Master J na Shaa wamekuwa kwenye uhusiano kwa miaka mingi sasa na wameendelea kuwa imara.
Lakini pamoja na kuwa hivyo, bado uhusiano wao wa kikazi una nafasi
kubwa zaidi. Hali hiyo ndiyo imemfanya Shaa kujitahidi kutofautisha
uhusiano wao na kazi kwakuwa kwake Master J ni bosi wake.
“Bosi wangu meaning ni CEO wa MJ Records, label iliyonisaini na
ananisupport sana namshukuru mwenyezi Mungu, ni CEO lakini ni one of my
best friends, nimemfahamu sasa for ten years,” Shaa alikiambia kipindi
cha Chill na Sky.
“He is one of my close advisors, ananishauri sana na nasikiliza sana
ushauri wake, akikataa kitu nazingatia, akiniambia fanya hivi
nasikiliza. Kwahiyo kama Shaa, Master ni my CEO, my boss and my very
close friend, kama Sarah hayo ni ya Sarah.”
Master J na Shaa walikutana kwa mara ya kwanza kwenye mradi wa Cocacola Popstars takriban miaka 10 iliyopita.
0 comments:
Post a Comment