Wednesday, March 13, 2013

"NAAPA KUILINDA NA KUITUNZA NDOA YANGU"...AUNT EZEKIEL

DIVA wa tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema atahakikisha anaitunza ndoa yake kwa kila namna maana hakuolewa ili aonekane amevaa shela tu, Risasi Mchanganyiko linakuhabarisha.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Aunt alisema ndoa yake ina thamani kubwa na anatambua ndiyo maana yupo makini kuilinda ili isivunjike kwa namna yoyote.
“Mimi natambua thamani ya ndoa na namna ambavyo mwanamke anatakiwa kufanya kwa mume wake. Mimi siyo aina ya wale wanaotamani kuvaa shela tu. Siyo mimi kabisa,” alisema Aunt.

Hata hivyo alipotakiwa kuwataja baadhi ya mastaa ambao wameolewa kwa lengo la kuvaa shela na si ndoa alikataa, akasema: “Wanajulikana vizuri sana. Hata hivyo sipo kwa ajili ya kuwazungumzia watu wengine.
“Ninachosema mimi kama Aunt nitailinda ndoa yangu kwa nguvu zangu zote ili nisiabike. Unajua kila kitu kinafanyika kwa mapenzi. Ninajiamini nilimpenda mume wangu kabla na bado nampenda na nitampenda milele, hivyo lazima niwe mbunifu ili niwe wake wa milele.”
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger