Wanasayansi kutoka nchini Brazil wanaoendelea kuchunguza ugonjwa wa Zika
unaonekana kuwa ni hatari zaidi tofauti na mwanzo walivyofikiria
Ugonjwa huo unasababishwa na virusi vya Zika ambavyo vinasababisha kuzaliwa kwa watoto wakiwa na vichwa vidogo.
Wakiongea na BBC, madaktari hao bingwa wamesema kuwa virusi vya Zika
vinaweza kuwa sababu ya kutokea kwa matatizo ya neva za fahamu kwa
mwanamke mmoja mjamzito kati ya watano wanaoathiriwa na Virusi hivyo.
Mwanzoni maafisa kutoka CDC waliripoti kuwa virusi vya Zika huenezwa
na mbu lakini njia nyingine ambayo unaweza kuambukizwa ni kufanya
mapenzi. Watafiti wa ugonjwa huo sasa wameanza kukukubali kuwa kuna
uhusiano kati ya mbu anayeeneza virusi na tatizo la watoto kuzaliwa na
dosari kwenye ubongo.
Madaktari nchini Brazil wameiambia BBC kuwa asilimia ishirini ya
mimba zilizoathiriwa na ZIKA zitasababisha aina nyingine ya kuharibiwa
kwa ubongo wa mtoto akiwa tumboni.
Watafiti hao wamesema kuwa asilimia moja ya wanawake walioathiriwa na
virusi vya Zika wakati wa ujauzito kuelezwa kuwa watapata watoto wenye
vichwa vidogo.
Bado watafiti wanaendelea kutafuta chanjo ambayo itasaidia kupunguza
kasi ya ugonjwa huo ambao umeenea zaidi bara la Amerika Kusini.
0 comments:
Post a Comment