
Siku hiyo saa 8 usiku, Kanisa la Betham lililokuwa likitumika zamani, liliteketezwa kwa moto na baada ya hapo watuhumiwa waliingia ndani ya kanisa kubwa la sasa, na kuchoma moto vitambaa vilivyofunika madhabahu.
Pia, usiku huo huo saa 9, Kanisa la Miracle Revival lililopo eneo la Makorola, lilinusurika kuchomwa moto baada ya juhudi hizo kuzimwa na watu waliojitolea kuuzima, wakati ulipokuwa umeshawashwa kwenye nguzo za kanisa hilo.
Wakati huo huo, Polisi mkoani wa Mbeya, inamshikilia mkulima Emmanuel Mlagala (28) kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo Faustino Lulambo (55), katika eneo Madibila, Mbarali Jumatano iliyopita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (RPC), Diwani Athumani, alisema ugomvi huo ulitokea katika mashamba ya mpunga saa nne asubuhi, na Faustino alikufa kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Alisema kabla ya kifo, kuliibuka ugomvi baada ya Mlagala kutuhumiwa kuiba simu, ambayo thamani yake haijajulikana. Polisi bado wanaendelea kuchunguza chanzo cha tukio hilo.
Share:

Saturday, May 18, 2013

TANGA: MAKANISA MAWILI YACHOMWA MOTO....

Makanisa mawili yamechomwa moto usiku wa kuamkia leo huku bila mafanikio watu wasiofahamika wakijaribu kuteketeza kwa moto banda moja la kuoneshea picha za video.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Costantine Massawe alisema tukio la kwanza lililotokea majira ya saa 8 usiku katika Kanisa la Betham lililoko eneo la Donge ambapo wahusika waliteketeza kwa moto jengo la Kanisa dogo lililokuwa likitumika zamani na kisha kuingia ndani ya Kanisa kubwa la sasa na kuviwasha kwa moto vitambaa vilivyokuwa vimefunika madhabahu.

Massawe alisema:
Kanisa lililoteketezwa hapo lilikuwa la zamani ila sasa linatumiwa na waumini wa Betham kwa ajili ya kufundisha watoto lakini ibada zote zinafanywa kwenye jengo hilo jipya ambalo ndilo lililochomwa vitambaa vilivyokuwa vimefunika madhabahu.
Aidha, alisema taarifa za kuchomwa Kanisa hilo zilitolewa na Sauli Taminola mmoja wa waumini hao ambaye analala hapo Kanisani ambaye anadai alishtuka kutoka usingizini mara baada ya kuona moto ukiwaka madhabahuni ndani ya Kanisa.

Tukio jingine la usiku huo huo alisema liliripotiwa kuhusisha Kanisa la Miracle Revival lililopo eneo la Makorora majira ya saa 9 za usiku ambapo watu walidai walishituka usingizini na kuona moto ukiwaka kwenye nguzo za Kanisa hilo ndipo wakapiga kelele za kuomba msaada.
Mchungaji ambae anaishi jirani na kanisa alisema aliona watu wakiwasha moto magurudumu (matairi) ya baiskeli na kuyafunga kweney boriti za kanisa ili ziweze kuungua moto lakini baada ya kuwakurupusha jaribio hilo lilishindwa kwakuwa moto ulidhibitiwa na watu pasipo kuleta madhara makubwa
alisema Kamanda Massawe.

Akizungumzia klabu ya pombe za kienyeji iliyoteketea usiku huo alisema tukio hilo lilitokea katika eneo la Kwanjeka kwenye baa inayofahamika kama ‘Bongola’ na kudai kwamba chanzo ni shoti ya umeme.

Kamanda Massawe alisema tukio la nne limehusisha banda moja la kuoneshea mikada ya picha za video huko huko Kwanjeka ambalo nalo lilikaka kuteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana lakini jaribio lao halikufanikiwa.
Share:

SKENDO: SISTA FEKI WA KIKATOLIKI ANASWA KANISANI....AISHI NDANI YA NYUMBA YA MASISTA BILA KUJULIKANA...!!

AMA kweli dunia inazidi kwenda ukingoni! Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Phyllis Wanjiru Kamau (44), raia wa Kenya amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa madai ya kujifanya mtawa wa Kanisa Katoliki na alikuwa akiishi kwenye nyumba za watawa wa kanisa hilo zilizopo Ipogolo mjini hapa.
Tukio hilo lililowashangaza polisi, lilijiri Mei 13, 2013  ambapo baada ya kuwekwa chini ya ulinzi na kumpekua, polisi walimkuta na ‘dokumenti’ zilizozidi kutia shaka.
Sista Wanjiru alikamatwa na jeshi hilo kufuatia masista wenzake orijino kubaini kuwa yeye si miongoni mwa watawa kwa ki-Katoliki kwa sababu ya kushindwa kuishi maisha ya kitawa ndani ya nyumba.
“Sisi tulimpokea tukiamini ni mwenzetu, lakini kadiri tulivyokuwa tukiishi naye, alionekana siye. Masista wa Katoliki tunajuana kwa vitendo hata kama atakuwa anatokea nchi nyingine,” alisema mtawa mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Mtoa habari huyo alisema ukiachilia mbali kukiuka maisha ya kitawa lakini pia Wanjiru alionekana ni msiri kwa mambo mengi aliyokuwa akiyafanya, hali iliyozidi kuwapa wasiwasi wenzake.
“Mambo yake mengi yalionekana  ni ya sirisiri, hakuwa muwazi wa maisha yake ya nyuma wala kuanika historia yake kama wengine tunavyofanya. Alitia wasiwasi hata shule aliyosoma,” alisema sista huyo.


Habari zinadai baada ya masista ndani ya mjengo kumshtukia Wanjiru, walikwenda kuripoti polisi wakitaka mwenzao huyo akamatwe na kukaguliwa kwa umakini ili kuonesha uhalali wa utawa wake na uraia wa Tanzania.
Ndipo polisi walipomzukia na kumweka mtu kati ambapo awali alikiri yeye ni sista lakini baada ya kukaguliwa na kubanwa sana alionekana ni sista feki na pia si raia wa Bongo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, Afande Michael Kamuhanda alipoongea na paparazi wetu aliweka wazi kuhusu sista huyo.
Alisema kabila la mwanamke huyo ni Muwembu kutoka nchini Kenya na alikiri kuwa alidakwa na polisi akiwa katika nyumba za masista zilizopo Ipogolo mjini Iringa.
Aliongeza kuwa baada ya kumtia mikononi, mwanamke huyo aligoma katakata kutoa maelezo ya kina juu ya uingiaji wake nchini Tanzania licha ya kwamba nchi aliyotokea ipo Jumuiya ya Afrika Mashariki kama ilivyo Tanzania. Nchi nyingine zilizopo kwenye jumuiya hiyo ni Uganda, Rwanda na Burundi.
Kamanda Kamuhanda akaendelea kusema kuwa wakati wa kumpekua Wanjiru walifanikiwa kumkuta na baadhi ya laini za simu za makampuni mbalimbali ya simu ya ndani na nje ya Tanzania.
Mbali na laini za simu, pia alikuwa na hati za kusafiria (passport) mbili, moja ikiwa ni ya Afrika Mashariki yenye namba Ke. 020659 huku hati ya nyingine ikiwa na ya Kenya yenye namba A. 1790366.
Afande huyo akizidi kumuanika sista Wanjiru alisema katika hati hizo, ilionesha kuwa alitembelea Rwanda, Uganda na Tanzania ambapo siku za hivi karibuni alikuwa wilayani Tarime Mkoa wa wa Mara.
Katika hali ya kushangaza, akiwa anahojiwa sista huyo alianguka kama mtu mwenye ugonjwa wa kifafa, jambo linalowawia vigumu polisi kupata maelezo ya kina dhidi ya dhamira yake ya kuingia Bongo.
Kamuhanda ameitaka jamii kuwa makini na wageni mbalimbali, huku akiwaasa kuacha tabia ya kuwaamini watu kwa muonekano wao, kutokana na mwanamke huyo kutumia njia hiyo ambayo inamfanya kila mtu kumuamini.
Share:

Friday, May 17, 2013

CD ZA UAMSHO NA ZILE ZA SHEIKH ILUNGA ZAPIGWA MARUFUKU....!!


Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar inayoongozwa na Dr Shein na Makamu  wake Maalim Seif kupitia Jeshi la Polisi wamepiga marufuku rasmi CD  zote za mawaidha ya Kiislam za UAMSHO,MUJAHID ABOUD ROGO na SHEIKH ILUNGA.
 

Agizo hilo lilitolewa na OCD  wa  zamani Murtad MKADAM ambae kwa  sasa yupo ofisi kuu ya polisi kitengo cha madawa ya kulevya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif.

Alisema cd hizo za kiislam ni chanzo cha uvunifu wa amani hapa nchini na ndio zinazosababisha uchochezi baina ya dini ya ukiristo na uislam.


OCD alibainisha kuwa mpaka sasa wameshawakamata watu kadhaa wanaojihusisha  na  kuuza cd hizo na kuwaonya wale wote ambao huweka kuzisikiliza maana watachukuliwa hatua kwani serikali ina mkono mrefu.
...



Akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa kwamba waliowakamata hawawaoni kuwa wamewadhulumu kwa kufanya biashara halali ya uzaji cd, Ocd alijibu cd zile za mawaidha ni Haram wala sio riziki ya halali kwa upande wa serekali kwani zinapelekea uvunjifu wa Amani katika nchi.
Share:

Monday, May 13, 2013

WAISLAM NA WAKRISTO WAGOMBEA KUCHINJA NG'OMBE MSIBANI HUKO GEITA...!!

*Waislamu, Wakristo wabishana nani achinje ng’ombe
*Washindwa kuelewana, ng’ombe akaachwa yakapikwa maharage

WAISLAMU na Wakristo katika Kijiji cha Katoro, kilichopo Kata ya Katoro, wilayani Geita, Mkoa wa Geita, juzi nusura wazichape msibani baada ya kutokea malumbano ya nani achinje na nani asichinje ng’ombe msibani hapo.

Tukio hilo lilitokea siku hiyo saa nne asubuhi kwenye msiba wa marehemu Monica Zacharia (26), ambaye alikuwa mke wa mfanyabiashara wa mjini Katoro, Elias Peter. Mwanamke huyo alifariki Mei 9 mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, muda mfupi baada ya kujifungua.

Hali ya kutoelewana ilianza baada ya wafanyabiashara wa mjini Katoro, ambao ni marafiki wa mume wa marehemu, kufika msibani hapo wakiwa na ng'ombe kwa ajili ya kitoweo cha waombolezaji.
Share:

Saturday, May 11, 2013

"WAKRISTO MSILIPIZE KISASI"...ASKOFU PENGO.


WAKRISTO wametakiwa kutolipiza kisasi juu ya maovu yaliyofanywa na kikundi cha watu kwa kurusha bomu kanisani na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine 66 kujeruhiwa. Tukio hilo lilitokea Jumapili wakati wa uzinduzi wa kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi lililoko Olasiti jijini hapa.
Share:

BAADA KUTOKA NJE YA GEREZA SHEIKH PONDA ANENA MAZITO, ADAI MIKAKATI YA KUKAMATWA KWAKE ILIPANGWA MUDA MREFU...!!



SIKU moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam, kumwachia na kumweka chini ya uangalizi wa mwaka mmoja Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, jana aliibuka na kusema umefika wakati wa Waislamu kufanya uamuzi mzito.

Akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu, baada ya swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Mtambani, Dar es Salaam, Sheikh Ponda, alisema hatua ya yeye kuwekwa ndani kamwe haitamkatisha tamaa na kurudi nyuma katika mapambano ya madai ya Waislamu nchini.

Alisema kutokana na hali hiyo, kwa muda mrefu Waislamu wamekuwa wakinyanyaswa kinyume cha sheria, wakati wana madai ya msingi ndani ya taifa lao.
Share:

Friday, May 10, 2013

"NDUGU ZETU HAWAJAHUSIKA NA SHAMBULIZI LA BOMU LA KANISANI JIJINI ARUSHA".....WAARABU



Taarifa za kuaminika toka kwa mwanasheria

Jambo hilli limefanyiwa fabrications kadhaa, kwa uchache tu;

Ndg. zetu hawa sio kweli kama ilivyoripotiwa kwamba:
1). Walifika jumamosi na kesho yake jumapili litakatokea tukio hilo,
2). Na si kweli eti kuwa baada ya tukio eti wakaanza kuondoka kupitia Nairobi road na hivyo kukamatwa wakiwa njiani wanaondoka kuelekea Kenya kupitia Namanga.

UKWELI ULIVYO KWA MAELEZO YA NDUGU ZAO:

WENZETU HAWA WASAUDI WAWILI WALIKUJA SIKU TATU KABLA YA TUKIO HUSIKA KWA MATEMBEZI YAO BINAFSI AMBAYO MARA KWA MARA HUWA WANAYAFANYA KUJA KUWATEMBELEA NDG. ZAO HAPA TZ ARUSHA KAMA MTU MWINGINE ANGEWEZA KUFANYA KIMATEMBEZI.

WALIPOFIKA WALIKUWA WAKILALA KATIKA HOTELI MOJA "B" (JINA NALISITIRI) ILIYOPO ENEO LA KITUO KIKUU CHA MABASI YAENDAYO MIKOANI HAPA ARUSHA AMBAYO INAMILIKIWA NA MCHAGGA MMOJA MKRISTO, SIKU YA TUKIO BAADA YA KUTOKEA, MMILIKI HUYO WA HOTELI HIYO ALIPIGA SIMU POLISI AKIELEZA KWAMBA HOTELINI KWAKE WAMEFIKIA WATEJA AMBAO ANA SHAKA NAO HIVYO POLISI WALIFIKA NA KUWAKAMATA HAO WAWILI HAPO HAPO HOTELINI NA KUWATAFUTA WENYEJI WAO WAWILI "X" NA "Y" NA WOTE KUKAMATWA NA KUPELEKWA KITUO KIKUU CHA POLISI HADI LEO.

My take:
Suala hili linageuzwageuzwa na watu humu ndani pamoja na mtaani ili mradi kuonekana tu waarabu hawa wanakosa. Ni kwanini watu tunashindwa kumuelewa hata kiongozi mkuu wa katoliki Tanzania ndg Kadinali Pengo ambae kwa maneno yake ameseme lisihusishwe na dini bali ni mgogoro wa ndani ya 'KANISA LENYEWE'

Kwanini hatuwabebeshi mzigo huu waswahili wenzetu ambao dalili zaonyesha wazi kuwa wametenda kosa hilo mfano Victor Ambrose?
Ni wazi bado tunaelement za chuki dhidi ya hawa waarabu na dini yao pia. Ni vyema tungojee mwisho wa uchunguzi polisi watasemaje kuliko kulijadili suala hili kwa kuegemea upande mmoja(bias).
Share:

PONDA AANZA UCHOCHEZI TENA....ANATAKA SERIKALI IANZE KUUA WAKRITO NA AMEDAI NECTA HUWAFELISHA WAISLAMU...


Wakizungumza kwenye msikiti wa mtambani Kinondoni mara baada ya swala, Sheikh ponda na ustaadh mukadam  wameapa kupambana hadi dakika ya mwisho. 
Mukadam amemsifia Allah kwa kuwapa adhabu ya ugonjwa,watu kadhaa akiwemo  mkubwa mmoja  alie mahututi Afrika kusini(wanadai  eti alihusika kuwatengenezea mashtaka),na afisa mwingne wa jeshi kufarik ajalini baada ya kuwanyanyasa selo!
KAULI ZA SHEIKH PONDA.

Alitamka  kuwa :"Nitapambana hadi mwisho' huku watu wakisema takbir alah akbar! Amesema Wakristo wanapendelewa na serikali. Serikali ilisema aliekojolea kuran ni mtoto,wakati yeye kawakuta watoto jela akiwemo wa miaka 10,aliyekwapua mkoba.,ila yule mkristo wa miaka 14 serikali ilisema mtoto na haikumchukulia hatua zozote!


Pia kasema ana CD zikionyesha jinsi serikali inavyoua na kupanga kukandamiza uislamu. Kampongeza sana Zitto kabwe kwa mchango wake wa kutetea uislamu bungeni na kamponda yule aliepeleka cd alizoita za uchochezi bungeni! 


Karudia tuhuma za kuwa NECTA kuna udini na Waislamu wanafelishwa! Kasema serikali inapendelea na kuendeshwa na wakristo. Pia kuhusu bomu la Arusha kasema, wamekamatwa waarabu ,mbona hawajakamata wazungu? Anasema huo ni mpango wa kuonea waarabu na uislamu!

Ponda  kasema wakristo hajawahi kuuawa na serikali,ila waislamu tu ndo wanauawa! Mwembechai waliuawa, Pemba waliuawa. Anadai hata Pemba Waislamu waliuawa na serikali ikitumwa na Kanisa! 



Amehoji,mbona hatujawahi kusikia mchungaj au padri kauawa?kasema pemba kuna helcopter zilikua zinalipua majahazi ya waislamu(wakiwa baharini) wakati wanakimbilia Mombasa naTanga.!

Pia kasema,nchi hii hakuna udini,ila kuna mapambano ya waislamu kudai haki zao na redio iman imefungiwa kuwaonea waislamu wasipate pakusemea

Share:

Thursday, May 9, 2013

HUYU NDIYE GAIDI ALIYERUSHA BOMU KANISANI, AFUNGA NA KUNENA MANENO MAZITO....SOMA HAPA..!!

 
Kijana aliyemkimbiza hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha akiwaelezea wananchi ilivyokuwa.


ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ameibuka.
Kijana huyo ambaye wakati akizungumza na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari jijini Arusha juzi alisahau kutaja jina lake, alisema kuwa shughuli ya kumnasa mtuhumiwa huyo haikuwa lelemama hata kidogo.
Alisema siku ya tukio baada ya bomu hilo kulipuliwa kanisani hapo, yeye alimwona mlipuaji huyo hivyo akaungana na watu wengine kumkimbiza.
“Mtuhumiwa alikuwa akikimbia ujue, sisi tulimkimbiza bila kuogopa kama ana mabomu mengine kwenye mfuko. Alipoona hatukati tamaa, alifika kwenye shamba la miwa akajilaza, lakini mbwa waliokuwa na sisi walitusaidia sana,” alisema shujaa huyo.
Aliendelea kusema kuwa walipomdaka mtuhumiwa huyo walimkuta na mfuko wa rambo,  walipochungulia ndani yake walishtuka, kumbe alikuwa na mabomu yaliyosalia!
Hata hivyo, alisema yeye na mabomu yake hawakumwachia na dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo hilo wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumuua ndipo polisi walipofika eneo hilo na kumchukua mtuhumiwa huyo kwenda naye kituoni.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kijana huyo amekuwa staa ghafla, hivyo wakaitaka serikali kumfikiria kwani ameonesha kitendo cha kishujaa.
“Huyu kijana amekuwa staa ghafla aisee, kitendo alichokifanya ni cha kishujaa, si rahisi, serikali ingemfikiria kwa lolote,” alisema mtu mmoja aliyejiita Massawe na kuungwa mkono na wenzake.
Share:

PICHA ZA TUKIO ZIMA LA HUKUMU YA PONDA TOKA MAHAKAMA YA KISUTU....!!

Akitetra jambo na baadhi ya watu!
Akihojiwa na mmoja wa waandishi wa habari!
Mhadhiri Maarufu wa Kiisilamu Sheikh Habibu Mazinge (suti nyeusi) akimlaki Sheikh Ponda mara baada ya kuachiliwa huru.

Ponda akizungumza na waandishi wa habari.
"Kuna utaratibu umeandaliwa na jumuiya na taasisi za kiisilamu Tanzania tutawaita tutazungumza kwa pamoja lakini kikubwa ninachoweza kusema kwamba tumeshuhudia uonevu na dhulma tunayofanyiwa waisilamu nanyie ni mashuhuda hapa leo." Alisema.


Safari ikaanza!

Akaingia kwenye gari!

Msafara ukavamiwa na wafuasi baada ya dereva wa garilake kusimamisha awasalimie wafuasi hao jambo ambalo polisi walikuwa hawalitaki na kuzua mabishano mazito lwenye mataa ya Maktaba Squire. 

Wafuasi wakajimwaga barabarani!

Wafuasi wakivamia gari kumsalimia baada ya dereva wagari hilo kulisimamisha huku polisi wakimvamia aliondoe gari hilo haraka.
Waliufukuza msafara huo hadi pale ulipotokomea!
Msafara uliendelea kukimbizwa hadi walipotokomea mbali kwa spidi ya kuwakimbia.
Waumini wa dini ya Kiisilamu ambao walijitokeza kkusikiliza hukumu ya kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49, wakimbeba juu juu mmoja wa wafuasiwake ambao walishtakiwa pamoja mara baada ya kushinda kesi hiyo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.

HATIMAYE katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili. ...


Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.
Mara baada ya kutolewa hukumu hiyo mahakamani hapo pali ibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo.

 
Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
 
1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya ardhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo la umiliki.
 
2.Upande wa Serikali haukuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
 
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
 
4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.
 
5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. 

Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu.

Tumewashinda!
Furaha!
Machozi yalitiririka, Jazba na ahawali zikapanda!
Safari ya kuelekea Mtambani Kinondoni Ikaanza.


Mmoja wa ndugu wa mtuhumiwa akilia baada ya kumkumbatia nduguyake kutokana na kushinda kesi hiyo.
"Pole ndio safari ya kusaka haki" Ndugu alisikika kabla ya kulia.
Waliopo kwenye majengo ya karibu wakatoka nnje kushuhudia!

Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari kwa lolote litakalotokea.

Waandishi nao walifanya mahojiano na baadhi ya washtakiwa na ndugu wa washtakiwa hao.
Ulinzi wa Ponda wakati wa kuondoka mahakamani hapo baada ya kuachiliwa.
Msafara wa ulinzi ukiondoka Kisutu!
Kama kawaida walikuwepo pia!
Share:

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger