Thursday, May 2, 2013

"MBWA WANGU NI ZAIDI YA MUME KWANGU"....WEMA...!!

BEAUTIFUL Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa faraja kubwa kama mbwa wake, Ivan na Gucci.

Wema Sepetu ‘Madam’ akiwa na mmojawapo wa mbwa wake.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Wema alisema hawezi kukaa zaidi ya siku tatu bila kuwaona mbwa wake hao kwani amewazoea kwa kuwa humuondolea ‘stress’ za hapa na pale.
“Juzikati nilikwenda Arusha mara moja tu siku hiyohiyo nikawa nawakumbuka Ivan na Gucci mpaka nikawa natamani kurudi kwa ajili yao, kusema kweli hawa ndiyo kila kitu kwangu,” alisema Wema na kuongeza:
“Nimewazoea lakini wao pia ndiyo zaidi, hawataki kubanduka pindi ninaporudi kutoka katika kazi zangu, mtu akiwachukua tu umewakorofisha,” alisema Wema.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger