Wanachama wa chama tawala cha Uturuki cha AK na chama kinachoungwa mkono
na Wakurdi wamepigana ngumi bungeni kuhusiana na mpango wa kuwaondolea kinga
wabunge ya kutoshitakiwa.
Wabunge wakionyeshana umwamba Bungeni nchini Uturuki,
Ngumi hizo ziliibuka bungeni wakati kamati ya bunge ilipokutana kujadili
mabadiliko hayo yanayoungwa mkono na serikali ili kubadili Katiba
kuwaondolea kinga hiyo wabunge.
Baadhi ya wabunge walikunjana mashati kwenye meza, wengine wakirusha chupa za maji na kurushiana ngumi bungeni.

0 comments:
Post a Comment