MWIMBAJI chipukizi katika muziki wa Injili nchini, Mary Msigwa,
amelalamikia wasanii wenye majina makubwa katika muziki huo
kutowathamini, vyombo vya habari na wadau wa muziki huo pindi wanapotaka
msaada kwa ajili ya kukuza muziki wao.
Msigwa alilalama kwamba nyimbo za wasanii chipukizi hazipewi nafasi
ya kuchezwa kwenye redio na runinga mbalimbali bila sababu za msingi.
Mary alisema changamoto nyingine zinazowakabili waimbaji wachanga ni
kukosa fedha kwa ajili ya kurekodia, kushindwa kujitangaza kiasi kwamba
wanashindwa kutambulika kwa jamii.
“Wasanii chipukizi hatuthaminiwi na hii imesababisha baadhi ya
wenzetu kushindwa kuendelea na huduma hii kwani hata kama ukifanikiwa
kurekodi kwa kujibana shida inakuwa kwa watangazaji wa redio na
televisheni ambao huwa hawazipi nafasi nyimbo zetu na hii inasababisha
tushindwe kufahamika kwenye jamii,” alisema mwimbaji huyo.
0 comments:
Post a Comment