STAA wa sinema za
Kibongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa ameeleweka vibaya alipoandika
mitandaoni kuwa hajawahi kununua simu za bei mbaya zaidi ya kupewa na
watu.
Baada ya kuweka maneno hayo na watu
kumnanga kuwa amezoea kuhongwa na hajawahi kununua simu za ‘maana’,
alizungumza na mwanahabari wetu na kufafanua:
“Kiukweli simu nyingi za kisasa nimekuwa
nikipewa na ndugu, jamaa na marafiki na si kuhongwa na mabwana kama
wengi walivyomsema,” alisema Shamsa.
0 comments:
Post a Comment