Thursday, April 4, 2013

MAUNO YA WOLPER WOLPER YAWACHENGUA WATU UKUMBINI


VIUNO alivyokatika  staa maarufu wa filamu, Jacqueline Wolper viliwachengua ile mbaya watu waliohudhuria harusi ya wasanii maarufu wa Bongo Movies, Jimmy Mafufu na Idrissa Makupa ‘Kupa’.
 
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Ukumbi wa Urafiki uliopo Ubungo, jijini Dar baada ya  wasanii kwenda mbele ya ukumbi kwa zamu na kuonyesha uhodari wa kuyarudi mangoma ambapo ilipofika zamu ya Wolper, alionekana kuwazidi wenzake kwa utundu wa kucheza.
Baada ya kuonesha vitu adimu ambavyo havikuoneshwa na staa yeyote kati ya waliomtangulia, wageni waalikwa walishangilia na kupiga makofi hadi aliporejea sehemu aliyokaa awali.

 
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger