Saturday, July 18, 2015

LINAH Aweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi

Linah akiwa na mpenzi wake Williams Bugeme

Akizungumza na Bongo5 leo, Linah amesema mwanaume aliye naye kwa sasa ni mwanaume aliyekuja kumuokoa akiwa katika wakati mgumu wa kimapenzi.

Kiukweli malengo yetu ni ndoa na wala haitachukua muda mrefu. Mungu akijalia mwakani,” amesema Linah. “Sasa hivi nataka ndoa mambo ya kuzini sitaki. Mimi sidhani kama ndoa ina ugumu wowote. Nataka sasa hivi kuwa wa halali kwa mtu mmoja na baadaye tupate watoto. Kwa jinsi tulivyoongea kazi ni kazi na mapenzi ni mapenzi, kwahiyo nafasi yangu ya kazi itakuwa pale pale. Na ninafikiri huyu ni mtu sahihi kwangu, ninafikiri ni mtu ambaye anaweza akawa mume wangu ndio maana nimekimbilia ndoa,” ameongeza.

Amekuja kwangu kama mtu anayenipenda, ameona jinsi ninavyoumia kimapenzi. Kwahiyo huyu amekuja kama mtu mwenye nia, ni aina ya mwanaume ambaye nilikuwa namtafuta kwa muda mrefu na hatimaye amefika, sasa hivi nafurahi.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger