Wednesday, March 6, 2013

PENNY AANIKA KILICHOMFANYA DIAMOND AMUACHE WEMA, ADAI CHANZO NI WEMA MWENYEWE...!!

SIRI ya Mtangazaji wa Televisheni ya DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ kumpindua Wema Isaac Sepetu kwa mwanamuziki Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ imevuja huku Wema mwenyewe akidaiwa kuchangia.
Diamond akiwa na Penny.

Mmoja wa marafiki wa Wema aliyeomba hifadhi ya jina alimtonya mwandishi wetu hivi karibuni kuwa, chanzo cha Penny kumnasa Diamond ni tabia ya Wema kupenda kumsifia sana Diamond kwa Penny huku akitoa siri asizostahili kuzianika kwa marafiki zake wa kike.

Alisema, Wema na Penny walikuwa marafiki (picha ukurasa wa nyuma zinathibitisha) na kwamba Wema alikuwa akimringishia mwenzake jinsi Diamond anavyojua kubembeleza na kumjali mwanamke na hapo ndipo mtangazaji huyo akafanya mapinduzi.

“Wema alikuwa  akimsifia Diamond kuwa anajua mapenzi na wanawake wengine wakishaambiwa hivyo huwa wanafanya wawezavyo kumnasa mwanaume huyo.
Wema akiwa na Penny.

“Ndicho kilichotokea kwani alichokifanya Penny ni kumtega Diamond na hatimaye akamnasa. Ndiyo maana tunashauriwa kutowasifiasifia waume zetu mbele za marafiki zetu wa kike kwani ndiyo mwanzo wa kuibiwa,” alisema sosi huyo.

Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Wema kuzungumzia madai hayo lakini hakupatikana huku simu ya Penny ikiwa haipatikani.
Wema na Diamond wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu lakini katika siku za hivi karibuni Diamond amehamia kwa Penny.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger