MKURUGENZI wa Bendi ya Double M Plus, Muumini Mwinjuma, amesema
atachukua hatua za kisheria dhidi ya mwanamuziki mwenzake wa bendi
hiyo, Salehe Kupaza, aliyedai alimtwanga makonde.
Sakata hilo lilitokea Jumamosi mara baada ya bendi hiyo kumaliza
kutoa burudani katika ukumbi wa Star Point, uliopo Kigogo ambapo Muumini
alikataa kumpa posho mwimbaji wa kike, Amina kutokana na
kutokufanya kazi siku hiyo.
“Amina amekuwa na tabia ya kuchagua nyimbo za kuimba na wakati
mwingine hapandi kabisa jukwaani sasa juzi (Jumamosi) sikumpa posho kwa
kuwa hakufanyakazi na Jumapili nilimuita kwenye kikao nijue kama anataka
kuendelea na bendi au la, mara akaja Kupaza akaniambie nimpe Amina
posho nikamtaka atuache kwa kuwa hajui makubaliano yetu.
“Wakati nilipotoka nje nikashangaa nimepigwa ngumi ya usoni na
Kupaza, nikadondoka kama nilielekea kupoteza fahamu ndio watu
wakanisaidia, nikaenda kuripoti kituo cha polisi cha Urafiki nikapewa
PF3 nikatibiwa Palestina, bado nina maumivu kwenye jicho, Kupaza
kanidhalilisha mbele ya mashabiki,” alisema.
Alisema kwa udhalilishaji huo hatokaa kimya, atahakikisha hatua za
kisheria zinachukuliwa huku akidai kwamba hataweza kufanyakazi naye
tena.
0 comments:
Post a Comment