Monday, February 4, 2013
"MTU YEYOTE ATAKAYEMFANYIA SHEREHE LULU, AMA ZAKE AMA ZANGU"...MUNA WA BONGO MOVIE
STAA wa filamu za Kibongo, Muna (pichani) amefunguka kuwa akiona mtu anajitokeza kumfanyia sherehe msanii, Elizabeth Michael ‘Lulu’ atapambana naye na ikiwezekana atapelekwa yeye Segerea.
Muna ambaye alitoa sapoti kubwa kufanikisha dhamana ya Lulu anayekabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, alifunguka hayo baada ya kusikia kuna baadhi ya wasanii wamejipanga kumfanyia sherehe msanii huyo.
“Wee! Ole wake nione mtu anajitokeza kumfanyia sherehe, ama zake ama zangu. Wakati alipokuwa Segerea wengi wao walikuwa hawaendi hata kumuona, sasa hivi wanamtafutia nini? Kwa hili, watanipeleka mimi Segerea,” alisema Muna.
Weka Maoni yako Hapa
0 comments:
Post a Comment