Showing posts with label WOLPER. Show all posts
Showing posts with label WOLPER. Show all posts

Tuesday, May 3, 2016

Picha: Jack Wolper Awapa Suprise Mashabiki Wake Kwa Kupost Picha Zinazoonyesha Kuwa ni Mjamzito

Zikiwa zimepita siku kadhaa toka Jack Wolper atupe somo la mapenzi kipindi hichi cha baridi leo amewapa Suprise Mashabiki Wake Kwa Picha Hizi za Ujauzito, Jack Wolper inasemekana kwa sasa yupo South Africa na Mkongo Man....Hongera Jack.

Share:

Friday, April 29, 2016

Wolper atoa sababu iliyomfanya apunguze kuvaa nguo za kiume

Kweli ujana ni maji ya moto. Mwigizaji kutoka kiwanda cha filamu bongo, Jacqueline Wolper amesema mchumba wake ndiye sababu iliyomfanya apunguze kuvaa nguo za kiume.

Miaka kadhaa nyuma CV ya Wolper ilichafuliwa na skendo zilizokuwa zinamiuandama kuwa yeye ni msagaji japo mara nyingi mwenyewe amekuwa akizikana hizo taarifa kuwa hazina ukweli wowote.

Akiongea kwenye kipindi cha Nirvana, kinachoruka kupitia EATV, Wolper alisema ‘nilikuwa navaa vile kutokana na wakati ule, sasa hivi nimeshakuwa na mchumba’.

“Nilikuwa navaa vile kutokana na wakati ule ulivyokuwa. Kuna watu walikuwa wanapenda, lakini sasa hivi nimeshakuwa mchumba wa mtu. Ni kweli lazima nivae gauni, kwahiyo mtu unatakiwa ujibadilishe wewe mwenyewe usisubiri kubadilishwa,” aliongezea.

Wolper aliendelea kusema, “hata hivyo bado sijaacha kabisa, kidogo unakuwa unagusia mashabiki zako wanakuwa wanakupenda.”
Hata hivyo Wolper japo amekiri kuwa na mchumba mpya kwa sasa lakini hayupo tayari kuweka mahusiano yake hadharani kama mwanzo alivyokuwa anafanya.
Share:

Thursday, April 28, 2016

Mrembo Jack Wolper Afunguka Kuhusu Pete...Adai Amejifunza Kusugua Goti Kwani Mambo ya Ndoa Mungu tu Ndio Anajua

Jack Wolper Ametoa Somo zuri kuhusu pete ya uchumba wanazovalishwa wadada na kufungwa nazo.Ameweka picha hii hapa chini na kuandika maneno yafuatayo:


"Trully witchcraft and am sure wanaume wanafanya hivi ili awe na uhakika upo hapo tu unamsubiri wakati yeye anaponda maisha yake

Na mwisho wa siku wengine wanaenda kuoa kwingine sio alikovalisha pete
Binafsi naomba tujitahidi sisi wakina dada (hata mimi najishauri) kutokusimamia ahadi pekee and put your life pending.. You love him COOL

He loves you back EVEN BETTER
ILA ilo lisikufanye ukasimamisha maisha yako kwajili yake... Anataka kukuchumbia kubalianeni whats way forward then Mjipange kwa pamoja kuelekea lengo lenu... Engagement sio one person goal (sio wajibu wa mwanaume pekee kusimamia uchumba wenu na kujua lini utafkia ndoa, ni maisha ya wote wawili na hivi vitu ulizeni hata wazazi wetu VINAPANGWA, vinajadiliwa na vinawekewa kipindi cha kutimiza) mwanzo tamaduni ilikua ni kuchumbia kwa muda tu then ndoa ila siku hizi unaweza parara hata miaka nane na pete mwanaume hana hili wala lile, na sisi kinadada tunavyojua kuachia moyo unakuta maskini hata ukitongozwa unakataa kwakua unajua una mchumba wako.. Unaweka DP ya pete na kumshukuru Mungu... Huku mwenzio anajua ame seal deal anaanza kupeta mtaani na wengine... Si anapata all the benefits.. Tayari ana mke "majukumu" kuna tofauti ya mke wa ndoa na mke wa majukumu..

Utampikia utamfulia utafanya kila kitu ila Mungu pishia mbali akidondoka leo hii itabaki Marehemu alikua hana ndoa wala mtoto... Tena worst ni wale unakuta umeshazaa nao ndo balaa.. Yaani Mungu tunusuru tu sisi waja wako

Kwakweli inabidi wapenzi tubadilike Sio unakubali kupokea lipete la mtu unakaa nalo faithful kumbe mwenzio ana macommitment yake uko anakopajua

Women are strong and we can make it on our own, ndoa ni nzuri na bonus tu
Cha muhimu kupambana usimamishe maisha yako hayo mengine yanakuja tu
Kama kimepangwa imepangwa na kama haijapangwa hata ubinuke haiwezi kua
Ndio maana mimi siku hizi nimejifunza kusugua goti, haya mambo ni Mungu pekee ndio mwenye jibu la mwisho na sahihi.

Lets just pray na kama umeolewa pray for your sisters na hata wanao wa kike..
Kwakweli mahusiano siku hizi yanahitaji Mungu kupita kiasi" Jack Wolper
Share:

Wednesday, October 9, 2013

JACKLINE WOLPER KUJA NA MOVIE MPYA.....

jack wolper         Jack wolper Mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI wa kike anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper aka Wolper Gambe ameingia mzigoni na kuibuka na staili kama ya gwiji la muziki na filamu ulimwenguni hayati Whitney Houston pale aliposhuka na bonge la movie la Bodyguard na sasa Jack naye kaigiza kama mtoto wa Mh. Rais ni mzigo kutoka kampuni ya RJ Company chini ya Director Ray.

.

jacck 600 b
jack wolper 600
Jack Wolper, Salha Israel, Sudi MuhogoWolper Gambe akiwa katika picha ya pamoja na walinzi wake katika movie la Kiikulu.
Wakati mkali huyo akifanya yake ni kwa support ya mlimbwende wa kitambo Bongo Salha Israel akisimama kama mlinzi wa binti wa kishua ni movie ambayo itatikisa na kuandika historia ya kipekee sana, kumbukumbu zinaonyesha kuwa Jack Wolper kila mzigo anaoshiriki unakuwa ni moto wa kuotea mbali kulingana na staili yake ya kubadilika kwa kila filamu.
Kila heri kwa Jack Wolper Salha miss 2011 na washiriki wote wanaopiga mzigo na kamanda Ray the Greatest kutoka RJ Company ni shughuli mwanzo mwisho , tutakupa nyeti kuhusu movie hili stay tune soon!
Share:

Monday, May 27, 2013

JACK WOLPER ALIA NA MATAPELI YANAYOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA JINA LAKE KUOMBA HELA WATU

Katika kile kinachoonekana ni mwendelezo wa matapeli wa mjini kutumia majina ya waigizaji maarufu nchini kutapeli watu kwa njia ya mtandao, dhahama hii sasa imemkuta mwanadada Jacqueline wolper baada ya watu wanaoaminika kuwa ni matapeli kutumia jina lake kujipatia fedha na vitu vingine kiudanganyifu.
Akizungumza kwa simu na tovuti ya bongomovies, mwanadada Jacqueline wolper  alisema matapeli hawa sasa wameamua kutumia mtandao wa instagram na mtandao mwingine wa kijamii uitwao badoo kwa jina la “wolper gambe25” katika kutapeli watu kwa kuwaomba hela au michango mbalimbali kupitia account hizo feki

“Leo nilikuwa naenda saluni, baada ya kufika tuu, yule dada wa saluni akaanza kunilalamikia kuwa mbona sijaenda kuchukua viatu nilivyomuagiza pamoja na hela? 


 
Nikawa sijui cha kumwambia maana sikumuagiza viatu na wala sijampigia simu kumwambia anitumie hela, ndipo aliponionesha huo ujumbe kwenye simu yake na ndio nikagundua hizo account feki za hao watu wanaoutumia jina langu kutapeli watu” Alisema Jack.

“Mimi sipo facebook na wala sitarajii kujiunga, nawaomba sana mashabiki wangu wajue hilo. Natumia mtandao wa instagram kwa jina la wolpergambe au jacklinewolperjacklinewolper.”
Alisisitza Wolper

Pia alisema kuwa amegundua leo kuna mtu mwingine anayetumia jina lake kuomba watu wamchangie kuhusu kampeni inayoitwa “Zinduka” na amewataka sana mashabiki wake wasije wakafanya hivyo kwani mtu huyo ni mwizi na analengo la kumchafulia jina lake.

Share:

Friday, May 24, 2013

JACKLINE WOLPER NA BABY MADAHA WASHIKANA MASHATI WAKIGOMBANIANA NYUMBA YA KUPANGA


Sakata la wawili hao lilifika polisi na kubainika kuwa Madaha alilipa kodi kwa tapeli wakati Wolper alitoa fedha zake kwa mwenye nyumba hivyo kumfanya awe na haki ya kuhamia.
 

Akizungumza na mwandishi wetu, juzi jijini Dar es Salaam, Madaha alisema pamoja na kubainika kuwa alitapeliwa, mtu pekee ambaye angeweza kumsaidia kupata fedha zake (shilingi milioni tatu) ni Wolper lakini anamchenga.

“Ni kweli nimetapeliwa lakini Wolper kama msanii mwenzangu alikuwa na uwezo wa kunisaidia maana yeye anaishi pale lakini nimemwambia, ananipiga chenga. Sitaongea naye milele, hana utu kabisa. Milioni tatu ndugu yangu si pesa ndogo.”


KAULI  YA  WOLPER

Wolper alipotafutwa na kusomewa malalamiko ya Madaha alisema: “Naweza kusema Madaha hana akili, ni mpuuzi kwa sababu angekuja kwa busara nyumbani kwangu tungezungumza na baba mwenye nyumba tukajua namna ya kumsaidia.

“Lakini yeye kabla hajaomba ushirikiano kwangu, tayari naanza kusumbuliwa na magazeti kuwa eti nimemtapeli. 

Halafu hajawahi kunipigia simu bali alikuwa anawatuma watu wake kwangu. Kwa nini asingekuja mwenyewe?
 

“Ina maana yeye ni staa sana au? Huyu hana lolote anataka kupanda kwa kutumia jina langu,” alisema Wolper.
Share:

Monday, May 6, 2013

AIBU: JACQUILINE WOLPER ATUPIWA VIRAGO VYAKE NJE BAADA YA KUSHINDWA KULIPA KODI YA NYUMBA.....!!

STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kutupiwa nje na baadaye kuzuiliwa vyombo vyake kwenye ile nyumba ya kifahari ya kupanga aliyokuwa akiishi Mbezi Beach, Dar es salaam.

Madai hayo yalitua kwenye dawati la Ijumaa Wikienda hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa ishu hiyo ilijiri maeneo hayo baada ya bishosti huyo kudaiwa kuwa alishindwa kulipa kodi ya pango ya mwezi mmoja ambayo ni Dola 1,500 (zaidi ya Sh. milioni 2.4 za madafu).
Kwa mujibu wa ‘sosi’ wetu aliyekuwepo eneo la tukio, Wolper aliwatuma ndugu zake kwenda kuchukua vyombo hivyo lakini walipofika mama mwenye nyumba (jina tunalo), aliwazuia na kumpigia simu staa huyo akimwambia kuwa anatakiwa kulipa fedha kabla ya kuchukua vitu vyake.



 
“Wolper alipopigiwa simu alikuja juu na kumwambia mama mwenye nyumba kuwa kama anamfuatilia eti atamfunga kama mume wa mama huyo alivyofungwa na kumwambia kuwa atampelekea polisi wakamkamate,” alidai mtu huyo.
Sosi huyo aliendelea kudai kuwa baada ya kuona soo limekuwa la kutishana, mama huyo alikwenda kumfuata mjumbe wa nyumba kumi aliyefahamika kwa jina moja la Musa na kumueleza kisha kumuomba asimamie zoezi hilo.
Baada ya kujazwa data hizo, Ijumaa Wikienda lilifanya jitihada za kumsaka Wolper na alipopatikana alisema kuwa hajawahi kudaiwa na huyo mama na anayesema hivyo huenda alimuona wakati anahamisha vitu vyake kwani kwa sasa amehama kwenye nyumba hiyo.
Mwandishi wetu hakuishia hapo, alimtafuta shemeji wa mama mwenye nyumba aliyetajwa kwa jina moja la Jamal ambaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo na kwamba suala hilo lilimalizika ambapo vyombo vya Wolper vilitolewa kwa ajili ya kufanya usafi kwani kuna mtu mwingine alikuwa akihamia.
Mjumbe wa Nyumba Kumi, Musa alipotafutwa kwenye simu yake ya kiganjani ili kuzungumzia sakata hilo alikiri kufikishiwa malalamiko ya Wolper.
Alisema kuwa msanii huyo alikuwa hajamaliza kulipa fedha, akawatuma ndugu zake wakachukue vitu vyake lakini kabla hawajavichukua mama mwenye nyumba aliwazuia mpaka alipwe chake na alipotimiza hilo ndipo akaachiwa vitu vyake.
Share:

Friday, May 3, 2013

"NAJUTA KUJIINGIZA KWENYE MAPENZI"...!!

DIVA wa kiwango cha juu cha filamu hapa Bongo, Jacqueline Wolper, ameonekana kujutia historia yake ya kimapenzi baada ya kufungukia kitendo cha yeye kumuanika kila aliyekuwa akimpenda kwamba kimemtibulia na sasa amejifunza kutokana na makosa.
Jacqueline Wolper.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Wolper alisema kuwa, kwenye maisha yake ya huko nyuma ameshajianika akiwa na wapenzi tofauti lakini sasa atakayempa nafasi kwenye moyo wake hatamuanika ila hilo litakuja baadaye sana kwani sasa hivi kaweka pembeni kwanza mambo ya mapenzi.
“Sitaki yajirudie yaliyotokea katika maisha yangu ya huko nyuma, hata hivyo sasa hivi niko bize sana na kazi, mambo ya wanaume nimeamua kuyaweka pembeni kwanza,” alisema Wolper na kuongeza:
“Sitaki itokee kama ilivyokuwa kwa Dallas ambapo kila mtu alijua alikuwa ni mtu wangu, kwa sasa nimeamua kutulia kwanza na hata nikimpata mwingine watu hawatamjua hadi wakati wa ndoa.”
Share:

Sunday, April 28, 2013

"UREMBO SIYO KIPAJI NA SI KILA MWANAMKE MZURI ANAWEZA KUIGIZA"...JACKLINE WOLPER



Muigizaji Jacqueline “Jackie” Wolper amewashangaa wanaodhani kuwa urembo wa mwanamke ni mbadala wa kipaji hasa katika sanaa ya maigizo. 
Alisema urembo ni moja ya sifa ya mwanamke lakini kamwe hauwezi kumfanya asiye na kipaji kuwa nacho.“Ukiwa mrembo ni bora zaidi,kwa kuwa itamfanya avutie kwenye movie,lakini pamoja na hayo ni lazima awe na uwezo wa kuigiza kulingana na kipande husika”alisema Wolper. 
  Wolper aliendelea kulalama kuwa kila mtu akijona ana sura ya kuvutia na umbo zuri basi anajua anaweza kuigiza ndio maana matokeo yake wanafanya vitu sivyo na mwisho wake wanaacha fani kabisa. 
  Alifafanuwa kuwa kuigiza ni zaidi ya urembo hivyo yeyote ambaye anafikiri anaweza kufanya kazi hii kwa uzuri wa sura na umbo ajaribu kama hakuchemka.
Source: Mwananchi
Share:

Thursday, April 4, 2013

MAUNO YA WOLPER WOLPER YAWACHENGUA WATU UKUMBINI


VIUNO alivyokatika  staa maarufu wa filamu, Jacqueline Wolper viliwachengua ile mbaya watu waliohudhuria harusi ya wasanii maarufu wa Bongo Movies, Jimmy Mafufu na Idrissa Makupa ‘Kupa’.
 
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Ukumbi wa Urafiki uliopo Ubungo, jijini Dar baada ya  wasanii kwenda mbele ya ukumbi kwa zamu na kuonyesha uhodari wa kuyarudi mangoma ambapo ilipofika zamu ya Wolper, alionekana kuwazidi wenzake kwa utundu wa kucheza.
Baada ya kuonesha vitu adimu ambavyo havikuoneshwa na staa yeyote kati ya waliomtangulia, wageni waalikwa walishangilia na kupiga makofi hadi aliporejea sehemu aliyokaa awali.

 
Share:

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger