Msanii wa muziki, Gigy Money anatarajia kuachia video yake
mpya ya wimbo ‘Tikisa Supu’, ambapo amewataadharisha watoto kukaa mbali
na kazi hiyo.
Muimbaji
huyo ambaye pia ni video queen, amesema kuwa ameamua
kuachia wimbo ‘Tikisa Supu’ baada ya kuona tayari kuna watu wengi
ameshaimba nyimbo za kutikisa sehemu za miili yao.
“Unaniuliza kucheza, nitikise nini? maana watu wameshatikisa kiuno, mapaja, nitikise matiti? no, hawataki. Nitikise Supu, wanataka. Kwa hiyo kwa lugha za kwenye runinga nikisema nitikise makalio haitaleta picha nzuri, na nyimbo naihisi itapendwa sana,” alisema Gigy.
Video ya wimbo ‘Tikisa Supu’ utatoka katikati ya mwezi huu baada ya kukamilika kwa matayarisho ya mwisho.
0 comments:
Post a Comment