Thursday, December 20, 2012

AUNT LULU AJUTA KUMKOSA KOFFI..


MTANGAZAJI mwenye matukio ya kumwaga Bongo, Lulu Mathias ‘Aunt Lulu’ alinaswa akihangaika kumtega mwanamuziki kutoka Kongo, Koffi ili aingie mkenge


Lulu Mathias ‘Aunt Lulu’.
Ishu hiyo ilipigwa chabo na paparazi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar wakati mwanamuziki huyo alipokuwa akifanya shoo yake.


“Lengo la Aunt Lulu aliyevaa vazi lililomuacha mgongo wake kujipitishapitisha back stage alipokuwa amekaa Koffi lilikuwa kumnasa msanii huyo lakini hadi anapanda jukwaani hakufanikiwa hata kuongea naye,” alisema sosi aliyemshuhudia.
Alipoulizwa kuhusu ishu hiyo na paparazi wetu, Aunt Lulu alifunguka:
“Wewe chezea mimi, mwenyewe alidata na mapigo yangu, sema ndiyo hivyo alikuwa bize na shoo, najuta kumkosa” alisema Aunt Lulu mwenye shepu ya peke yake.

SOURCE: GPL
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger