Ni mara ngapi umeenda kwenye ofisi fulani hapa nchini na ukakuta asilimia 50 ya wafanyakazi ni raia wa kigeni?
Na kinachosikitisha zaidi ni kuwa mara nyingi wageni ndiyo wenye vyeo
vya juu na hulipwa mishahara mikubwa. Hilo linaelekea
mwisho kwasababu Rais Dkt John Pombe Magufuli ameziagiza wizara zote
kuhakikisha kuwa zinapunguza ajira kwa raia wa kigeni na kuwapa nafasi
zaidi wazawa.
Akiongea kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, May Mosi,
Magufuli alidai kuwa kuna maeneo mengi ambayo yameajiri raia wa kigeni
wakati ni kazi zinazoweza kufanywa na wazawa.
Alidai kuwa kama tatizo ni lugha iweje wachina wanafanya kazi nchini
bila kujua lugha nyingine zaidi ya kwao na kwamba hata watanzania
wasiojua Kiingereza wana haki ya kupewa ajira na wakawasiliana kwa lugha
yao.
Katika hatua nyingine Magufuli aliagiza kupunguzwa kwa kodi ya
mshahara (PAYE) kutoka asilimia 11 hadi 9 kuanzia kwenye bajeti ya mwaka
2016/2017.
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kitaifa yalifanyika Dodoma.
0 comments:
Post a Comment