Monday, May 2, 2016

Kesi ya Mdee, Kubenea yapigwa kalenda

KESI ya shambulio inayowakabili Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo na Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga imeahirishwa leo katika Mahakama ya Kisutu kutokana na upande wa mashtaka kutokamilisha upelelezi. 
 
Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Shafii Juma, mfuasi wa Chadema; Manase Mjema, Diwani wa Kimanga pamoja na Alfonce Kinyafu, Diwani wa Kimara Saranga ambao kwa pamoja wanadaiwa kumshambulia Theresia Mmbando, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa harakati za Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
 
Helleni Liwa, Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ameahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 2 Juni mwaka huu.
 
Mdee, Waitara, Shafii na Kinyafu walifikishwa mahakamani hapo tarehe 2 Machi mwaka huu ambapo Kubenea na Mjema walifikiswa 11 Machi.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger