Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza kuwa hakuna afisa wa taasisi
na mashirika ya umma atakayelipwa mshahara wa zaidi ya shilingi za
Tanzania 15 milioni, ambazo ni sawa na dola 6,900 za Marekani.
Akiongea katika uwanja wa Mazaina, mjini Chato, kiongozi huyo alisema agizo hilo litatekelezwa katika mwaka ujao wa kifedha.
Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, Dkt Magufuli alisema si haki kwa
Tanzania kuwa na watu katika mashirika ya umma wanaolipwa mishahara ya
zaidi ya shilingi za Tanzania 40 milioni wakati wafanyakazi wa ngazi za
chini wanalipwa Sh300,000 kila mwezi.
Ilikuwa mara ya kwanza kwa Dkt Magufuli kufanya ziara rasmi mji huo wa nyumbani tangu kuchaguliwa kuwa rais Oktoba mwaka jana.
Alisema mishahara hiyo minono itafyekwa na watu wanaolipwa mishahara ya chini kuongezewa.
0 comments:
Post a Comment