Godfrey Magila ni mtaalamu wa Teknolojia kwenye upande wa mitandao na ndio aliyetengeneza App ya Tigo Back-Up, amekaa kwenye Interview na Millard Ayo
na kueleza urahisi wa kukamatwa kwa yeyote anaefanya kosa la
kimtandao ikiwa tayari sheria ya makosa ya kimtandao imeshaanza kufanya
kazi Tanzania.
Tayari watu kadhaa wameshafikishwa
Mahakamani Tanzania akiwemo aliyemtukana Rais Magufuli, aliyeandika
habari za uongo za mkuu wa majeshi kulishwa sumu.…Wengi wanaamini sio
rahisi kukamatwa hata ukitumia jina ambalo sio lako kwenye mtandao ila
Magila anasema ni rahisi sana.
Anasema
Anasema
Kila mtu aliyejiunga kwenye mtandao kuna kama unaacha alama ya unyayo kwahiyo hilo watu wanalichukulia kirahisi lakini lina umuhimu wake na ndio linafanya ijulikane muda, sehemu na taarifa nyingine kuhusu wewe pale unapotafutwa, unyayo unaonyesha mpaka aina ya simu‘
Kubadilisha jina na kumtukana mtu kwenye mtandao itasaidia usikamatwe?
‘Kuna baadhi ya vitu hata ukibadilisha jina haisaidii mfano mitandao mingi ukijiunga au email unaambiwa uingize namba ya simu kwa ajili ya uthibitisho, utatumiwa msg kwenye simu ili uthibitishe…. tayari namba yako uliyoiweka ina taarifa zako nyingi na hiyo ni moja tu ya njia nyingi zinazoweza kufanya ukamatwe’
0 comments:
Post a Comment