Showing posts with label SKEND. Show all posts
Showing posts with label SKEND. Show all posts

Tuesday, December 3, 2013

"NI KWA WAPUMBAVU WANAOANDIKA UJINGA WANIKWAZE,KAMA HUNIPENDI U BETTER F**K OFF!" IRENE AFUNGUKA BAADA YA MASHABIKI WAKE KUMSHAMBULIA

 .
Hapo jana mwanadada Irene uwoya aligeuka mada ya mtandao mmoja maarufu wa kijamii baada ya kuweka picha ya mwigizaji wa marekani Vin Diesel ikiwa na maneno ya “R.I.P – Bwana ametoa na bwana ametwaa” kwa jamaa huyo kuwa amefariki kitu ambacho sio kweli na ndipo mashabiki walipoanza kumshambulia mwanadada huyo kuwa awe anafanya research na sio kupost vitu ambavyo havielewi il mradi amepost.


Chanzo nini?

Hivi majuzi wapenzi wa filamu walipata na msiba wa mwigizaji wa maarufu wa filamu ya fast and furious Paul Walker aliyefariki kwa ajali ya gari huko nchini marekani. Mwigizaji huyu alikuwa karibu sana na mwigizaji Vin Diesel ambaye aIrene uwoya aliweka picha yake kuwa amekufa na ndipo mashabiki walipomvaa kuwa aliyekufa ni Paul hivyo atumie google kufanya uchunguzi na sio kuandika mambo amabyo hayajui kama tunavyomnukuu shabiki mmoja akimchana live Irene
Clarah: JAMAN IMENBIDI NIPOST HII KITU COZ NLISHTUKA KWANZA LOH !! @ireanuwoyaonepiceintown (Jina analotumia irene kwenye mtandao huo wa kijamii)  HUYU KAKA ANAITWA VAN DIESEL NI ACTOR MKUBWA TU .HAJAFA JAMAN MAANA UMENISHTUSHA KUMPOST NA KUMWISH BWANA AMETOA NA BWANA KATWAA .JAMAN KUNA GOOGLE IMERAHISISHA MAMBO YOTE UNGEGOOGLE JINA LA PAUL WALKER SIDHAN KAMA UNGEKOSA.JAMAN TUWE MAKINI NA HIZI TAARIFA MAANA WENGNE TUNAPRESSURE.ILIBIDI NIANGALIE NEWS YOUTUBE KAMA KWELI HUYU KAFA NA KAFAJE KUMBE MWENZETU PICHA GONGANA !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!"""""""!!!!!!!!! @vandiesel MAY GOD GIVE U LONG YEARS TO LIVE MAANA KUNA MASNURA HUMU

Irene ajibu

Baada ya comment za mashabiki hao kuwa nyingi ndipo Irene alioamua kuitoa picha hiyo na baadaye kuwapa makavu wote waliomponda kwa kuandika ujumbe huu…
Irene uwoya: Hiii msg nikwawale wapumbavu wanao andika ujinga ili wanikwaze....maana kuna mijitu haijui nimeandika vile coz yule nimtu wake wakaribu na ninampenda ndomana nime post....ila ile mijitu isio na akili inavamia tuuu....kwanza kama unaona unipend na unikubali u better f#k off...sihitaji mijitu miswahili humu...nataka watu wenye upeo na adabu....nadhan mnajijua na mme nisoma....mi siogop mtuuu....nakama itakuuma kunywa sumu ufe

Mashabiki wagoma kumuelewa, wazidi kumpa makavu zaidi

ROGER: Kubali tu ulikosea mama yaishe.... maana mi naweza nikakuambia Irene R.I.P... kisa Kanumba Kafa... kuwa mtu wa Karibu haimaanishi ndo umwambie yeye arest in peace na kuweka picha yake kabisa

Levyl: Sasa kwann kaitoa c angeaacha kama yuko ryte

MrslucaS: Umebugi kubali tuu pyeee

Dorryjacob:  Swry hakuna anayekuchukia tatizo ulikosea na binadamu hukose..ww ulipost hyo pic ukijua ni paul kumbe ni vian so mbona rahic tu, ungesema umekose tatizo hutaki kushindwa kumbe kuna watu pia humu pamoja kwamba si masuper star bt nao ni vichwa hawakubali mbona ni simple like dat..na ndio maana umeitoa hyo pic maana na ww umejua umekose! Na pia anamafans zake wanaompenda so hawafurah ulivyomtabiria kifo..pole mummy kama umekwazika
Share:

Tuesday, May 14, 2013

KASHFA YA WABUNGE WA KIKE KUJICHUBUA YAIBUA MJADALA MZITO...!!

KUMBE! Baadhi ya wabunge wa kike ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanatumia vipodozi vinavyochubua ngozi ya juu ya mwili ili wawe na mwonekano mweupe (kama wazungu).
Kauli hiyo ya kushangaza ilitolewa bungni Mei 9, mwaka huu na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy wakati alipokuwa akichangia Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu udhibiti wa dawa kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
Akizungumza bila kupepesa macho, Mheshimiwa Kessy  alisema kuwa baadhi ya waheshimiwa wa kike ndani ya mjengo wanatumia vipodozi ambavyo vina madhara makubwa kwa afya ya mtumiaji.

Grace Kiwelu.
MSIKILIZE KWA KINA
“Labda niseme tu TFDA wanapaswa kusimamia kuhakikisha vipodozi vyenye madhara haviingii nchini, watu wengi sana wanaathirika na kupata magonjwa ya kansa ya ngozi.
“Humu ndani (bungeni) wapo waheshimiwa ambao wanatumia vipodozi hivyo ambapo wanapokuja kuumwa serikali inapoteza fedha nyingi kwenda kuwatibia nje ya nchi,” alisema Kessy.

WABUNGE WAMEKASIRIKA?
Habari za ndani zinaweka wazi kwamba, baada ya Mheshimiwa Kessy kuzungumza madai hayo, baadhi ya waheshimiwa hao wameonesha kukasirishwa na kauli hiyo wakisema ililenga kuwachafua.
“Kwa kweli waheshimiwa wangekuwa wanachuja cha kuzungumza, mambo mengine ukiyasikia unapata picha kwamba lengo la msemaji ni kuchafua watu,” aliweka wazi mbunge mmoja alipoongea na gazeti hili huku akigoma jina lake lisiandikwe gazetini.

ALICHOSEMA MTAALAM WA AFYA
Baada ya kauli hiyo ya Mheshimiwa Kessy ambayo ndiyo habari ya mjini kwa sasa, Ijumaa Wikienda lilizungumza na mtaalam wa masuala ya afya ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.
Alibainisha kuwa tatizo litokanalo na matumizi ya vipodozi vikali ni kubwa sana Bongo na kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele, taifa linazidi kuangamia kwa ugonjwa wa kansa ambayo husababishwa na kujichubua.
“Serikali kupita mamlaka zinazohusika inapaswa kutilia mkazo suala hili na kuhakikisha inathibiti mianya yote ya kuingizia madawa haya ambayo madhara yake ni makubwa kwa taifa, hasa magonjwa ya ngozi kama vile kansa.
“Hii ni hatari kubwa sana, kwa sababu wabunge ambao ndiyo walipaswa kuwa mfano wa kuigwa, badala yake wao wenyewe wanadaiwa kuwa watumiaji wazuri,” alisema mtaalam huyo.

WABUNGE WANENA
Baada ya mtaalam huyo kuweka wazi hali halisi ya madhara ya matumizi ya madaya hayo, Ijumaa Wikienda lilipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya waheshimiwa wabunge wanawake ambapo kila mmoja alifunguka kivyake:

 
ZARINA MADABIDA (Viti Maalum CCM)
“Mimi ni Pharmacia (mtayarishaji na mtoaji wa madawa), natambua vema madhara ya hivyo vipodozi. Sina uhakika kama kuna wabunge wanatumia lakini kama wapo basi nawashauri waache mara moja.
“Mimi situmii hata kidogo, si unaniona hata rangi yangu ni maji ya kunde ya asili?!”

GRACE KIWELU  (Viti Maalum- Chadema)
“Mbunge ni mtu mzima huwezi kumzuia. TFDA wanapaswa kufanya kazi yao ya udhibiti, kweli wanaofanya hivyo wapo lakini tunapaswa kuwapa elimu.
“Mimi situmii, kuanzia mikono hadi miguu yangu vinafanana. Hakuna ‘pepsi mirinda’ katika mwili wangu.”

SUZAN LYIMO  (Viti Maalum-Chadema)
“Wabunge wanapaswa wawe mfano, japo hii ni ishu personal (binafsi) lakini ni vema basi wakatazama madhara yake. Vipo vipodozi ambavyo havina madhara na vingine vina madhara.”

CHIKU ABWAO  (Viti Maalum-Chadema)
“Wabunge ni watu wazima, kujichubua ni ishu private (siri). Lakini na yeye Mheshimiwa Kessy kama ameona wabunge wana tatizo hilo anapaswa kuwashauri waache. Mimi natumia vipodozi lakini visivyo na madhara.”

CATHERINE MAGIGE (Viti Maalum-CCM)
“Ni mambo binafsi, kuhusu wanaotumia mimi sina comments (maoni) yoyote. Ningekuwa natumia mimi ungeniona vinavyoniathiri, sijawahi kutumia kabisa jamani.”

 
ESTER BULAYA (Viti Maalum-CCM)
“Kwanza sikuwepo bungeni siku hiyo mheshimiwa huyo alipotoa hoja yake. Halafu mimi ni mweusi, huwa sipendi kutumia vipodozi vya kuchubua ngozi ili niwe mweupe, napaka mafuta ya kawaida kabisa. Urembo wangu mkubwa mimi upo kwenye nywele.”

ANNA KILANGO  (Same Mashariki-CCM)
“Ha! Haa! Haaa! Mimi situmii jamani, rangi yangu mimi ni natural  (ya asili) hakuna mkorogo hata kidogo, sijui kama wapo wanaotumia.”

SARAH MSAFIRI (Viti Maalum-CCM)
“Hivyo vitu vinahitaji utaalam sana kabla ya kutumia, mimi situmii hivyo sina uzoefu wowote labda uwaulize wanaotumia.”

ZAINABU KAWAWA (Viti Maalum-CCM)
“Ni kauli ya kitawala, siwezi kutolea tamko lakini pia madhara ni ya kitaalam.”

 
MARY MWANJELWA (Viti Maalum-CCM)
“Baadhi ya waheshimiwa walikwazika lakini kiukweli vipodozi hivyo vina madhara makubwa. TFDA wanapaswa kutoa ufafanuzi juu ya hilo.”

DUKA LATAJWA
Baadhi ya waheshimiwa waliliambia gazeti hili kuwa, waheshimiwa wanaojichubua hutumia vipodozi vyenye ‘kaloraiti’ kutekeleza nia yao na kwamba duka lao kubwa kwa Dar es Salaam lipo Kariakoo kwa jamaa Mkongomani aitwaye Hashim.
Share:

MFANYABIASHARA WA MADINI ANAYEDAIWA KUMUUA ASKARI APANDISHWA KIZIMBANI...!!

MFANYABIASHARA wa madini ya tanzanite, Lawi Abayo (33) amefikishwa kwenye Mahakama ya Mkoa wa Manyara akikabiliwa na mashitaka ya kumuua kwa kumpiga risasi askari polisi wa kituo cha Mirerani wilayani Simanjiro G.7037 Joseph Tairo (28).
Abayo alifikishwa mahakamani mjini Babati na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Rashid Chaungu. Mfanyabiashara huyo anatetewa na wakili maarufu wa kujitegemea wa jijini Arusha Duncan Oola.
Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Mkaguzi wa Polisi, Mbaruku Makame aliieleza Mahakama kuwa Abayo alitenda kosa hilo Aprili 7, mwaka huu kwenye Mtaa wa Kazamoyo katika Mji mdogo wa Mirerani.
Alidai kuwa Abayo alimpiga risasi ya kichwa askari wa Kituo cha Polisi, Mirerani wilayani Simanjiro, Tairo mkazi wa Kijiji cha Kabolo Mkuu wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro ambaye alifariki dunia Aprili 15, mwaka huu.
Aliongeza kuwa siku ya tukio hilo, Abayo bila halali alimpiga risasi askari huyo wakati akiwa kazini akimpeleka kwenye Kituo cha Polisi mhalifu aliyefanya vurugu kwenye Baa ya Kazamoyo Resort iliyopo mji mdogo wa Mirerani.
Makame alidai pia kuwa baada ya Tairo kumkamata mhalifu huyo, Abayo alikuja na gari aina ya Prado lenye namba za usajili T 671 ATK na kutoa bastola kisha kumpiga risasi ya kichwa na kuondoka na gari hilo akiwa na mhalifu huyo.
Mshtakiwa huyo Abayo hakutakiwa kujibu lolote mahakamani hapo kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kisheria wa kusikiliza kesi hiyo na Hakimu Chaungu aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 22, mwaka huu itakapotajwa tena.
Share:

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger