Kweli ujana ni maji ya moto. Mwigizaji kutoka kiwanda cha filamu
bongo, Jacqueline Wolper amesema mchumba wake ndiye sababu iliyomfanya
apunguze kuvaa nguo za kiume.
Miaka kadhaa nyuma CV ya Wolper ilichafuliwa na skendo zilizokuwa
zinamiuandama kuwa yeye ni msagaji japo mara nyingi mwenyewe amekuwa
akizikana hizo taarifa kuwa hazina ukweli wowote.
Akiongea kwenye kipindi cha Nirvana, kinachoruka kupitia EATV, Wolper
alisema ‘nilikuwa navaa vile kutokana na wakati ule, sasa hivi
nimeshakuwa na mchumba’.
“Nilikuwa navaa vile kutokana na wakati ule ulivyokuwa. Kuna watu
walikuwa wanapenda, lakini sasa hivi nimeshakuwa mchumba wa mtu. Ni
kweli lazima nivae gauni, kwahiyo mtu unatakiwa ujibadilishe wewe
mwenyewe usisubiri kubadilishwa,” aliongezea.
Wolper aliendelea kusema, “hata hivyo bado sijaacha kabisa, kidogo unakuwa unagusia mashabiki zako wanakuwa wanakupenda.”
Hata hivyo Wolper japo amekiri kuwa na mchumba mpya kwa sasa lakini
hayupo tayari kuweka mahusiano yake hadharani kama mwanzo alivyokuwa
anafanya.

0 comments:
Post a Comment