Showing posts with label bongo. Show all posts
Showing posts with label bongo. Show all posts
Friday, October 11, 2013
Sunday, May 12, 2013
UPDATE: MATOKEO MABOVU YA KIDATO CHA NNE KUCHELEWESHA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA...!!
Matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yaliyotarajiwa kutangazwa mwezi huu yatachelewa ili kutoa nafasi kwa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kurekebisha matokeo mabaya ya mitihani kidato cha nne ya mwaka jana yaliyofutwa na serikali mwezi huu.
Matokeo ya kidato cha sita ambayo huwa yanatangazwa mwanzoni mwa mwezi Mei mpaka sasa hayajatolewa na kwamba hayatatangazwa mpaka matokeo mapya ya kidato cha nne yatakaporekebishwa rasmi.
Matokeo ya kidato cha sita ambayo huwa yanatangazwa mwanzoni mwa mwezi Mei mpaka sasa hayajatolewa na kwamba hayatatangazwa mpaka matokeo mapya ya kidato cha nne yatakaporekebishwa rasmi.
Alipoulizwa juu ya suala hilo, Naibu Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Philipo Mulugo alisema ingawa wakati huu ndio unaopaswa yatangazwe matokeo ya kidato cha sita haitafanyika hivyo hadi yatangazwe matokeo mapya ya kidato cha nne baada ya kufutwa.
Hata hivyo, akasema huenda yakatolewa pamoja au yakafuata wakati mwingine lakini mara baada ya kukamilisha kazi ya kurejea na kusahihisha matokeo ya kidato cha nne.
"Siyo kwamba yamechelewa kwani muda wa kujiunga na chuo ni Septemba hivyo haitawaathiri kwa hilo," alisema Mulugo.
Kuhusu hatma ya wanafunzi wa kidato cha nne ambao wapo mashuleni wanaendelea na masomo ya kidato cha sita, alisema kama kutakuwa na wanafunzi ambao wapo madarasani shule zilizowasajili zitakuwa hazijafuata mfumo wa elimu unavyoelekeza.
Alifafanua kuwa mfumo wa elimu kwa kidato cha nne ulibadilishwa na kwamba endapo mwanafunzi akifaulu anatakiwa kujiunga rasmi kidato cha sita Julai na si vinginevyo.
Alisema licha ya ucheleweshaji wa matokeo hali hiyo haikuwaathiri wanafunzi hao kwa kuwa ratiba ya kwenda masomoni haijaanza kwa mujibu wa kalenda ya shule ya serikali.
Serikali ilifuta matokeo ya kidato cha nne ya 2012 na kuiagiza Necta kuyaandaa upya kwa kutumia utaratibu wa usahihishaji na upangaji madaraja uliotumiwa mwaka 2011
Taarifa ilisema mfumo uliotumika mwaka jana na kusababisha wanafunzi kushindwa vibaya haukufanyiwa utafiti na maandalizi ya kutosha kabla ya kutumika.
Matokeo hayo yaliyotangazwa mwezi Februari mwaka huu yalionyesha kuwa asilimia 60 ya wanafunzi walishindwa mtihani.
Wednesday, May 8, 2013
SKENDO: MWALIMU AUAWA BAADA YA KUZINI NA MKE WA ASKOFU...!!
Kakamega, Kenya
KUNDI la watu wenye hasira huko Kakamega lilimpiga hadi kumwua mwalimu ambaye alibambwa akifanya mapenzi na mke wa askofu.
Askofu huyo alikuwa akiendesha ibada ya mazishi kijijini Tomboo, Jimbo la Malava.
Mkuu wa Wilaya ya Kakamega Kaskazini, Gideon Ombongi , alisema mwalimu huyo na mke wa askofu walitoroka kwenye mazishi na kuingia nyumbani kwa askofu huyo ambapo ni mita chache tu kutoka mazishini.
Baada ya kukamilisha ibada ya mazishi, askofu aliingiwa wasiwasi na kuamua kumtafuta mkewe alipokwenda. Alipofika nyumbani kwake aliwakuta wawili hao wakifanya mapenzi jikoni.
Mapigano yalitokea kati ya askofu na mwalimu huyo ambapo mwanamke alikimbia.
Mkuu wa Polisi wa Kakamega Kaskazini, Justus Kitetu, alisema mapigano hayo yalivutia watu ambao walijaa kwenye nyumba ya askofu.
“Askofu aliwaambia wanakijiji kilichokuwa kimetokea nao wakampiga mwalimu na kumwua,” alisema na kuongeza kwamba askofu amekatwa kwa uchunguzi. Mke wa askofu naye alikamatwa lakini aliachiliwa.
Tuesday, May 7, 2013
"MIMI NI LEGEND WA BONGOFLEVA.....NITASHIRIKIANA NA LADY JAYDEE BEGA KWA BEGA.....SIWEZI KUFUATA MANANEO YA RUGE"....PROFESSA J.
Lady Jay Dee Professa Jay
Fahamu hiki alichokisema professa Jay kuhusu miaka 13 ya Lady Jay Dee Baada ya Lady Jay Dee
Fahamu hiki alichokisema professa Jay kuhusu miaka 13 ya Lady Jay Dee Baada ya Lady Jay Dee
kutangaza siku ya kuachia album yake mpya sasa #Fahamu . Professa Jay kuhusu miaka 13 ya Lady Jay Dee "Nitakuwa na @JideJaydee kwenye show yake ya miaka 13 ya LADY JD, Kwa NGUVU zangu zote, AKILI zangu zote na UWEZO wangu wote, KARIBUNI SANA"
Monday, May 6, 2013
BAADA YA CLOUDS KUGOMA KUPIGA NYIMBO ZA BONGO FLEVA LEO, TIMES FM WAWAJIBU KWA KUSEMA "LEO SISI NI BONGO FLEVA MPAKA KUCHWEE, HASIRA YA MKIZI FURAHA KWA KUNGURU"......!!
Kwa Kutumia Kilicho chetu , Asili yetu na Muziki wetu leo katika vipindi vyote utaskikia muziki wa nyumbani wa BONGO FLEVA kwa asilimia Kubwa.
Sunday, May 5, 2013
LINAH NA BARNABA WASUSIA SHOW YA MIAKA 13 YA LADY JAY DEE...!!
Linah na Barnaba wameiambia Bongo5 kuwa hawatakuwepo kwenye show ya miaka 13 ya muziki ya Lady Jaydee itakayofanyika May 31, kwa kile walichodai ni kutoafikiana kwenye malipo.
Wamesema licha ya kuendelea kuwepo kwa majina yao kwenye poster ya show hiyo, hawatotumbuiza siku hiyo.
“Dada yetu alituita, akatuambia kwamba ana kazi yake ya kutumiza miaka 13 kwahiyo akawa anasema anahitaji wasanii ambao watamsupport kwaajili ya kufanya show,” amesema Linah. “Sisi tulifuata protocol zote kwasababu kama wasanii tuna viongozi, tukafuata protocol zote kuweza kukubaliana naye mpaka tukafikia hatua kwenye masuala ya biashara, yaani malipo. Kwenye upande huo kidogo tukawa tumepishana, kwenye upande wa masuala ya maslahi. Lakini sasa tunashangaa yeye kuanza kuweka posters.”
Kwa upande wake Barnaba amesema hawajashindwana na Lady Jaydee lakini wao kama wasanii wana menejementi na matakwa ya ofisi zao na hivyo muafaka ulishindwa kufikiwa na pia walikuwa na booking zingine.
Hata hivyo Barnaba amesema hakuna ugomvi wowote baina yao na Lady Jaydee. “Tuko safi tu na dada, mbona tuliafikiana vizuri tu na tuko kwenye maongezi mazuri tu, tulishaongea na hili suala liko vizuri,” amesema Barnaba.
Friday, May 3, 2013
NGASSA AINYIMA USINGIZI SIMBA, ADAI HANA MKATABA NAO TENA....!!
UONGOZI wa Klabu ya Simba umetamka na kusisitiza kuwa kiungo wao, Mrisho Ngassa, amebakisha mkataba wa mwaka mmoja zaidi klabuni hapo, lakini mchezaji huyo amesema hana mkataba.
Simba imetoa tamko hilo baada ya kiungo huyo kutangaza dau la shilingi milioni 150 kwa timu itakayomhitaji ikiwemo Simba kutokana na mkataba wake kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zakari Hans Pope amesema Ngassa bado ana mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea timu hiyo na kudai kushangazwa na taarifa anazozitoa kiungo huyo kuwa mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, kitu ambacho siyo sahihi.
Aliongeza kuwa kama Ngassa anataka fedha nyingine za kumuongezea ni vema akauambia uongozi na siyo kuzungumza kwenye vyombo vya habari.
“Ngassa ni mchezaji halali wa Simba mwenye mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea timu yetu, kama unakumbuka tulimchukua Azam kwa mkopo kisha tukamuongezea mkataba mwingine wa mwaka mmoja,” alisema Hans Pope.
Wakati Hans Pope akitamka hayo, Ngassa amekuwa akisisitiza mara kwa mara kuwa hakusaini mkataba wa ziada klabuni hapo na kudai kuwa atakuwa huru mara baada ya msimu huu kumalizika.

Tuesday, April 30, 2013
HAMMER Q AMCHAKAZA NA KUMTOA MANUNDU MKEWE MARA BAADA YA KUMTAMBULISHA KWA TX MOSHI...!!
Nguo za Hammer Q zikiwa zimetapakaa damu
Hiki ni kipigo ambacho Salha alikipata baada ya kumtambulisha rafiki yake wa kiume ambae ni Tx Moshi kwa mumewe Hammer Q.
Baada ya utambulisho huo....sinema ya ngumi na mateke ilianza....
Inavyosemekana alimpiga mateke, mangumi, akampasulia kioo kichwani, kampiga na jiko la mkaa kichwani