Showing posts with label UKATILI. Show all posts
Showing posts with label UKATILI. Show all posts

Friday, May 20, 2016

Tanzia: Askari wa Usalama Barabarani, Ally Kinyogoli Auawa kwa Kupigwa Risasi

Watu wasiojulikana wakiwa na pikipiki aina ya Boxer,usiku wakuamkia leo wamemuuwa kwa kumpiga risasi kadhaa katika sehemu mbalimbali za mwili wake Askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani, Ally Kinyogoli nyumbani kwake Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani.

Baada ya kumuua, watu hao walitokomea kusikojulikana bila kuchukua kitu chochote

Kinyogoli alijizolea umaarufu katika kipindi cha redio One kila siku asubuhi alipokua akitoa taarifa za hali za barabarani zikiwemo njia zenye foleni kwa wakazi wa jijini.
Share:

Sakata la Mauaji Msikitini Mwanza: Kundi la Kigaidi la ISIS Lahusishwa

YADAIWA ni kisasi baada ya Polisi kuwakamata wanaharakati wa IS saa 24 kabla.

"baada ya swala kumalizika, watu hao waliingia na kuwaamuru kulala chini huku wakitoa bendera nyeusi na maandishi ya meupe ya Kiarabu kisha kumtaka Imamu wa msikiti kujitokeza mbele, bendera hiyo ni kama ile inayotumiwa na kundi la kigaidi la IS"

"Imamu alipojitokeza huku tukiwa tumelala chini, watu hao walisikika wakisema 'Kwa nini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na polisi, wengine wanapigana 'jihad'...hali hiyo ilitushtua zaidi baada ya Imamu kuanza kuchinjwa kwa panga,"

"Ghafla wakatuamuru kulala kifudifudi na kudai wao ni IS wamekuja kufanya kazi yao, kisha wakaanza kutushambulia na kujeruhi. Mwenzangu niliyekuwa naye pembeni alikatwa panga na kuangukia juu yangu, hali hiyo ilinifanya nionekane kama nimekufa,"

Habari za uhakika ambazo Nipashe imezipata zinasema. Imam huyo na wafuasi wake, waliuwawa na kundi la watu wanane waliokuwa na bunduki moja, mapanga, mashoka na majambia, kwa kuchinjwa ndani ya msikiti na watu wanaosemekana ni washirika wa Kundi la kigaidi la Dola ya Kiislamu (IS), ambalo linaendesha harakati zake katika nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati.

Waliouawa katika tukio hilo ni Imamu Feruz Elias (27), mkazi wa Ibanda Relini, Mbwana Rajab (40), mkazi wa Ibanda na Khamis Mponda (28) mkazi wa Mkolani.

Habari kutoka ndani ya duru za uchunguzi mkoani Mwanza, zilizopatikana jana, zilisema polisi ilikuwa ikifuatilia mienendo ya kikundi kinachoonekana kuwa cha kigaidi na kufanikiwa kukamata wafuasi kadhaa kabla ya kutokea mauaji hayo juzi.

"Uwezekano wa kuwapo kwa uhusiano baina ya wauaji hao na kikundi cha kigaidi kinachosakwa na polisi, unatokana na ukweli kuwa kabla ya kufanya mauaji hayo, watu hao walihoji kuwapo kwa ibada hiyo wakati "(Waislamu) wenzetu wamekamatwa na polisi."

Imam wa msikiti na wafuasi hao katika barabara ya kwenda Shinyanga, waliuwawa wakati wa ibada ya saa 2:00 usiku na watu hao waliokuwa na bendera nyeusi yenye maandishi meupe ya Kiarabu kama bendera ya IS na pia wakiwa wameficha nyuso zao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi ili kufahamu kama tukio hilo linahusiana na ugaidi au la.

Habari za kiuchunguzi zinadai polisi ilishtushwa na kuwapo kwa mauaji ya watu yanayodaiwa kuwa ya ujambazi, lakini bila kuwapo kwa ulazima wa majambazi kuwaua watu hao walioporwa mali zao pia.

Chanzo kimoja cha habari kutoka duru za uchunguzi kilisema kwa kawaida, jambazi huwa haui mtu kama hapakuwa na ubishi katika kusalimisha mali au fedha zinazoporwa. Pamekuwa na matukio ya mauaji ya wafanyabiashara ya mara kwa mara, katika maduka ya simu na kutuma na kupokea fedha, ambayo yamegharimu maisha ya takriban watu wanne tangu kuanza kwa mwaka huu mkoani Mwanza.

Katika kufuatilia mauaji hayo, ndipo vyombo vya usalama vilipogundua kuwapo kwa kikundi cha kigaidi mkoani humo.

MASHUHUDA WASIMULIA

Mashuhuda walionusurika katika tukio hilo, wakizungumza na Nipashe jana eneo la msikiti huo, walisema majira ya saa 3.00 juzi usiku baada ya kumaliza swala, waliingia watu wapatao 10 wakiwa wameshika mashoka, mapanga na majambia na kuwaamuru waumini wote kulala kifudifudi.

WALIONUSURIKA

Kijana aliyenusurika katika tukio hilo, Abubakari Makabwa (19), alisema baada ya swala kumalizika, watu hao waliingia na kuwaamuru kulala chini huku wakitoa bendera nyeusi na maandishi ya meupe ya Kiarabu kisha kumtaka Imamu wa msikiti kujitokeza mbele.

Bendera hiyo inafanana na ile inayotumiwa na Kundi la IS.

"Imamu alipojitokeza huku tukiwa tumelala chini, watu hao walisikika wakisema 'Kwa nini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na polisi, wengine wanapigana 'jihad'...hali hiyo ilitushtua zaidi baada ya Imamu kuanza kuchinjwa kwa panga," alisema Makabwa.

Alisema baada ya Imamu kukatwa kwa panga shingoni, wauaji hao walianza kuwachinja wengine waliolala kabla ya amri ya kutoka kwa mmoja wa wauaji hao, kuwaamuru watoto kuondoka ndani ya msikiti huku wakiendelea kuwachinja wengine.

Makabwa alisema baada ya kutoka akiwa anakimbia na wenzake wanne kupitia mlango wa nyuma, walikutana na mtu mwingine akiwa ameshika bunduki akilinda usalama nje, hali iliyowatia shaka zaidi.

"Tulisikia sauti ya yule mwanamke aliyekuwamo ndani akisema wapige risasi hao. Tulilala vichakani na wala hatukuonekana kutokana na wauaji hao walipofika msikitini walizima taa zote, lakini mshika bunduki hakuweza kurusha risasi yoyote," alisema.

Aidha, alisema baada ya kufanikiwa kukimbia, watu hao walirusha bomu la mafuta ambalo lililipuka huku lingine likishindwa kulipuka ndani ya msikiti huo.

Naye manusura mwingine, Abeid Gati, alisema awali baada ya watu hao kuingia ndani ya msikiti huo, alidhani ni askari polisi hivyo kumfanya akae chini.

"Ghafla wakatuamuru kulala kifudifudi na kudai wao ni IS wamekuja kufanya kazi yao, kisha wakaanza kutushambulia na kujeruhi. Mwenzangu niliyekuwa naye pembeni alikatwa panga na kuangukia juu yangu, hali hiyo ilinifanya nionekane kama nimekufa," alisema Gati.

Alisema baada ya tukio, alikaa kwa muda mrefu kama mfu hadi waliporusha chupa ya mlipuko na kuunguza ndoo kubwa ya plastiki na nyingine ilishindwa kulipuka, ndipo alikimbia nje kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa.

MWENYEKITI WA MTAA

Mwenyekiti wa mtaa wa Utemini, Jukaeli Kiula, alisema alipata taarifa za tukio hilo saa 3:20 usiku kutoka kwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Said, aliyekuwa mmoja wa waumini wa msikiti huo.

"Baada ya taarifa hizo, tulikusanyana kama 'wananzengo' (wanajamii) na kwenda msikiti hapo, tuliwakuta watu watatu wakiwa wamepigwa mapanga na kujeruhiwa vibaya sana, nilipiga simu polisi nao walifika eneo la tukio muda mfupi baadaye," alisema Kiula.

Kiula alisema msikiti huo una waumini zaidi ya 20 wanaoswali hapo, hivyo baada ya kuvamiwa na watu hao walishindwa kujitetea kwa lolote kutokana na mazingira yaliyopo kwenye msikiti huo.

Katika hatua nyingine aliwaomba, wananchi wa mtaa huo kutoa ushirikiano ili watu hao waweze kupatikana kwani ni sehemu ya watu waliopokelewa na kuhifadhiwa na jamii ya eneo ulipotokea uhalifu huo.

MCHUNGA NG'OMBE

Eneo lililotokea mauaji hayo kuna misikiti miwili huku mmoja ukimilikiwa na dhehebu lililopo chini ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na mwingine uko chini ya Aswar al Sunn.

Mchunga ng'ombe anayechunga maeneo karibu na msikiti wa Sunn, Mussa Masanja, alisema kuna eneo ambalo linamilikiwa na msikiti huo, huwa anawashuhudia vijana wakifundishwa mchezo wa ngumi na karate karibu na mlima.

"Nilikatazwa na mtu mmoja wa msikiti wa Sunn kuchungia ng'ombe kwa madai nitaharibu miti, lakini baada ya kuchungulia kwa mbali niliwaona watu wazima wawili wakiwafundisha ngumi na karate vijana hali iliyonitisha," alisema Masanja.

KAMANDA WA POLISI

Akizungumzia tukio hilo, Msangi alisema juzi saa 2.30 usiku, katika msikiti huo, watu wasiozidi 15 wakiwa wamevalia 'kininja' huku wakiwa na silaha mbalimbali kama mashoka, mapanga na bendera nyeusi yenye maandishi meupe, waliingia ndani ya msikiti huo na kuzima taa.

"Watu hao walisikika wakiwaambia waumini hao, kwanini wanaswali wakati wenzao wamekamatwa na kushikiliwa na polisi, hali iliyowafanya waanze kuwashambulia papo hapo,"alisema Kamanda Msangi.

Msangi alisema watu hao waliwashambulia kwa silaha hizo watu wanne msikiti hapo na kuwajeruhi vibaya kichwani na shingoni, lakini kati yao watatu walifariki dunia na mwingine mtoto wa miaka 13, kujeruhiwa.

Hata hivyo, alisema baada ya tukio hilo, polisi mkoani hapa inawashikilia watu watatu huku msako mkali wa kuwasaka wengine ukiendelea maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Source: Nipashe
Share:

Thursday, May 19, 2016

Watu Watatu Wauawa Kwa Kukatwa Mapanga na Mashoka Jijini Mwanza

Mnamo tarehe 18.05.2016 majira ya saa 20:30hrs katika msikiti wa masjid rahman uliopo ibanda relini mtaa wa utemini @ mapankini kata ya mkolani wilaya ya nyamagana jiji na mkoa wa mwanza. 

Watu wasiozidi 15 wakiwa wamevalia mavazi ya kuficha uso wakiwa na mapanga, shoka na bendera nyeusi yenye maandishi meupe waliingia ghafla katika msikiti tajwa hapo juu wakati waumini wa msikiti huo wakiwa wanaswali na kuzima taa na kutoa sauti wakisema “kwa nini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na wanashikiliwa na polisi ?” na hapo hapo wakaanza kuwakata kwa mapanga baadhi ya waumini katika sehemu mbalimbali za miili yao. 

Walipata majeraha makubwa kichwani, shingoni na mikononi na walipoteza maisha yao papo hapo na mmoja kupata majeraha sehemu za kichwani na kukimbizwa hospitali ya wilaya ya nyamagana (butimba). 
 
Waliouawa, 1. Feruz ismail elias  mika 27, muha imamu wa msikiti huo na mkazi wa ibanda relini, 2. Mbwana rajab miaka 40, mbondei mfanyabiashara na mkazi wa ibanda, 3. Khamisi mponda miaka 28 dereva wa kiwanda cha samaki (TFP), mkazi wa mkolani, wote walijeruhiwa sehemu za kichwani, shingoni na mikononi. 

Aliyejeruhiwa ni ismail abeid @ ghati miaka 13, mkurya mwanafunzi wa madrasa katika  shule ya kiislamu itwayo jabar hila iliyoko maeneo ya Nyasaka aliyepata majeraha kichwani na anapata matibabu hospitali ya Nyamagana.
 
Kutokana na hali hiyo, waumini wengine walifanikiwa kukimbia huku wakipiga mayowe yaliyopelekea wahalifu hao kukimbia na kurusha ndani ya msikiti chupa mbili za konyagi zilizokuwa na petroli na tambi za moto, chupa moja ililipuka lakini haikuleta madhara makubwa.
 
Jeshila la polisi  limewakamata washukiwa watatu kwa ajili ya kuwahoji kuhusiana na tukio hilo, huku msako mkali wa kuwasaka watu wengine walio husika kwa namna moja au nyingine kwenye mauaji hayo ukiwa bado unaendelea. 

Napenda kuwaeleza  wananchi watulie wakati tukiendelea na upelelezi wa tukio hili, na natoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu wa mauaji hayo ili tuweze kuwakamata. 

Pia nashauri na kusisitiza kuwepo na kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada, kumbi za starehe pamoja na mitaa yao. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo hayo.

Imesainiwa na:
……………………….
Sacp: Ahmed Msangi
Kamanda wa Polisi (m) Mwanza.
Share:

Tuesday, May 17, 2016

Mganga wa Kienyeji Ambaka Mgonjwa wake

Mganga wa Kienyeji Hamza Saidi,(40) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa aliyekwenda kutibiwa masikio kwenye ofisi ya mganga huyo.

Mganga huyo, Mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji anatuhumiwa kumbaka msichana wa miaka 20, na kumsababishia maumivu makali.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma SACP Fredinandi Mtui alisema, mganga huyo alifanya tukio hilo, Mei 15 majira ya saa tano asubuhi.

Inadaiwa kuwa msichana alifika  nyumbani kwa mganga huyo akiwa na lengo la kutibiwa masikio lakini mganga alimwambia ili dawa hiyo ifanye kazi ni lazima afanye naye mapenzi kwanza.

“Alimrubuni kuwa dawa ya sikio ili ifanye kazi inatakiwa afanye tendo la ngono na kwa ujanja huo , alimbaka msichana huyo,” alisema Kamanda.

Kamanda Mtui alisema kwa sasa mganga huyo anashilikiwa na polisi na atafikishwa mahakamani wakati wowote.

Katika tukio jingine, mkazi wa Mvinza,  kata ya Kagera Nkanda Josephine Ntahukisiga  (42) ambaye ni mkulima amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya nyumba ya baba yake kwa kutumia shuka.

Tukio hilo lililotokea Mei 14, 2015 inaelezwa kuwa Ntahukisiga alivizia ndugu zake wakiwa wamelala ndipo alipoenda sebuleni na kujinyonga kwa kutumia shuka kwa kulifunga juu ya dari.

Kwa  mujibu wa baba wa marehemu, Andrew Ntahukisiga alisema marehemu alikuwa na msongo wa mawazo tangu watoto wake walipofariki kwa ajali ya moto mwaka 2015.
Share:

Mtu Mwingine Auawa Kwa Kukatwa Mapanga Usiku Sengerema Mkoani Mwanza

Wakati upelelezi wa tukio la watu saba wa familia moja kuuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana ukiendelea, mauaji mengine ya aina hiyo yametokea wilayani Sengerema.

Safari hii, mkazi wa Kijiji cha Bilulumo, Kata ya Kafunzo, James Mgambo (71) aliuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Kafunzo, Dotto Bulunda, mke wa Mgambo aliyetajwa kwa jjina la Nyangalo Masisa (65) alijeruhiwa katika tukio hilo na amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Sengerema.

“Chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana na polisi wamefika kwa ajili ya uchunguzi,” alisema Bulunda. 

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bilulumo, Said Makelemo alisema mapanga mawili yanayoaminika kutumika yalikutwa eneo la tukio.

Mmoja wa majirani wa familia hiyo, Lameck Kasabulilo alisema hawakusikia kelele za kuomba msaada.

Kwa mujibu wa msemaji wa familia, Hakimu Elisha, mazishi ya Mgambo yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya ukoo yaliyopo kijijni hapo.

Mgaga Mkuu wa Hospitali Teule Wilaya ya Sengerema, Dk Mary Jose alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti, huku hali ya majeruhi ikiendelea vizuri.

Mkuu wa Wilaya Sengerema, Zainab Telack alisema tayari uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo umeanza na kuapa wahusika watasakwa na kutiwa mbaroni.
Share:

Monday, May 16, 2016

Auawa Kwa Kuchomwa Visu Akituhumiwa Kutoka Kimapenzi na Mtalaka Wake

Mkazi wa Kijiji cha Chala B, Tarafa ya Chala wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa, Moses Nambasita (48) ameuawa kwa kuchomwa visu kutokana na kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Akisimulia mkasa huo mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Vincent Mwanambuu alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni baada ya kuvamiwa na kijana mmoja alipokuwa akitoka nyumbani kwake kwenda nyumba jirani, alishambuliwa kwa kuchomwa visu.

Mwanambuu alisema baada ya kupata taarifa hizo alitoa taarifa Kituo kidogo cha Polisi Chala, askari walifika na kuchukua mwili kwa ajili ya uchunguzi na kuanza msako dhidi ya mtuhumiwa.

Akielezea chanzo cha mauaji hayo, Mwanambuu alisema mtuhumiwa alipata taarifa kuwa Nambasita ana uhusiano na mtalaka wake, ambaye walikuwa wameachana kipindi kirefu.

Alidai kuwa kutokana na taarifa hizo, mtuhumiwa alipeleka shauri la ugoni katika Mahakama ya Mwanzo Chala.

“Lakini kabla hata shauri hilo halijamalizika, tunashangaa kuona mtuhumiwa ameamua kujichukulia sheria mikononi, baada ya kutekeleza unyama huo alikimbia na kutokomea kusikojulikana,” alisema.

Mtendaji wa Kijiji cha Chala, Godfrey Mwanakatwe alisema kutokana na mazingira hayo polisi wanawashikilia watu wanne kwa kosa la kushiriki mauaji hayo.

Hatua hiyo inatokana na baada ya wao kutoa taarifa kwa muuaji kuwa Nambasita ana uhusiano wa kimapenzi na mtalaka wake, ambaye mpaka sasa haijulikani alipo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, baada ya uchunguzi wa polisi ndugu wa marehemu waliruhusiwa kuuzika mwili huo.

Mwaruanda alisema chanzo cha kifo hicho ni wivu wa mapenzi na kuongeza kuwa mtuhumiwa alianza vizuri kwa kufuata sheria, lakini haijulikani kilichosababisha kuchukua uamuzi huo wa kinyama.

Alisema wanawashikilia watu watatu wakituhumiwa kushiriki mauaji hayo, kwa kutoa taarifa kwa mtuhumiwa kwamba Nambasita alikuwa na uhusiano na mtalaka wake.

Kamanda Mwaruanda aliwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi, hivyo wafuate taratibu kupata haki zao.
Share:

Thursday, May 12, 2016

Watu 7 wa Familia Moja Wauawa Kikatili Jijini Mwanza

WATU saba wa familia moja wameuawa kikatili wilayani Sengerema mkoani Mwanza juzi usiku. 

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa huo, John Mongella na Kamanda wa Polisi Mkoa, Ahmed Msangi katika eneo la tukio, alisema watuhumiwa katika tukio hilo hawajajulikana.
 
Kuni aliwataja waliopoteza maisha katika tukio hilo kuwa ni Augenia Philipo (62), Maria Philipo (56), Yohana Mabula (20), Regina Aloyce (12) na Mkiwa Philipo (13) huku wengine wawili wakitambulika kwa jina moja kila mmoja kuwa ni Donald na Samson.

Aidha, chanzo cha mauaji hayo ya kikatili hakijajulikana, ingawa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Zainab Telack alisema huenda mauaji hayo inawezekana yakawa ni ya kulipiza kisasi. 

Vyanzo vingine vinaarifu kuwa mauaji ya namna hiyo ni ya kawaida katika maeneo hayo, hasa msimu huu ambao kaya nyingi zinakaribia msimu wa mavuno.

“Bado kuna mkanganyiko juu ya chanzo cha mauaji hayo, wapo wanaosema kuwa huenda ni ya kulipiza kisasi lakini pia wengine wanasema yanatokana na msimu wa mavuno, lakini tunaamini uchunguzi wa Polisi ndio utakuja na majibu sahihi na ambao umeshaanza kazi hivi tunavyoongea,” alisema Kuni.
Share:

Friday, May 6, 2016

Baba Aua Mtoto wa Kambo chumbani.......Yadaiwa ni Baada ya kumtuma mkewe Dukani kununua Dawa

Watu wawili wamekufa katika matukio mawili tofauti, akiwamo mtoto Mariam Haule (2) kwa kunyongwa na baba yake wa kambo baada ya kumtuma mama yake dukani kisha kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alisema jana kuwa, tukio hilo lilitokea Mei 2.

Issa alisema kuwa mtuhumiwa huyo mkazi wa Kijiji cha Usimba, Wilaya ya Kaliua mkoani humo kabla ya kufanya mauaji hayo, alimtuma mkewe, Kalunde Malugu kwenda dukani kununua dawa .

Alisema baada ya mkewe kwenda dukani, alipata mwanya wa kufanya mauaji hayo kisha kutokomea kusikojulikana.

“Tunawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano ili tuweze kumkamata mtuhumiwa afikishwe kwenye mkondo wa sheria,” alisema Issa.

Kamanda huyo alisema jeshi hilo litahakikisha mtuhumiwa huyo anakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.

Mama wa mtoto huyo alisema alitumwa na mumewe dukani kununua dawa, lakini aliporudi alikuta mlango umefungwa na alipoingia ndani alibaini mtoto wake ameuawa.

Alisema hafahamu sababu za mauaji hayo na wala hakukuwa na malalamiko au madai yoyote kutoka kwa mumewe kuhusiana na mtoto huyo.

Katika tukio la pili; Mkazi wa Kijiji cha Rwamkoma wilayani Butiama, Magesa Machera (46) amekutwa ameuawa kwa kunyongwa baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi alisema tukio hilo lilitokea Mei 3, mwaka huu saa tisa usiku.

Alisema inadaiwa kuwa siku ya tukio hilo, mpenzi wake, Remmy Samwel (35) alitoka nje kwenda kujisaidia, lakini aliporudi alimkuta Machera akiwa chini amekufa.

Ng’anzi alisema mpenzi wake huyo ambaye ni mgeni katika kijiji hicho huwa na mazoea ya kwenda kumsalimia mara kwa mara na walikuwa wakinywa pombe za kienyeji. “Uchunguzi wa mauaji hayo unaendelea na polisi inamshikilia mpenzi wake,” alisema.
Share:

Thursday, May 5, 2016

Habari Kamili Kuhusu Mauaji Yaliyotokea Bagamoyo...Mume Achinja Mke na Mtoto Kisa Wivu wa Mapenzi

 
JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Frowin Peter Mbwale (26) mkazi wa Kawe Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuua kwa kuwachinja mkewe Oliver Erasto (23) na mtoto wake Emanuel Frowin (3) kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Bonaventura Mushongi alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:30 jioni eneo la Zinga kata ya Dunda Tarafa ya Mwambao wilayani Bagamoyo.
 

Mushongi alisema kuwa katika hali isiyo kuwa ya kawaida juzi siku ya tukio mtuhumiwa akiwa na mwenzake alijulikana kwa jina la Rajabu Juma (20) Mkazi wa Makongo Jijini Dar es Salaam waliwaua watu hao kwenye vichaka vilivyopo kwenye eneo hilo la Kaole.

“Muda huo mtuhumiwa akiwa na mwenzake alimhadaa mke wake kuwa waende kwenye nyumba yao ambayo inaendelea kujengwa kwa lengo la kuitazama ambapo mke wake alikubali na kumbeba na mtoto wao na kwenda huko ambako aliwachinja shingoni,” alisema Kamanda Mushongi.

Alisema kuwa mtuhumiwa kumbe lengo lake halikuwa kuangalia ujenzi wa nyumba yao huko Kaole kumbe alikuwa na lengo lingine la kufanya unyama huo ambao aliutekeleza akiwa na rafiki yake huyo ambaye walishirikiana kumchinja mke na mtoto wake.
 
“Chanzo cha mauaji hayo ni mtuhumiwa huyo alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa ana uhusiano na mwanaume mwingine aitwaye Hamza mkazi wa Kawe Jijini Dar es Salaam na kusababisha mauaji hayo ya kusikitisha ambayo yamewaumiza watu wengi,” alisema Mushongi.

Alibainisha kuwa miili ya marehemu hao ilikutwa ikiwa imechinjwa na watu hao umbali wa mita 100 kutoka barabara ya magari itokayo Kaole kwenda eneo la Mbegani.

Aidha alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa majira ya saa 3:30 usiku baada ya wananchi Zinga kuwatilia mashaka walipokuwa wakijaribu kutaka kutoroka na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika, miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo kusubiri ndugu kwa ajili ya mazishi.
Share:

Mauaji ya Kutisha Kaole Bagamoyo Jana Jioni..Mama na Mtoto Wachinjwa Kama Kuku

Watu wawili mama na mtoto wamenyongwa hadi kufa kisha kuchinjwa kama kuku maeneo ya kaole jioni ya jana

Habari kutoka Kaole; Majira ya saa 12 jioni jana, ilipita pikipiki eneo hilo ikiwa imepakiza watu watatu, dereva wa nne! Wanaume wawili, mwanamke na mtoto.
Walipofika eneo la darajani, porini kidogo, pikipiki ilipaki, watu wote wakashuka ndipo hatua za utekelezaji mauaji hayo zilianza.

Inadaiwa kwamba, Mama na mtoto wake walinyongwa Kwanza kabla ya kuchinjwa shingo mithili ya kuku!
Lakini wakati mauaji hayo yakitekelezwa kulisikika makelele porini ambapo baadhi ya wananchi waliyoyasikia walielekea huko ndipo walipokutana na wauaji hao wakiwa na majambia yaliyoloa damu wakitokea porini.

Walipowaona watu hao walikimbia na kuacha pikipiki yao ambayo inashikiliwa Polisi. Katika eneo la tukio, mbali na pikipiki pia kulikutwa simu tatu za mkononi na mkoba wa mwanamke aliyeuawa.
Kwa mujibu wa taarifa, watu hao ni wageni Kaole na mpaka sasa bado miili yao haijatambuliwa!

Picha zinatisha mno ndo maana hazijatumwa humu kama una ndugu yako mwenye mtoto wa kiume umri miaka 3-5 halafu kapotea mazingira ya kutatanisha jitahidi kufuatilia.
Share:

Monday, May 2, 2016

Video: Mwanamke Afariki Guest House kwa Kulishwa Sumu na Mpenzi Wake,, Mwanaume Akimbia

Tukio limetokea Guest House Kimara Dar es salaam usiku wa May 1 2016 ambapo Mwanaume mmoja aliyeingia kwenye nyumba hiyo ya Wageni akiwa na Mwanamke, alikimbia kwa kusingizia kwenda dukani kununua vocha wakati Mwanamke huyo akikaribia kukata roho na hakurudi tena.

Wakati tunasubiri uchunguzi wa Polisi, mashuhuda kwenye eneo la tukio wamesema inavyoonekana Mwanamke huyo aliwekewa sumu kwenye chips alizokua anakula ndani ya chumba cha nyumba hiyo ya Wageni chips ambazo inadaiwa walitokanazo kwenye safari yao na kuja nazo Guest House.
Share:

Friday, April 29, 2016

Mfanyabiashara Auawa gesti Kwa Kuchomwa Kisu

Mfanyabiashara wa mazao, Eliusta Peter(40),   amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni akiwa katika  nyumba ya kulala wageni wilayani Kilombero.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea   Aprili 22  baada ya  wahudumu wa nyumba  ya wageni ya  Sayari kubaini   maiti katika chumba namba mbili.

Inadawa Aprili 20 mwanamke huyo  akiwa na kijana mmoja ambaye  jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi, walifika kwenye nyumba hiyo na kuchukua chumba kimoja wakisema  wao ni wafanyabiashara wa mazao.
 
“Mwili wa marehemu uligundulika ukiwa kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Sayari chumba namba mbili   saa 11 jioni na ulipochunguzwa ikagundulika kuwa kifo kilisababishwa maumivu ya jereha,”alisema Matei.

Mwanamke huyo  alikuwa na jeraha   kushoto mwa bega lake lililotokana na kuchomwa na kitu chenye ncha kali

Matei  alisema kwa taarifa walizozipata  bila shaka kijana aliyekuwa naye  anahusika na mauaji hayo.

Wakati huo huo, jeshi la polisi wilayani Kilosa limemkamata Rogasian Jeremia kwa tuhuma za kumshambulia mkewe,   Faustina Sizayi(25) kwa kumkatataka kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mtuhumiwa alikamatwa akiwa anajihusisha na kazi ya ulinzi wa maduka baada ya polisi kumsaka kwa muda mrefu na ndipo Aprili  24  alikamatwa  baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Share:

Wednesday, April 27, 2016

Afisa tarafa matatani kwa ubakaji

 Binti anayedaiwa kubakwa
Afisa Tarafa mmoja mkoani hapa, ameingia matatani akituhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita (jina linahifadhiwa) ndani ya ofisi yake na kumsababishia maumivu makali.
Denti huyo mwenye umri wa miaka 12, alisema afisa tarafa huyo amembaka mara tatu kwa siku tofauti na kwamba siku ya kwanza, alimuita ofisini kwake wakati akitoka shuleni.

“Asubuhi wakati tunaenda shuleni na wenzangu, tulipita jirani na ofisi yake tukamkuta akiwa nje, akawa anatukonyeza, wenzangu wakasema ndiyo kawaida yake,” alisema mwanafunzi huyo kwa uchungu na kuongeza kuwa baada ya muda wa masomo kuisha, akiwa anarejea nyumbani kwao akiwa peke yake, afisa tarafa huyo alimuita.

“Aliniuliza kama najua kucheza mchezo wa kibabababa, nikamjibu sijui, akaniambia atanifundisha, akaniingiza ofisini kwake. Nilipofika ndani alianza kuniambia ananifundisha mchezo wa kibabababa, akachukua koti lake na kuniziba mdomo nikawa nakosa hata pumzi, akanivua nguo naye akavua zake akanipakata na kuanza kunibaka
Share:

Monday, April 25, 2016

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Elimu (Duce) Auawa Kwa Kuchomwa Kisu na Mpenzi Wake


Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Elimu (Duce), jijini Dar es Salaam, Bertha Mwarabu (23), ameuawa na mwanafunzi mwenzake kwa kuchomwa kisu kwenye titi na tumboni kwa kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika hosteli za chuo hicho zilizopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.

Kamanda Kalunguyeye amemtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Masamba Musiba (27) ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho, ambacho ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Amesema mauaji hayo yalitokea juzi saa 3:45 usiku baada ya Musiba kuingia chumbani kwa marehemu ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake na kuanza kumshambulia kwa kisu.

Ameongeza kuwa baada ya marehemu kuanza kushambuliwa, alipiga kelele kuomba msaada na ndipo wanafunzi wenzake walipokwenda na kumkamata mtuhumiwa wakati akijaribu kukimbia.

Amesema kelele za marehemu, ndizo zilizowashtua wanafunzi wenzake.
 
Kamanda Kalunguyeye alifafanua kuwa marehemu alikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu lakini alifia njiani.

Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, amesema tukio la mauaji hayo ni la kwanza kutokea chuoni hapo.

Profesa Mukandala alisema tangu aanze kufanya kazi chuoni hapo kwa miaka mingi, hajawahi kushuhudia tukio la namna hiyo na kuongeza kuwa amesikitika kwa kuondokewa na mwananfunzi huyo.
Share:

Video: Mwajiri amlisha sumu mfanyakazi wake


Siku moja baada ya kituo cha afya cha Tandale kukiri kumpokea kijana Abdul Mohamed anayedaiwa kulishwa sumu na mwajiri wake na kisha kupewa rufaa katika hospitali ya Mwananyamala, kumemlazimisha mganga mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Azizi Msuya kuingilia kati swala la mgonjwa huyo baada ya kuwapo kwa taarifa zinazobabaisha.


Share:

Thursday, October 1, 2015

Ukatili! Mtoto wa darasa la nne aunguzwa na maji ya moto na shangazi yake



Mtoto Dorine anayedaiwa kuchomwa mikono na shangazi yake.
Ni ukatili ulioje ambao amefanyiwa mtoto Dorine (12), denti wa darasa la nne Shule ya Msingi Makabe, Mbezi jijini Dar.
Dorine anadaiwa kuunguzwa na maji ya moto yaliyochemshwa kwenye jiko la gesi na walezi wake wa karibu akiwemo shangazi yake aliyetajwa kwa jina moja la Scola ambaye alitiwa mbaroni na bibi yake ambaye haikujikana alipo.

Katika tukio hilo la Septemba 26, mwaka huu, Scola alidaiwa kutekeleza tendo hilo, chanzo kikielezwa ni upotevu wa shilingi 20,000.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Scola alimtaka Dorine aseme amezipeleka wapi fedha hizo, lakini binti huyo alisema hajui chochote.
Ilidaiwa kwamba, katika hali isiyokuwa ya kibinadamu, wakati Dorine akiwa anahojiwa tayari maji ya moto yalikuwa yakichemka.


Ilisemekana kwamba, baada ya kuona Dorine hataki kusema zilipo fedha hizo, Scola akamuamuru aingize mikono ndani ya sufuria lililokuwa jikoni huku maji yakichemka.
Dorine alipokataa, Scola akadaiwa kumshika kwa nguvu, akisaidiana na mama yake ambaye ni bibi wa Dorine na kuizamisha kwenye sufuria la maji mikono hiyo na kumsababishia mtoto huyo majeraha ya kutisha.
Ilisemekana kwamba, baada ya tukio hilo, familia hiyo ilifanya siri kubwa na kutompeleka hospitalini lakini baadhi ya majirani walibaini hilo na kusambaza taarifa ndipo familia hiyo ikampeleka hospitalini kwa siri.

Alipofikishwa katika Hospitali ya Kanisa Katoliki Luguruni, Mbezi mtoto huyo alilazwa baada ya mahojiano na wauguzi ambapo aliwaeleza kila kilichotokea.
Hata hivyo, maelezo ya Dorine kwamba aliunguzwa na shangazi na bibi yake yalipingwa na Scola ambaye alisema mtoto huyo alikuwa akikimbia akaangukia maji ya moto.
Taarifa alizopata mwanahabari wetu kwenye hospitali hiyo kupitia muuguzi wa zamu, zilieleza kuwa taarifa sahihi za tukio hilo ni zile alizozitoa mtoto  huyo.

Katika mahojiano na wauguzi, Dorine ambaye alikuwa amelazwa kwenye Chumba cha Stuff Na. 16 hospitalini hapo, alifafanua kuwa anaishi kwa shangazi yake  baada ya baba yake mzazi kuachana na mama  yake na baba kuoa mwanamke mwingine.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kwamba, Scola alishikiliwa na Jeshi  Polisi Kituo cha Mbezi-Kwayusuf na baadaye aliachiwa kwa dhamana lakini bibi hakukamatwa.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, RPC Camilius Wambura alipoulizwa na gazeti hili juu ya tukio hilo alikiri kulijua na kwamba alipokea taarifa za aina mbili hivyo alimwagiza OCD wa Mbezi-Kwayusuf kulifuatilia na kumpa taarifa kamili.
Alisema taarifa moja ilidai, Dorine aliunguzwa lakini ya pili ilidai aliangukia kwenye sufuria yenye maji ya moto hivyo uchunguzi unaendelea ili kupata taarifa kamili.
Share:

Wednesday, September 30, 2015

Unyama: Watu Watano wa Familia Moja Wachinjwa Kama Kuku Simiyu


Watu watano wamefariki dunia papo hapo kwa kukatwa katwa  mapanga  na kuchinjwa kama wanyama katika kitongoji cha Kisesa kata ya Bugalama wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.

Watu hao ambao ni wa familia moja walifanyiwa unyama huo kwa kukatwa katwa mapanga sehemu ya shingoni.

Akizungumza na  waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoani hapa Gemine Mushy alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 9 ambapo Baba, Mama pamoja na watoto wao 3  waliuawa.

Mushy aliwataja waliofanyiwa unyama huo kuwa George Charles (30) ambaye ni Baba wa familia, Siku John (23) Mama wa Familia na watoto wao ambao ni Mchambi George (7) Tuma George (5) pamoja na Amos George (Miezi 9) wote wasukuma wa kitongoji hicho.

Kamanda Mushy alieleza chanzo kuwa ni mgogoro wa ardhi kati ya marehemu (George) pamoja na Baba yake wa kambo ambaye alinunua kipande cha ardhi alikokuwa akiishi marehemu.

Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo jeshi la polisi lilifanya msako na kuwakamata watuhumiwa 3 ambao aliwataja kuwa ni Migata Lusalago (50) Jihelya Migata (30), Solo Kengele (31) wote wasukuma wa kijiji cha Bugalama.

Kamanda mushy alieleza kuwa waliokamatwa ni Baba wa kambo wa Marehemu pamoja na watoto wake wawili ambao ilidaiwa kuwa wameweza kushiriki katika kutenda tukio hilo la kinyama.

Katika hatua nyingine  Mushy  alisema kuwa uchunguzi wa kina unaendelea kufanyika ili kuwapata wahusika zaidi wa tukio hilo.
Share:

Thursday, December 5, 2013

UKATILI! AMUUA MPENZI WAKE KWA KUMCHOMACHOMA NA KISU BAADA YA WAZAZI WA BINTI KUMKATAA ASIMUOE....

.

KIFO cha kikatili cha mwanafunzi aliyeuawa siku chache baada ya kuhitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Luguruni na mkazi wa Kimara Golani, Dar, Sharifa Rajab (18) bado ni simanzi nzito katika familia yake.
Sharifa aliuawa kikatili Novemba 22, mwaka huu, Kimara Golani jijini Dar na mtu anayedaiwa ni mpenzi wake ajulikanaye kwa jina la Abdul (22) ambaye ni dereva wa bodaboda.
SIMULIZI YENYE MAJONZI
Akizungumza kwa masikitiko makubwa, baba wa marehemu, Rajab Abdallah alisema siku ya tukio asubuhi, yeye na mke wake wakiwa kazini, Sharifa aliondoka nyumbani hapo  bila taarifa na kuwaacha wadogo zake tu.
“Tuliporudi jioni, mimi na mama yake tulianza kuhangaika kumtafuta bila mafanikio. Mwisho tuliamua kurudi kulala japokuwa usingizi ulikataa. Unajua tena mtoto ni mtoto. Huwezi kupata usingizi wakati mwanao hujui aliko.

“Tulipanga siku iliyofuata kwenda kutoa taarifa polisi, lakini ilipofika saa kumi na moja alfajiri, tuliletewa ujumbe kwamba kuna mwili wa mwanamke umekutwa kwenye chumba cha jirani.
“Ilikuwa vigumu kusema kwamba mwili huo ni wa mtoto wetu Sharifa, tuliamini kifo kipo, lakini watakufa wengine si mtoto wetu Sharifa.

“Hata hivyo, tulifunga safari kwenda kuuangalia mwili huo. Sikuamini hata kidogo nilipogundua kwamba ni mwanangu ndiye alilala kitandani, amekufa kwa kuchomwa kisu kooni na kwenye mbavu zote, kitanda chote kilijaa damu. Sharifa alikuwa si Sharifa tena bali marehemu Sharifa,” machozi yanamlengalenga.
Anaendelea: “Inaniuma sana! Mbaya zaidi nilijua  chumba hicho ni cha  kijana ambaye ni dereva wa bodaboda, anaitwa Abdul. Nikajiuliza ina maana alikuwa ni mpenzi wake? Sikupata jibu.”
TABIA YA MAREHEMU
Baba wa marehemu aliongeza kuwa, kwa kipindi chote cha uhai, Sharifa  hakuwahi kuonesha dalili kwamba alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi, alikuwa ni msiri sana.

MTUHUMIWA WA MAUAJI AACHA UJUMBE
Habari zaidi zilidai kuwa, baada ya mtuhumiwa huyo kutekeleza mauaji ya binti huyo aliacha ujumbe wa maandishi akisema kuwa watu wasihangaike kumtafuta kwani na yeye anakwenda kujiua.
Hata hivyo, mtuhumiwa hakwenda kujiua, badala yake alifika Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani (UBT) kutafuta usafiri wa kurudi kwao Tanga lakini alipokosa aliamua kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Ubungo na kukiri kuua.

Mmoja wa viongozi wa serikali ya mtaa (hakutaka kutaja jina lake) alisema mtuhumiwa huyo alipohojiwa polisi alisema hajui kilichotokea, akaomba apewe nafasi akamzike mpenzi wake huyo.

KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni,  ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo alisema kwa mujibu wa mtuhumiwa alifanya kitendo hicho kutokana na wazazi wa msichana huyo kukataa yeye asimuoe na tayari alikuwa na mchumba mwingine.

Marehemu Sharifa alizikwa Novemba 24, mwaka huu katika Makaburi ya Golani Nzasa, Dar. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.

GPL
Share:

Tuesday, November 12, 2013

MWENYEKITI WA CCM ATOLEWA UTUMBO NA WAMANG'ATI WALIOKAIDI AMRI YA KUTOPITISHA MIFUGO YAO BARABARANI.....


MWENYEKITI wa CCM Kijiji cha Chole wilayani Kisarawe, Pwani, Kondo Shamte (36) yuko katika hali mbaya baada ya kuchomwa mkuki tumboni na wafugaji wa kabila la Wamang’ati na kusababisha utumbo wake kuwa nje.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ambaye kwa nafasi yake kijijini hapo ndiye anayeheshimika zaidi, tukio hilo lilijiri Agosti 28, mwaka huu.
 
Akizungumza kwa masikitiko makubwa nyumbani kwake kijijini hapo, Kondo alisema katika kijiji hicho kulijengwa barabara na wahisani (hakuwataja jina). Wanakijiji wakaombwa kuitunza barabara hiyo kwa masharti kwamba wasipitishe mifugo.

Alisema siku ya tukio, wafugaji hao walipitisha mifugo katika barabara hiyo licha ya amri iliyokuwepo, alipoona hali hiyo aliwafuata na kuwaomba wapitishe pembeni.
 
“Walikataa, nikaamua kuwatuma wajumbe wangu wawafuatilie kwa nyuma ili wasiendelee kupitisha mifugo hiyo,” alisema mwenyekiti huyo.

Akaendelea: “Baada ya wafugaji hao kuona nimetuma wajumbe wakarudi hadi nilipokuwa nimesimama na kuniambia kuwa niliwatuma wale wajumbe ili wakawafanyie fujo, wakatoa vitisho kwamba ule ndiyo ungekuwa mwisho wangu.
 
Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa kabla yeye hajazungumza chochote, mfugaji mmoja alichomoa mshale na kumrushia ambapo ulimwingia tumboni kisha wote wakakimbia.
 
Alisema alijitahidi sana kuutoa mshale huo huku tayari akiwa ameanguka chini. Alipofanikiwa, ndugu na jamaa nao walitokea na kumkimbiza Hospitali ya Kisarawe.
 
“Pale hospitalini Kisarawe ilishindikana kunitibu, nikakimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Dar es Salaam) ambako nilifanyiwa upasuaji mkubwa kwa kukata  sehemu ya utumbo iliyoharibika,” alisema.
 
Mwenyekiti huyo aliendelea kuweka wazi kwamba baada ya operesheni hiyo daktari alimwambia ni lazima sehemu ya utumbo utolewe nje mpaka sehemu ya ndani ipone vizuri ndipo waurudishe, hivyo kwa sasa haja kubwa anaitolea ubavuni.
 
“Hivi sasa haja kubwa natolewa kwa hapa ubavuni mpaka nitakaporudi tena hospitali mwezi Desemba, mwaka huu,” alisema.
 
Hata hivyo, Kondo alisema kitu kinachomuuma zaidi ni kutomuona kiongozi wa CCM hata mmoja aliyefika nyumbani kwake kumjulia hali wala kumpa msaada wowote kwani hivi sasa yuko katika hali ngumu ya kimaisha kutokana na gharama za kutibu kidonda chake kuwa juu.  


Credit-Global publisher
Share:

Friday, November 8, 2013

PICHA ZINTISHA..!! KIJANA ACHINJWA KAMA KUKU KISHA WAUAJI WAONDOKA NA KICHWA CHAKE..!!

MATUKIO ya mauaji ya kikatili yameendelea kushamiri mkoani Rukwa, baada ya watu wasiojulikana kumuua kikatili mtu mmoja kwa kumchinja  na kutokomea kusikojulikana na kichwa cha mtu huyo.


 
Baadhi ya askari polisi wakitelemsha maiti ya mtu ambaye ameuawa  kwa kukatwa kichwa na watu kutoweka na kichwa chake usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kuhifadhi katika hchumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya mkoa iliyopo mjini Sumbawanga.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa watu hao baada ya kufanya mauaji hayo walikwenda kumtupa kwenye eneo hilo ambapo asubuhi ya kuamkia leo ndio kiwiliwili chake kilibainika kuwepo hapo lakini hakina kichwa kwani waliondoka nacho.

Kwa upande wake, Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema kuwa polisi inaendelea kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo hili hatua ziweze kuchukuliwa

Share:

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger