Basi
la Abiria la Kampuni ya TAHMEED linalofanya safari zake kati ya Tanga-
Dar es Salaam, limeteketea kwa moto katika barabara ya Chalinze- Segera.
Taarifa
kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa hakuna mtu aliyefariki wala
kujeruhiwa kutokana na ajali hiyo lakini mizigo ya abiri ndiyo
imeteteketea ndani ya basi hilo.
Ajali imetokea wakati basi hilo
likiwa limesimama baada ya Abiria mmoja kuomba Msaada akajisaidie
(kuchimba dawa) na ndipo abiria waliokuwamo ndani ya gari alianza
kusikia harufu ya moshi wa tairi linaloungua na ndipo wakatoka nje ya
gari na muda mfupi gari lote likashika moto.
0 comments:
Post a Comment