Friday, June 10, 2016

Picha: Raymond wa ‘WCB’ Aringishia Mabunda ya Hela Instagram

Wakati mtaani raia wakilalamika kuhusu ukata wa hela toka Rais Magufuli aingie madarakani, mkali wa wimbo ‘Kwetu’ kutoka WCB, Raymond ‘Rayvanny’ ameamua kuringisha mabunda ya hela kupitia ukurasa wake wa instagram.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Natafuta kiki’ amepost picha kupitia instagram yake na kuandika jina la wimbo wake huo, huku mashabiki wakitoa maoni yao juu ya wingi pesa hizo.

Raymond alisaini ‘WCB’ mapema mwaka huu kabla ya hapo alikuwa anafanya kazi Tip Top Connection huku akiwa karibu zaidi na Madee.

Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki hao.

Tajibetese
Mmmmh @rayvannyy kama unatupenda fans wako hii ndo number yangu 0768046197 hata alfu kumi tuisogeze ramadhan

Blackgal_ake_dede
Hiyo kiki ndio yenyewe sio ya mademu fanya kunigawia basi ndugu @rayvanny

Am_coco_
That’s why I love you 😁,… Harmo abaki tu kwa mchaga, mi mpare nakutaka wewe .

Celinn1988
Watu wanavyojua kupangia watu kweny hela zao, mtadhani zenu mmefanyia kitu cha maana au mnaropoka tuu hapa.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger