Showing posts with label maajabu. Show all posts
Showing posts with label maajabu. Show all posts

Tuesday, October 15, 2013

MIUJIZA:MTOTO ALIYEKUWA AMEFARIKI AOMBEWA NA KUFUFUKA....!!


Mtoto aliyefufuka (katikati) akiwa ameshikwa na Mch. Gwajima (kulia) na Mch. Costa (kushoto)

Ni jumapili tulivu katika viwanja vya kanisa jipya la Ufufuo na Uzima jijini Arusha; ambapo
Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Tanzania, Mch. Josephat Gwajima ameendelea na ziara yake mkoani humo kwa kuwafundisha viongozi wapya wa masomo ya kumtumikia Mungu maarufu kama Potential shepherd. Mwisho wa Ibada ya Asubuhi ambayo ilitawaliwa na mafundisho zaidi ilifungua pazia kwa ibada ya jioni ambayo ilikuwa ni fursa kwa wale ambao hawakuweza kuwepo asubuhi nao kushiriki.

Majira ya saa kumi kamili, sifa zilivuma na baadaye kufuatiwa na ukaribisho wa Mch. Gwajima kutoa neno la Uzima. majira ya saa kumi na mbili kasoro; akaingia mama mmoja katikati ya ibada akiwa amembeba mwanaye ambaye kwa muonekano wa awali alikuwa amelegea mwili wote yaani amekufa.
Mama huyo ambaye alikuwepo katika mafundisho ya asubuhi na kujiunga na mafundisho hayo ya potential shepherd; aliendelea kusema kuwa baada ya kuona mwanaye hapumui wala mapigo ya moyo hayasikiki hakuona msaada wa haraka zaidi ya kumkimbiza kanisani hapo Ufufuo na Uzima.


Aliingia kanisani wakati Mch. Josephat Gwajima akiwa anahubiri hivyo kupokelewa na Mchungaji Msaidizi aitwaye Yeconia Bihagaze ambaye alimuombea mtoto huyo palepale na muda mfupi uliofuata mtoto alifufuka kutoka kwa wafu. Mungu ameendelea kudhihirisha neno la Mchungaji Josephat Gwajima ndani ya jiji la Arusha hali inayosababisha maelfu ya watu kuingia na kutoka katika viwanja hivyo kwaajili ya maombezi.


Jackson Benty akiimba katika ibada kanisani hapo.
Hata hivyo GK ilipotaka kupata maelezo zaidi kuhusiana na mambo yalivyokuwa mpaka mtoto huyo kufikishwa madhabahuni, mwanahabari wetu kutoka Ufufuo hakupata nafasi ya kukutana na mama huyo kwa maelezo zaidi kutokana na mwanahabari wetu kutingwa na kazi nyingi za media kanisani hapo.


Mchungaji Gwajima akifundisha kanisani hapo. Picha na shuhuda zaidi tembelea

mwakasegebibiliablog
Share:

Monday, October 14, 2013

VIDEO: MAITI YAGOMA KWENDA KUZIKWA MPAKA BAADA YA KUBEMBELEZWA.....



Share:

Tuesday, October 8, 2013

MAAJABU MTOTO ALIYEFUFUKA....!!


TUKIO la mtoto Shaaban Maulid, 16, aliyefariki dunia miaka mwili iliyopita kabla ya mwaka huu kuonekana (kufufuka), limeendelea kutikisa baada ya maajabu mengine kujiri.
Shaaban, alifariki dunia na kuzikwa Januari, 2011 lakini Septemba 30, mwaka huu, alionekana akiwa hai, ingawa alikuwa akizungumza kwa taabu.
Kwa vile kufufuka kwa Shaaban ni jambo lililoacha wazi midomo ya wengi hususan waliohudhuria mazishi yake miaka miwili iliyopita, ilibidi kaburi alilozikwa lifukuliwe ili ndani yake ijulikane kuna nini.
Tamko la kufukua kaburi la Shaaban ni azimio la kifamilia, hasa baada ya ndugu na majirani kupendekeza, kwani kufufuka kwake, kulivuruga vichwa vingi, wapo walioamini inawezekana, ila wengine wakipinga kwamba mtoto huyo aliyeibuka sasa ni mzimu tu.

MAUZAUZA KABURINI
Shaaban alizikwa kwenye eneo la nyumba ya baba yake, Maulid Shaaban, kwa hiyo haikuwa shida kulipata kaburi, kwani familia nzima na hata majirani wanalijua kwa sababu walishiriki kumzika.
Jumatano iliyopita, shughuli ya kufukua kaburi la Shaaban ilifanyika. Kazi hiyo ilianza saa 2 asubuhi chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi, kabla ya kukamilika saa 4.30 asubuhi.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa kipindi chote ambacho ufukuaji ulifanyika, mauzauza mengi yalitokea, hivyo kusababisha taharuki na hata watu wengine kutimua mbio.
Wakati shughuli ya ufukuaji ikiwa mbichi kabisa, alitokea mbwa kutoka kusikojulikana ambaye alifika na kuanza  kujigalagaza juu ya kaburi hilo, huku akibweka.
Hali hiyo, ilitafsiriwa na wengi kwamba mbwa huyo alikuwa hataki kaburi hilo lifukuliwe, ingawa baadaye aliondoka taratibu akibweka na kutokomea kusikojulikana.
Saa 2.30 asubuhi wakati ufukuaji ukiendelea, mwanamke jirani anayeitwa Sharifa Hitler, alianguka na kupoteza fahamu, kabla ya kuzinduka dakika 20 baadaye, kufuatia jitihada za kumuwekea kipande cha sabuni mkononi.
Baada ya kuzinduka, Sharifa alisema kuwa alisikia kichwa kinakuwa kizito, akapatwa na kizunguzungu kisha akapoteza fahamu.
Saa 3.05 asubuhi, tukio lingine litokea, kwani kipindi kaburi linafukuliwa, ukuta wa nyumba ya baba yake Shaaban, nao ulianguka na kutoa sauti yenye mshindo mkubwa.
Sauti hiyo iliwatisha wengi, kwa hiyo watu walikimbia kwa kutawanyika, kila mmoja akishika uelekeo wake.
Kuanguka kwa ukuta huo, kulifanya kazi ya kufukua kaburi isitishwe kwa muda ili kutawanya kifusi cha ukuta wa nyumba, kuhakiki kama kuna mtu aliangukiwa na kufunikwa.
Hata hivyo, baadaye iliamriwa mambo yote mawili yafanyike kwa wakati mmoja, baadhi wahusike na utawanyaji wa kifusi na wengine waendelee kufukua kaburi ili kwenda na muda.

MAAJABU NDANI YA KABURI
Kule kwenye kifusi, ilionekana hakukuwa na tatizo lolote lakini kwenye kaburi baada ya ufukuaji kukamilika, mambo yaliyoonekana ni haya;
Mosi; kwa mila za Kiislam, ndani ya kaburi, kuna sehemu ndogo ambayo huchimbwa kulingana na kimo cha marehemu, kisha kulazwa ndani yake.
Sehemu hiyo huitwa mwanandani, kwa hiyo baada ya kufukua, badala ya kukuta mwili, wafukuaji walikutana na chungu kikubwa.
Pili; kile chungu kilikuwa kimefunikwa na mifuko aina ya viroba. Tafsiri ya wengi walioshuhudia tukio hilo ni kwamba sanda aliyozikwa nayo Shaaban miaka miwili iliyopita, ndiyo iliyogeuka kiroba.
Tatu; ndani ya chungu kulikuwa na mifupa ya kiumbe cha ajabu, kwani kwa muonekano haifanani na ya binadamu wala mnyama yeyote anayefahamika, kwani ilikuwa ni midogomidogo mno.
Nne; kulikuwa na madawa yenye umbo la kimimika, rangi nyeusi.
Dunia Mrisho ambaye alikuwa shuhuda wa tukio hilo na alikuwepo miaka miwili iliyopita wakati Shaaban akizikwa, alisema kuwa yaliyoonekana ndani ya kaburi hilo, yamewashangaza wengi.
“Huyu mtoto tulimzika kwa heshima zote za Kiislam na mwili wake ulikuwa kwenye sanda, hii mifuko ndani ya kaburi imetoka wapi? Tunashangaa pia kukuta chungu ndani ya kaburi na kina mifupa na yule mbwa aliyetokea na kutokomea ni wa nani? Hapa kuna kitu,” alisema Dunia ambaye ni mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

KWANI SHAABAN ALIKUFAJE?
Januari Mosi, 2011, Shaaban akiwa na afya njema kabisa, aliondoka nyumbani kwao asubuhi kwenda kuchunga mbuzi kwenye malisho.
Tangu siku hiyo, Shaaban hakuonekana tena, ingawa jitihada za kumtafuta zilifanyika kwa nguvu sana kwa usimamizi wa jeshi la polisi.
Katika eneo la malisho, mbuzi alioondoka nao Shaaban walionekana wakiwa katika idadi kamili lakini mtoto huyo ndiye hakuonekana.
Siku nne baadaye, Shaaban alikutwa akiwa amefariki dunia na mwili wake ulikutwa ndani ya kisima katika Mtaa wa Mbugani, Geita.
Baada ya kujiridhisha kwamba amefariki dunia na wazazi wake kumtambua kwamba ni mtoto wao, alizikwa katika makaburi ya eneo la nyumbani kwao.

SHAABAN ALIFUFUKAJE?
Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mama mzazi wa mtoto huyo, Aziza Ramadhani, 45, ambaye alisimulia jinsi alivyoweza kumuona mtoto wake huyo akiwa hai.
“Ilikuwa Septemba 30, mwaka huu, nilikuwa naelekea sokoni kwenye shughuli zangu za kuuza mbogamboga. Ilikuwa saa 1.30 asubuhi, nikiwa Mtaa wa Nyankumbu, nilikutana na mwanangu Shaaban.
“Nilishtuka na sikuamini haraka. Nilimwita kwa jina lake, mwanangu Shaaban ni wewe? Akaniitikia kwa kutikisa kichwa. Hakuweza kutoa sauti vizuri, alikuwa anazungumza kwa taabu.
“Nilikwenda kumshika mkono kuhakikisha kuwa ni binadamu au mzimu huku nikiwa siamini kabisa kuwa ni yeye. Nilipoona kuwa ni yeye nilimpigia simu mume wangu, akaja tukamchunguza vizuri na kubaini kuwa kweli ni mtoto wetu Shaaban.
“Ni maajabu kabisa, sisi tuliamini amekufa na tukamzika miaka miwili iliyopita. Kweli hii dunia ni ya maajabu,” alisema Aziza ‘Mama Shaaban’.
Aliendelea kusema kuwa mtoto huyo alikuwa na alama ya kinundu kwenye paji la uso na mguuni ambalo ni kovu iliyosababishwa na kuchomwa na mwiba.
Aliongeza kuwa vilevile Shaaban alikuwa na mwanya uliofanana na wa baba yake ambapo huyu alama zote hizo anazo.
Alisema kuwa walikagua alama hizo kipindi cha kuutambua mwili wake pale alipofariki dunia na kujiridhisha ndipo walipomzika.
“Baba yake alipokuja eneo la tukio, tulimpeleka hospitali kwa sababu hali yake haikuwa nzuri, mpaka sasa bado yupo hospitali akitibiwa,” alisema Aziza.

SHULENI KWAKE NAKO
Mtoto huyo aliyevuta hisia za watu wengi mjini Geita, amethibitishwa na walimu wake katika shule aliyokuwa anasoma kwamba ndiye aliyezikwa.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mwatulole, Geita, Joseph Nungula, alisema kuwa amemwangalia Shaaban na kujiridhisha ni mwanafunzi wake yuleyule ambaye miaka miwili iliyopita zilitolewa taarifa za kifo chake na baadaye kuzikwa.
“Nimemtambua mtoto huyo kwa sura na alama, hasa ya usoni na alikuwa na mahudhurio mazuri shuleni. Pia maendeleo yake kitaaluma yalikuwa mazuri,” alisema mwalimu huyo huku akiungwa mkono na wanafunzi waliokuwa wanasoma na Shaaban.

BABA ANAZUNGUMZA
Maulid Shaaban ‘Baba Shaaban’, alisema kuwa ni kweli kabisa mtoto wao alitoweka na alipatikana akiwa ameshafariki dunia.
Aliongeza, mwili wa Shaaban ulikutwa ndani ya kisima cha maji, hivyo walitoa taarifa polisi kisha waliruhusiwa kuchukua mwili.
“Daktari alithibitisha alimkagua na kujiridhisha kwamba ameshakufa. Tukaamua kumzika kwenye kiwanja cha nyumbani kwangu, Kitongoji cha 14, Kambarage, hapa Geita.
“Shughuli zote za matanga tulifanya, baada ya hapo hatukuwa na wazo la Shaaban kurudi duniani. Leo hii kila kitu tunaona ni maajabu, Shaaban huyuhuyu ambaye tulimzika amerudi duniani,” alisema Maulid.

DAKTARI AELEZA
Shaaban amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, akifanyiwa uchunguzi zaidi na matibabu zaidi kwa sababu bado hajaweza kuzungumza vizuri.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Geita, Dk. Adamu Sijaona anayemtibu mtoto huyo, alisema kuwa tayari wazazi wake wameshachukuliwa sampuli na kuhifadhiwa kwenye maabara na mifupa iliyokutwa kaburini imechukuliwa kwa uchunguzi wa DNA.
“Hali yake inaendelea vizuri hasa katika kutamka maneno ikilinganishwa na wakati anafikishwa hospitalini kwa mara ya kwanza kwa sababu alikuwa hawezi kutamka neno hata moja,” alisema Dk. Sijaona.

OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
Mchunguzi kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Ziwa, Lukas Nduguru, aliliambia gazeti hili kuwa wamechukua vipimo vya wazazi na mtoto pamoja na baadhi ya mabaki ya mifupa iliyokuwa kwenye kaburi hilo kwa ajili ya vipimo vya vinasaba (DNA) ili kubaini mwili wa nani ulizikwa kwenye kaburi hilo.
“Ofisi ya mkemia mkuu wa serikali ilipata taarifa za huyo mtoto aliyezikwa mwaka 2011 kwamba ameonekana akiwa hai, kwa hiyo majibu ya vinasaba yatatoka ndani ya siku 14 au mwezi mmoja.
“Tuna changamoto za kukatika umeme mara kwa mara, kwa hiyo ndani ya kipindi hicho tutakuwa tumekamilisha,” alisema Dk. Ndunguru.

NENO LA KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paulo, mbali na kuthibitisha kufukuliwa kwa kaburi hilo kwa kibali maalumu cha mahakama, alisema mtu hawezi kufa kisha kufufuka kwa hiyo jeshi la polisi haliamini kama mtoto aliyezikwa ni yeye.
“Unajua hatuna imani na hili isipokuwa tunasubiri majibu ya uchunguzi wa watalaamu kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa serikali,” alisema Paulo.

NI TUKIO LA PILI GEITA
Tukio kama hilo ni la pili kutokea katika Wilaya ya Geita katika kipindi kisichozidi miezi mitano ambapo Aprili 12, mwaka huu, mwanamke aliyetambulika kwa jina la Flora Onesmo, 45, aliyefariki dunia Februari 28, 2008 katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kisha kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya, Kata ya Butundwe, alionekana akiwa hai.
Flora, alikutwa hai Aprili 12, mwaka huu, akiwa ameketi nje ya nyumba ya dada yake aitwaye Monica James, anayeishi Kijiji cha Kasamwa, Geita.

UWAZI LIPO KAZINI
Uwazi bado lina kazi ya kufanya kuhusiana na Shaaban na Flora, yapo maswali mengi hayajajibiwa, kwa hiyo lipo kazini likiibuka litakuwa na mengine mengi ambayo pengine yatakuwa mazito zaidi. MHARIRI.

Share:

Tuesday, May 21, 2013

MAAJABU YA MTOTO ALIYETESWA NA WAZAZI WAKE MBEYA NA KUFUNGIWA NDANI MIAKA 2....!!

Moto Joshua akiwa amekaa uwani kwenye nyumba  yao huku wazazi wake wakiwa wamemwacha peke yake toka asubuhi bila ya kumpatia chakula mtoto huyo tumemkuta katika hali mbaya sana kwani tunemkuta amejisaidia haja ndogo na hana hata nguo za kubadilisha.
Kwa ujumla mtoto Joshua hata kutembea hawezi kwani simama yake ni ya kutetemeka migu tu 

Hizi ni nguo za joshua na kaka yake nguo hizi hazifuliwi bali zikirowa na mkojo huwanikwa tu juani na kisha kuvaliwa tena

Mtoto Joshua akiwa ana tushangaa maana anaona amevamiwa kwakweli inasikitisha sana

Hapa ndiyo mtoto joshua huwa anacheza wakati wa mchana

Mlango ulio wazi ndimo mtoto Joshua hufungiwa humo

Hiki ndicho chumba mtoto Joshua hufungiwa kama picha unavyoiona kona hiyo ndiyo mtoto huyo hujibanza

Kushoto ni kaka wa Joshua yeye amesema huwa anashinda nyumba za jirani kucheza wakati mdogo wake amefungiwa ndani

Angalia picha hii kwa makini jinsi mtoto Joshua anavyomwangalia mama yake mlezi yaani mama wa kambo.

Sekera Watsoni (40) amembeba mtoto Joshua kuonyesha anampenda na kuwa anamhudumia vizuri mtoto huyo.

Huyu mama pamoja na mumewe ndiyo wanaomtesa mtoto Joshua.
Hawa kaka zake Joshua wakituonyesha sehemu wanayolala pamoja na joshua wakati mama huyo yeye amesema  yeye huwa analala na joshua chumbani kwake 

Baadhi ya majirani wakisimulia mkasa huo.

Amini usiamini mtoto Joshua baada ya kuona mkeka mzuri alijilaza kwa furaha kwani amezoea kulala sakafuni.
Mama mlezi wa Joshua akijiandaa kumpeleka joshua kituo cha afya akapate matibabu baada ya kuamriwa kufanya hivyo.


Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.

Tukio hilo limetokea leo jijini mbeya katika  mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga ambapo majirani wa karibu na mtoto huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa huo kufika nyumbani anapoishi mtoto huyo kwa lengo la kufahamu maendeleo yake .

Mtoto huyo amefahamika kwa jina la Joshua Joseph umri unao kadiriwa  kuwa ni kati ya miaka miwili au mitatu  ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake wakiwa wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao.
Akizungumzia tukio hilo Kaimu barozi wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi ya utapiamlo.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea  taarifa kuhusiana na   suala hilo  ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za mtaa kwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.

Aidha baada ya kuhojiwa alikiri kosa ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa ambao walimtaka kuhakikisha anamtunza vema mtoto huyo kwa kumpatia chakula bora pamoja na huduma nyingine.

Mara baada ya mtu huyo kupewa kalipio na viongozi wa mtaa hali hiyo iliendelea tena ambapo wao kama viongozi wa shina pamoja na wananchi walimuita yeye pamoja na mke wake aitwaye  Sekera Watsoni (40) kuhama mtaani hapo kwa kwa kipindi cha miezi sita ambapo walikaidi agizo hilo.

Amesema mara baada ya watu hao kugoma waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika umoja wa ubarozi wao na kuto watambua tena kama wananchi wa eneo hilo kutokana na vitendo vyao vya kikatili dhidi ya mtoto huyo.
Kwa upande wao Maafisa maaendeleo ya jamii kata ya Igawilo na Iyunga ambao ndio waliofika katika eneo hilo wamesema kuwa matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ndani ya jamii hasa kwa vitendo vya kunyanyaswa kwa watoto wanawake.
Mmoja wa Maafisa hao Ndugu Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo. 
Amesema hali ya kiafya ya mtoto si ya kulizisha kutokana na kusumbuliwanna maradhi mbalimbali yanayotokana na kukosekana kwa lishe bora pamoja na huduma nyingine.
Amesema anawashukuru majirani pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mtaa ambao wamekuwa karibu na mtoto huyo kwa kipindi chote cha miaka miwili licha ya kutokuwepo kwa ushirikiano toka kwa  wazazi wa mtoto ambaye kwa sasa amefikishwa katika kituo cha afya  Inyala Kata ya Iyunga  jijini hapa.

Awali inaelezwa kuwa baba na mama wa mtoto huyo  wamekwisha tengana kwa kipindi kirefu sasa kutokana na kutokuwepo kwa maelewano ndani ya nyumba hiyo hali ambayo ilimfanya baba huyo kuoa mwanamke mwingine ambaye ndiye anaye ishi na mtoto kwa sasa kama mama wa kambo.

Amesema kutoka na kuwepo kwa mgawanyiko huo ndani ya familia baba pamoja na mama huyo ambaye ni mke wa pili walichukua jukumu la kuishi na watoto wote walio achwa na mwanamke wa kwanza ambapo kwa asilimia kubwa ndiko kuliko sabababisha kuwepo kwa hali hiyo ya manyanyaso ya mtoto.
Hata wakati wa tukio hilo la kumtoa mtoto huyo ndani baba mzazi wa mtoto hakuwepo katika maeneo hayo ya nyumbani ambapo maafisa ustawi wa jamii pamoja na majirani waliamua kuchukua jukumu la kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha afya Inyala kilichopo Kata ya Iyunga kwa lengo la kumfanyia uchunguzi na kutambua nini kinacho msumbua mtoto huyo.
Share:

Wednesday, May 15, 2013

"MWANAMKE MWENYE JINSIA MBILI ANATAKA KUNIOA, NIFANYEJE?"......NAOMBENI USHAURI...!!

HAta sielewi nianzie wapi ila kwa ufup ni ivi..nna rafik angu nilifahamiana nae nkiwa kazin mwaka 2011 mpaka leo tumekua close na kusaidiana kwakila jambo,,few days pass akaniomba aje kwangu tule wote dinner..soon after eating she told me dat she av smthin 2tell me n ask me..chakushangaza akanitamkia kua anataka kunioa,,astaghafiru llah nilichukizwa xana kwa kauli ile na nkamwambia aondoke kwangu immediately akawa analia sn na kunambia pls gv me sm few minutes i wana 2tel u smthn dat u dnt knw abt me or u ddnt even thot abt me.,akaendelea am not a girl as how u see me bt am a male they call us(shemales)..ckuamin cz anamuonekano wa kike ni mrembo ata kuliko wanawake wengne ana figure nzur,,shape ya kike na sura ya kike bt dp down she is not a girl,,nkamuomba anihakikishie kua kwel yeye ni shemale km ambavyo anasema,,she romove her clothes 

owwwwhh..OMG...kwel Mungu ni m'bora wa Uumbaji yaan ana matiti makubwa na anavaa brah like us women..oohh wat else shud i say? Cz she looks perfectly like a woman n she av everything in a woman bt she av got a (Pussy n Dick)..dick iko kwa juu na pussy imekaa chin ila anasema dick ndo iko strong zaid ya Pussy na tangu azaliwe hajawah kuingia kwenye period....n she is serious inlove with me n i jus tried 2avoid her bt she follows me here n there..i need ur ideas wat God say abt dos peoples who av got two genders??do dey not suposed 2 marry cz dey got women appearance?? ,,OMG.....,,, xo confuzed..,,!!
Share:

VIDEO YA WANAFUNZI WA MANZESE WALIOKUWA WAKIDONDOSHWA NA MAPEPO JANA....ANGALIA HAPA...!!


Hali ya taharuki ilitokea jana katika shule ya sekondari Manzese jijini Dar es salaam baada ya zaidi ya wanafunzi 40 kupatwa na ugonjwa wa kuanguka ovyo na kusababisha kukatishwa kwa masomo na kulazimishwa wanafunzi kurudi nyumbani kwa kuhofia usalama wao. 

VIDEO YA RIPOTI YA ITV 


Share:

Tuesday, May 7, 2013

HAWA NDIO MAPACHA WALIOUNGANA TOKA IRINGA .........ANGALIA PICHA....!!


Hawa  ndio mapacha  wawili  walioungana na  sasa  wanaendelea  kuishi  vema katika wilaya ya  kilolo ambako 
wanaendelea  kusoma ni  wakazi  wa wilaya ya Makete
Share:

Monday, April 29, 2013

VIDEO: MKULIMA AUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MOTO.... HUU NI UNYAMA ULIOKITHIRI...!!

UNYAMA: MKULIMA AUAWA KWA KUCHOMWA MOTO.....VIDEO YA TUKIO
Share:

MCHAWI AZIKWA AKIWA HAI PAMOJA NA MAREHEMU ALIYEDAIWA KUMUUWA KWA USHIRIKINA......!!

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji na kata ya Mkwajuni Wilaya ya Chunya Mkoani hapa wamemzika Mwanakijiji mwenzao akiwa hai wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mmoja kijijini hapo.
 Mwili wa marehemu aliyezikwa hai baada ya kutolewa kutoka kaburini. Pembeni ni jeneza la marehemu aliyetuhumiwa kumuua kwa ushirikina
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Apri 26 mwaka huu majira ya Saa Nane Mchana katika Kitongoji cha Maweni Makaburini baada ya Mhanga aliyefahamika kwa jina la Victory Mwachirui(68) kuhudhuria mazishi ya Pita Barton(28)aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Thobias Ismail amesema marehemu alipatwa na umauti akiwa anapatiwa matibabu kwa mganga wa jadi ambaye jina lake halikuweza kujulikana maramoja.
Amesema wakati taratibu za mazishi zikiendelea Ndugu wa marehemu walidai kuwa kifo cha Marehemu kilisababishwa na Mwachirui ambaye ni Katekista mstaafu kwa imani za kishirikina.
Ameongeza kuwa wakati kaburi likichimbwa kwa ajili ya kumzika marehemu ndipo vijana waliokuwa wakichimba waliagiza Wazee wa Mila wafike makaburini kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa mazishi na kukagua ukubwa wa Kaburi ambalo lilikuwa limekwisha chimbwa.
Kutokana na mwito huo walifika wazee wanne akiwemo Mzee Mwachirui ambaye walimsisitiza kusogea jirani na kaburi ambapo baada ya kusogea alipigwa na Sururu kichwani na kuangukia kaburini huku akisindikizwa na marungu.. Kwa habari kamili na picha zaidi, click link ifuatayo: Aliyezikwa akiwa hai afukuliwa na kukutwa amekufa chunya mbeya
Jeneza la aliyekufa kwa ugonjwa tayari limetolewa pembeni. Sasa anafukuliwa aliyezikwa akiwa hai
Jeneza la aliyekufa kwa ugonjwa tayari limetolewa pembeni. Sasa anafukuliwa aliyezikwa akiwa hai
Mwili wa aliyezikwa hai unatolewa kaburini
Mwili wa aliyezikwa hai unatolewa kaburini
Dada wa marehemu aliyezikwa akiwa hai
Dada wa marehemu aliyezikwa akiwa hai
Mwili wa marehemu aliyezikwa hai baada ya kutolewa kutoka kaburini. Pembeni ni jeneza la marehemu aliyetuhumiwa kumuua kwa ushirikina
Kwa habari kamili na picha zaidi, click link ifuatayo: Aliyezikwa akiwa hai afukuliwa na kukutwa amekufa chunya mbeya


Share:

Sunday, April 14, 2013

HILI NDIO SAKATA LA MWANAMKE ALIYEFUFUKA HUKO GEITA BAADA YA KUFARIKI MIAKA 5 ILIYOPITA....!!


Mji wa Geita na maeneo ya jirani juzi ulikumbwa na taharuki ya aina yake, pale mwanamke ambaye anadaiwa kwamba alifariki miaka mitano iliyopita alipoonekana akiwa hai katika eneo la Kasamwa.
 
Inadaiwa kwamba Flora Onesmo (45) alifariki Februari 28, 2008 katika Hospitali ya Wilaya ya Geita na kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya, Kata ya Butundwe, lakini juzi alfajiri alikutwa ameketi nje ya nyumba ya dada yake aitwaye Monica James, anayeishi Kasamwa.




Aliyekuwa wa kwanza kumwona Flora ni mdogo wake aitwaye Monica Onesmo ambaye baada ya kuamka saa 11:00 alfajiri nyumbani kwa dada yake, alimwona mwanamke aliyekuwa ameketi nje ya nyumba hiyo, lakini alimfananisha mwanamama huyo na marehemu dada yake.


“Baada ya kumwona nilimwita mtoto wake tunayekaa naye na nikampigia simu dada (Monica) ambaye alikuwa amelala chumba kingine nikamwambia kwamba nimeamka na kumkuta mwanamke amekaa hapa nje, lakini kila nikimwangalia anafanana na marehemu dada yetu,”alisema Jubili na kuongeza kwamba alipowaita wote walitoka nje.

 Alisema mtoto wa Flora (marehemu anayedaiwa kufufuka) anaitwa Rebeka Elisha (16) na kwamba walimchukua tangu 2008 wakati mama yake huyo alipofariki dunia katika Hospitali ya Geita ambako alikuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa ini.



Rebeka ambaye ni mtoto wa nne wa Flora alisema: “Mama mdogo alituita sisi tulikuwa tumelala akasema kwamba nje kuna mwanamke ambaye anafanana na marehemu mama yetu, ndipo na sisi tukatoka na kweli kumwangalia alikuwa ni yeye kabisa.”

Alisema walipomuhoji mama yake huyo kwamba ametokea wapi, aliwaeleza kuwa ametoka eneo la Katoro kwa mganga na aliletwa na watu ambao hakuwatambua Alhamisi saa 1:30 usiku ndani ya gari na watu hao walimshusha kwa mtu aitwaye Juma Luchunga ambaye ni jirani na dada zake hao.




Kauli ya Flora




Akizungumza na waandishi wa habari, Flora alisema yeye ni mkazi wa Katoro na kwamba alitokea Katoro nyumbani kwa mganga wa jadi ambaye hata hivyo hakumtaja kwa maelezo kwamba wataalamu wake (majini) wamemkataza.

“Nilikuwa naishi kwa mganga wa kienyeji ila alikuja mwanaume wakati nikiwa pale akaninywesha dawa kisha tukapakizwa kwenye gari na watu wawili ambao sikuwatambua, mmoja mwanamke na mwingine mwanaume mpaka hapa Kasamwa tukashushwa saa 1:00 jioni,”alisema Flora.


Alisema alipofika Kasamwa alikwenda kunywa uji kwa mama mmoja ambaye pia hakumtaja na kwamba baadaye alipelekwa nyumbani kwa mtu mwingine saa nne usiku, lakini watu wa nyumba hiyo walipomwona walimwambia: “Hapa si kwako twende tukupeleke kwa ndugu yako” na ndipo wakampeleka kwa dada yake ambako aliketi nje hadi alfajiri.


Flora alisema kabla ya kuishi kwa mganga alikuwa akiishi porini ambako alitupwa na watu asiowafahamu na baadaye aliokotwa na wasamaria wema ambao ndiyo walimpeleka kwa mganga ambako alikuwa akiishi muda wote.


Kuhusu ndugu, Flora alisema ana ndugu zake Sengerema na Geita kwamba Sengerema ndiko alikokuwa akiishi kabla ya kwenda porini.


Kadhalika mwanamke huyo anayedaiwa kufufuka alisema ana watoto watano, (idadi ambayo ni sawa na ile aliyoacha marehemu Flora), lakini alipoambiwa awataje alikuwa akichanganya majina.


Ndugu wapishana

Baba mzazi wa mwanamke huyo, James Tunge ambaye aliitwa baada ya kutokea tukio hilo alisema kuwa mwanaye alifariki, lakini anashangaa kuona leo anaonekana tena.



Hata hivyo, Tunge alisema alipomwona mwanamke huyo juzi asubuhi alikuwa akifanana kabisa na mwanaye Flora, lakini alipoondoka kwenda kufuata picha yake na kurejea alikuta amebadilika, kwani kovu alilokuwa nalo kabla ya kifo halikuwa likionekana.

“Kwa sasa naweza kusema huyu siyo ila asubuhi wakati namwona ni kweli alikuwa mwanangu marehemu, najua mwanangu alikuwa na kovu kubwa puani na shavu la kushoto, lakini sasa hivi anaonekana ana kovu moja la shavuni ila sehemu zingine za mwili wanafanana kabisa,”alisema Tunge.


Kwa upande wake Jubili alisema kuna kila dalili kwamba mwanamke huyo ni mdogo wake, kwani anavyojieleza maelezo yake yanafanana. Alisema anawatambua watoto wake na ndugu japo wakati mwingine ni kama anapoteza kumbukumbu na kubadilika badilika sura.


“Wakati tunamwona asubuhi alikuwa akifanana na dada yangu marehemu, kwani dada alikuwa na kovu kubwa puani na shavuni na kweli alikuwa nalo na baadaye tulipoendelea kumuhoji alianza kubadilika sura na mara kovu likawa halionekani tena, “alisema Jubili.


Kwa ujumla ndugu wa mwanamke huyo wanahusisha tukio hilo na ushirikina kwa kusema kwamba huenda ndugu yao alichukuliwa kwa njia za giza, lakini Mungu amemwezesha kurejea katika maisha ya kawaida.


Jubili alisema kifo cha Flora miaka mitano iliyopita kilikuwa cha mazingira ya kutatanisha, kwani aliugua ghafla baada ya kula viazi vitamu kwenye mji wa jirani na hapo kuanza kuvimba tumbo.


Kwa kuzingatia mazingira hayo, juzi Flora alipelekwa wilayani Sengerema kwa mganga wa jadi aliyejitambulisha kwa jina la Dk. Mkonogi Masendena .


Kabla ya kupelekwa Sengerema, suala hilo lilifikishwa polisi ambao baadaye waliruhusu Flora kuondoka na wanaodai kwamba ni ndugu yao na hata walipofika Sengerema walilazimika kwenda polisi kwanza.


Polisi mkoani Geita walithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba ndugu zake waliondoka naye.
Share:

Saturday, April 13, 2013

MBWA AKUTWA NA MGUU WA BINTI WA DARASA LA 7....!!


IMANI za kishirikina zimezidi kukitisa Kijiji cha Isange, Kata ya Isange, Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya baada ya matukio ya kupotea na kuuawa kwa watoto kutokea mara kwa mara ambapo safari hii binti mmoja wa darasa la saba ameuawa na mguu wake kukutwa ukiliwa na mbwa.
Binti huyo aliyeuawa amegundulika kuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba  aliyejulikana kwa jina la Lista Sebule aliyekuwa akisoma katika Shule ya Msingi Mpombo iliyopo Isange na alipotea katika mazingira ya kutatanisha na maiti yake kukutwa kando ya mto siku tisa baadaye. Katika tukio la awali, mtoto mmoja alikatwa kichwa na watu wasiojulikana kisha kutoweka nacho.
Mama mzazi wa marehemu, Christina Sakalile alisema binti yake (Lista) alipotea saa tisa jioni ya Machi 31, mwaka huu baada ya kutumwa kupeleka simu kibandani ili ‘ikachajiwe’ lakini hakurudi hadi giza lilipoingia, hali iliyozua wasiwasi na wakaanza kumtafuta bila mafanikio.
“Baada ya tukio hilo, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isange, Daudi Nsyani aliitisha mkutano wa wananchi wote ili mtoto atafutwe. Juhudi hizo zilizaa matunda Aprili nane, mwaka huu lakini alipatikana akiwa amekufa huku akiwa hana baadhi ya viungo mwilini,” alisema mama huyo huku akitokwa machozi.
  Mashuhuda wa tukio hilo walisema mwili wa marehemu ulipatikana ukiwa kando ya Mto Nkalisi uliopo kijijini hapo ukiwa umekatwa kichwa na miguu ambapo mguu mmoja ulipatikana baada ya mbwa kukutwa akiwa anaula na alipoona watu akawa anakimbia nao.
Hali hiyo iliwafanya watu kumfuatilia mbwa huyo ambaye aliongoza hadi kwenye mwili wa marehemu na kuwakuta mbwa wengine wawili wakiwa kando yake ambapo uongozi wa kijiji uliliarifu jeshi la polisi.
“Polisi walipofika walifanya uchunguzi na wananchi wakapiga kura ya siri ambapo watu wawili walikamatwa wakituhumiwa kuhusika na tukio hili. Mwili ulikabidhiwa kwa ndugu na wakauzika siku hiyohiyo na mazishi yake yaliweka historia kwa kuhudhuriwa na watu wengi,” alisema shuhuda huyo.
Diwani wa Kata ya Isange, Elias Mwandele amethibitisha kutokea tukio hilo na aliwataka wazazi kutowapeleka watoto kwenye shughuli za kuchunga mifugo kwa sasa.
Share:

Tuesday, April 2, 2013

MBEYA: VIBAKA WAMCHINJA MWANAFUNZI KAMA KUKU NA KUONDOKA NA KICHWA CHAKE...HII NI HATARI...!!

MWILI WA ALIYETUHUMIWA KWA MAUAJI YA MTOTO AYUBU AGEN UKIWA UMECHOMWA MOTO NAWANANCHI WENYE HASIRA KALI BAADA YA KUMKUTA MITA CHACHE KUTOKA KWENYE MWILI WA MAREHEMU AKIWA NA KISU KINACHODHANIWA KUTUMIKA KATIKA MAUAJI
MWILI WA MTOTO AYUBU UKITOLEWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA MAKANDANAWILAYA YA RUNGWE  
SAFARI YA KUELEKEA KIJIJI CHA IJOKA KWA MAZISHI
-wananchi wapanda hasira wamteketeza kwa moto mtuhumiwa.
- ajali nazo zamaliza watatu sherehe za  pasaka.
Na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
MATUKIO ya kutisha na ya kinyama dhidi ya watoto wadogo yameendelea kuutikisa Mkoa wa Mbeya, baada ya mwanafunzi wa chekechea, Ayoub Agen (6) kuuwa kwa kuchinjwa mithili ya kuku na wauaji kuondoka na kichwa chake.
Hata hivyo wananchi wenye hasira walifanikiwa kumnasa mmoja wa watuhumiwa wa tukio hilo, ambaye hata hivyo jina lake halikuweza kupatikana ambapo baada ya kummbana ili aeleze sehemu  walikokificha kichwa cha marehemu aligoma hivyo kuamua kumteketeza kwa moto.
Habari za uhakika kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Ijoka  katika kata ya Mpombo, wilayani Rungwe, Rafael Mwaikenda,  zinadai kuwa tukio hilo lilitokea Machi 31 majira ya saa 11:00 jioni.
Akifafanua zaidi Mwenyekiti  huyo alisema,  marehemu Agen alikuwa ni mwanafunzi wa chekechea katika shule ya msingi Lusanje kijijini hapo na kwamba alikutwa na mauti hayo ya kikatili baada ya watu hao wasiofahamika kufanikiwa kumuiba nyumbani kwao.
Mwaikenda alisema  mwili wa marehemu uliokotwa ukiwa umetenganishwa kichwa na kiwiliwili huku kichwa kikiwa hakionekani hadi sasa ikiwa ni muda mfupi tu baada ya watu hao wasiofahamika kumwiba toka nyumbani kwa wazazi wa marehemu .
“Marehemu alichukuliwa na watu hao wasiofahamika akiwa anacheza na wenzake na wenzake baada ya kuona hivyo waliamua kutoa taarifa ambapo muda mfupi walianza kumtafuta bila mafanikio, lakini wananchi wakiwa wanaendelea na harakati hizo waliukuta mwili huo ukiwa umetelekezwa kichakana na wauaji hao kuondoka na kichwa” alifafanua Mwaikenda.
Mkazi mwingine katika kijiji hicho, Tumpale Sankemwa, alikielezea mkasa huo, alisema baada ya wananchi kugundua mwili huo wa marehemu waliendelea kuwasaka wahusika na wakiwa katika harakati hizo ghafla walikutana na mtu mmoja ambaye walimtilia mashaka.
Alisema baada ya kumfanyia mahojiano ya kina kwa kuwa alikuwa hafahamiki na mgeni kijijini hapo, alikuwa akijibu jeuri hivyo kuwapandisha hasira wananchi jambo lililosababisha kuanza kumshambulia na hatimaye kumuua papo hapo.
Hata hivyo alisema wakati wananchi wakiendelea kumshushia kipigon mtu huyo licha ya kutotaja jina lake, alikiri kuhusika katika tukio hilo kwa kueleza kuwa waliohusika walikuwa watatu na kwamba wenzake walikuwa wameondoka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi wa jeshi la polisi,Diwani Athumani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hadi sasa kichwa cha marehemu huyo hakijaonekana  na jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi.
“Ni kweli tukio hilo limetokea, hata hivyo mtu anayetuhumiwa kushiriki mauaji hayo naye aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira  ambao licha ya kumuua waliuteketeza mwili wake kwa moto”.
Aliongeza kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo ni mwanaume anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 30 hadi 35  na kwamba uchunguzi wa awali umeonesha chanzo cha mauaji hayo kinahusishwa  na imani za kishirikina.
Wakati huo huo watu watatu  wamefariki dunia  na wengine wawili kujeruhiwa vibaya,  katika matukio mawili tofauti ya ajili za barabarani mkoani hapa.
Katika tukio la kwanza lililotokea eneo la Mbalizi wilayani hapa, majira ya saa nne usiku  katika barabara ya Mbeya- Tunduma, watu wawili, Meshaki Inkuru (24) na Said Ndasi (19) baada ya gari aina ya Toyota Chesser yenye nambari  za usajili T 516 AAA lililokuwa likiendeshwa na mtu asiyefahamika  kuwavamia wakiwa nje ya Hoteli ya Royal Tughimbe walikokuwa wakiendelea na sherehe za Pasaka.
Kamanda wa polisi aliwataja majeruhi wa tukio hilo ambao wamelazwa katika Hospitali teuli ya wilaya ya Mbeya ya Ifisi ni Shar Mkumbwa (20), Juliet Katemi (18)   wote wakazi wa mji mdogo wa Mbalizi.
Tukio lingine  ni lile lililotokea eneo la Soweto ambapo mtu mmoja mtembea kwa miguu, aliyetambuliwa kwa jina moja la Paul (60) kufa papo hapo baada ya kugongwa na gari ambayo hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja .
Share:

Wednesday, March 27, 2013

LAANA: YULE MTOTO WA MIAKA 8 ALIYEOA BIBI WA MAIAKA 61 ADAI SASA ANAJISIKIA FURAHA KUITWA BABA....!!


 
KUSHOTO: Sanele akibusiana na mkewe, Helen siku ya harusi yao wiki mbili zilizopita. KULIA: Sanele na Helen walipata chakula cha usiku pamoja nyumbani kwa mkewe huyo.

Huku miguu yake ikining'inia juu ya sakafu na sehemu yake ya chakula cha mtoto, inaonekana kama anakula chakula cha usiku na bibi yake.Ukweli ni kwamba Sanele Masilela, mwenye miaka 8, anafurahia chakula cha usiku na mke wake, baada ya kumuoa wiki mbili zilizopita, na inasemekana kwa sasa ameanza kujisikia kama mume kamili.

Mwanafunzi huyo alimuoa Helen Shabangu baada ya mababu zake kuwasiliana naye kutoka nyuma ya makaburini wakimweleza kwamba anatakiwa kuoa.Mwanafunzi huyo alimchagua rafiki wa familia yao na mama wa watoto watano Helen na familia yake ikalipa Pauni za Uingereza 500 kuwezesha mama huyo kuwa mkewe katika sherehe iliyogharimu Pauni 1,000 mjini Tshwane, Afrika Kusini.

Sanele alikiri kwamba tangu harusi hiyo, ameanza kujisikia kama mwanandoa.Alisema: "Siku hiyo ilikuwa ya kipekee na hakika ilikuwa kama alivyokuwa akifikiria itakuwa."Marafiki zangu walifikiri ni mzaha kwamba nilikuwa naoa lakini sasa najisikia kama mume."

Akiwa amevalia tai na suti ya rangi ya shaba, Sanele, mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watano, alivalishana pete mbele ya wageni 100 na hata kufikia kupigana mabusu na mkewe huyo.Lakini, licha ya muonekano, haikuwa halisia, ndoa hiyo ilikuwa ni kutimia mila na haikufungwa kisheria.

Wanandoa hao hawaishi pamoja lakini Helen mara kwa mara anamwalika kula naye chakula cha usiku pamoja kwenye nyumba anayoishi na familia watoto wake.Sanele amerejea kwenye maisha yake na kuendelea kufurahia shule na kucheza kandanda na marafiki zake lakini anakiri kwamba ndoa hiyo ilikuwa muhimu mno kwake.

Alisema: "Babu yangu aliwasiliana nami kupitia picha ya harusi ya mama yangu."Tuna mahusiano maalumu sababu nimerithi jina lake."Alisema aliona picha hiyo na kujihisi mnyonge kwamba hakuwahi kuweza kufunga ndoa yake mwenyewe hivyo alinitaka mimi nifunge ndoa. Nilimchagua Helen sababu nampenda sana."

Habari za harusi hiyo zimeshitua dunia nzima lakini Helen, ambaye ameshaolewa kwa miaka 30 sasa na kupata watoto watano wenye umri wa kati ya miaka 37 na 27, ametetea sherehe hiyo.Alisema: "Nafahamu habari hiyo imesambaa dunia nzima na kubwa ni kuwa nchi nyingine zimeweza kujifunza kuhusu utamaduni wetu na mababu zetu.

"Tulichofanya hakikuwa makosa. Ni utamaduni wetu tu. Pale mababu zetu wanapoagiza kitu, tunafanya kile wanachosema. Sidhani kama watu wengine wanaelewa hilo."Nafahamu mababu wamefurahi sasa sababu tuko sawa na kila kitu kinaonekana safi."Familia nzima imefurahi sana kuliko ilivyowahi kutokea."

Helen alikiri sherehe hiyo ya gharama ilikuwa kubwa kuzidi ilivyokuwa harusi yake halisi na mumewe, Alfred, mwenye miaka 65, na hakuna cha kujutia.Aliongeza: "Kila mara nitakuwa karibu na familia ya Sanele kuliko ilivyokuwa kabla ya harusi hiyo na kabla Sanele kunichagua mimi kama mkewe tulikuwa karibu mno.
"Hakuna kilichobadilika tangu wakati huo."

Mumewe kwa miaka 30, Alfred mwenye umri wa miaka 65, alisema: "Watoto wangu na mimi tumefurahi.
Sanele pia alisema anatarajia atafunga ndoa sahihi kwa mwanamke wa umri kama wake wakati atakapokuwa mkubwa.

Aliongeza: "Nilimweleza mama yangu kwamba nilitaka kuoa kwa sababu hakika nilikuwa nataka kufanya hivyo."Nimefurahi kwamba nimemuoa Helen - lakini nitaenda shule na kusoma kwa bidii."Pindi nitakapokuwa mkubwa nitaoa msichana wa rika langu."

Mama wa Sanele mwenye miaka 46, Patience Masilela aliongeza kwamba anaamini sherehe hiyo 'haikuwa na tatizo' na kwamba imewatuliza mababu.Alisema: "Hii ni mara ya kwanza kutokea katika familia hiyo."
Share:

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger