Binti anayedaiwa kubakwa
Afisa Tarafa mmoja mkoani hapa, ameingia matatani akituhumiwa kumbaka
mwanafunzi wa darasa la sita (jina linahifadhiwa) ndani ya ofisi yake
na kumsababishia maumivu makali.
Denti huyo mwenye umri wa miaka
12, alisema afisa tarafa huyo amembaka mara tatu kwa siku tofauti na
kwamba siku ya kwanza, alimuita ofisini kwake wakati akitoka shuleni.
“Asubuhi wakati tunaenda shuleni na wenzangu, tulipita jirani na
ofisi yake tukamkuta akiwa nje, akawa anatukonyeza, wenzangu wakasema
ndiyo kawaida yake,” alisema mwanafunzi huyo kwa uchungu na kuongeza
kuwa baada ya muda wa masomo kuisha, akiwa anarejea nyumbani kwao akiwa
peke yake, afisa tarafa huyo alimuita.
“Aliniuliza kama najua kucheza mchezo wa kibabababa, nikamjibu sijui,
akaniambia atanifundisha, akaniingiza ofisini kwake. Nilipofika ndani
alianza kuniambia ananifundisha mchezo wa kibabababa, akachukua koti
lake na kuniziba mdomo nikawa nakosa hata pumzi, akanivua nguo naye
akavua zake akanipakata na kuanza kunibaka
0 comments:
Post a Comment