Mzee majuto ambaye amejipatia umaarufu sana kwa
uigizaji hususani katika Comedy ametoa kauli rasmi kuwa kwa sasa ameamua
kuachana na kazi hiyo ya uigizaji na sasa kumtumikia Mungu na kuomba
asamehewe makosa kwa yale aliyotenda nyuma.
Mzee
Majuto amesema kuwa kwa sasa anaamini anaweza kuishi bila kutumia
kipaji chake hicho cha ugizaji na muda huu atatumia kumuomba Mungu
amsamehe makosa aliyotenda na kudai kuwa anaamini itawezekana kwani
Mungu ndiye anayetoa ridhiki kwa kila mtu.
Mashabiki zangu nawaomba wawe na amani tu kwa maamuzi yangu haya kwani hakuna kitu ambacho kinaishi milele kwani ni Mungu pekee ndiye anayeweza kuishi milele, imefika wakati nimeamua kumpuzika na kumtumikia Mungu, naamini maisha yatakwenda kwani kuna watu ambao hawana vipaji ila wanaishi vyema, wanatibiwa na maisha yao yanakwenda salama hivyo hata mimi nitaishi vyema' alisema Mzee Majuto.
0 comments:
Post a Comment