Monday, May 13, 2013

WAISLAM NA WAKRISTO WAGOMBEA KUCHINJA NG'OMBE MSIBANI HUKO GEITA...!!

*Waislamu, Wakristo wabishana nani achinje ng’ombe
*Washindwa kuelewana, ng’ombe akaachwa yakapikwa maharage

WAISLAMU na Wakristo katika Kijiji cha Katoro, kilichopo Kata ya Katoro, wilayani Geita, Mkoa wa Geita, juzi nusura wazichape msibani baada ya kutokea malumbano ya nani achinje na nani asichinje ng’ombe msibani hapo.

Tukio hilo lilitokea siku hiyo saa nne asubuhi kwenye msiba wa marehemu Monica Zacharia (26), ambaye alikuwa mke wa mfanyabiashara wa mjini Katoro, Elias Peter. Mwanamke huyo alifariki Mei 9 mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, muda mfupi baada ya kujifungua.

Hali ya kutoelewana ilianza baada ya wafanyabiashara wa mjini Katoro, ambao ni marafiki wa mume wa marehemu, kufika msibani hapo wakiwa na ng'ombe kwa ajili ya kitoweo cha waombolezaji.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger