Mfanyabiashara
wa mazao, Eliusta Peter(40), amefariki dunia baada ya kuchomwa na
kitu chenye ncha kali shingoni akiwa katika nyumba ya kulala wageni
wilayani Kilombero.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea Aprili 22 baada ya wahudumu wa nyumba ya wageni ya Sayari kubaini maiti katika chumba namba mbili.
Inadawa
Aprili 20 mwanamke huyo akiwa na kijana mmoja ambaye jina lake
limehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi, walifika kwenye nyumba hiyo na
kuchukua chumba kimoja wakisema wao ni wafanyabiashara wa mazao.
“Mwili
wa marehemu uligundulika ukiwa kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo
Sayari chumba namba mbili saa 11 jioni na ulipochunguzwa ikagundulika
kuwa kifo kilisababishwa maumivu ya jereha,”alisema Matei.
Mwanamke huyo alikuwa na jeraha kushoto mwa bega lake lililotokana na kuchomwa na kitu chenye ncha kali
Matei alisema kwa taarifa walizozipata bila shaka kijana aliyekuwa naye anahusika na mauaji hayo.
Wakati
huo huo, jeshi la polisi wilayani Kilosa limemkamata Rogasian Jeremia
kwa tuhuma za kumshambulia mkewe, Faustina Sizayi(25) kwa kumkatataka
kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mtuhumiwa
alikamatwa akiwa anajihusisha na kazi ya ulinzi wa maduka baada ya
polisi kumsaka kwa muda mrefu na ndipo Aprili 24 alikamatwa baada ya
polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
0 comments:
Post a Comment