SERIKALI kupitia Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu) imetenga zaidi ya Sh. 15 Bilioni katika
bajeti yake ya 2016/17 kwa ajili ya kuwaongezea vijana ujuzi
unaohitajika kwenye soko la ajira.
Jenista Muhagama, waziri wa wizara hiyo amesema hayo leo wakati wa mahojiano maalum na MwanaHalisi Online.
Amesema, kutokana na tatizo la ajira nchini, wameamua kutenga fedha
hizo ili kuwawezesha vijana kupata mafunzo katika maeneo mbalimbali ili
waweze kuzalisha.
Amesema, wamegundua nguvu kazi ambayo iliyopo haiendani na soko la
ajira na kwamba, miongoni mwa sekta zinazoongoza katika kuinua uchumi ni
kilimo, miundombinu, viwanda, hoteli, mafuta na gesi.
“Kwa hiyo sisi lazima tuwatayarishe vijana wetu wa Tanzania, ni ngazi
ngapi za ajira zitatakiwa? wakihitajika mafundi wa kuchomea mabomba ni
lazima vijana wetu wakapate ajira,” amesema Muhagama na kuongeza;
“Tuna program maalum kabisa ya kuwachukua vijana wetu kwa mujibu wa sheria lakini kwa kujitolea kwenda jeshini (JKT) na wanapokwenda kule wengi wanachukuliwa na taasisi zetu za ulinzi na usalama.”
0 comments:
Post a Comment