Tuesday, May 3, 2016

Kesi ya Kitilya na Wenzake Yaangukia Mahakama Kuu

April 29 2016 Kesi ya Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare  iliahirishwa.

Sababu zilizotajwa kuahirishwa kwa kesi hiyo ilikuwa ni jalada halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu baada ya kukatwa kwa rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.

Kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa leo May 3 2016 Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ambapo Jalada la kesi hiyo lilitegemewa kurudi leo lakini halijarudi hivyo kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 18 2016 watuhumiwa wamerudishwa rumande.

Aidha watuhumiwa walitakiwa kufika mahakama Kuu kwa ajili ya kuendelea na rufani ambapo baada ya kufika Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kuanza kusikiliza rufani hiyo May 5 2016.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger