Maswali yalikua ni mengi na mashabiki
walitaka kufahamu kwanini mwigizaji Lulu kutoka kwenye kiwanda cha
filamu Tanzania hakumpost kwenye Instagram kama ishara ya kuonyesha
ulimwengu kwamba anamkumbuka Marehemu Steven Kanumba na vilevile hakuhudhuria kwenye kaburi la Kanumba kama walivyofanya wengine.
Siku hiyo ya kutimia kwa miaka minne ya kifo cha Kanumba (Kanumba Day), Waigizaji mbalimbali wa movie Tanzania pamoja na watu wengine kama Mama Kanumba pamoja na Mama Lulu walikwenda kaburini lakini Lulu hakuonekana.
Kuhusu kutokuonekana kwake Lulu kwenye Exclusive na millardayo ameongea kama ifuatavyo
‘Kiukweli
sikuwahi kutaka kuongelea chochote kuhusu hiki kitu kwasababu
ninachoamini mimi nina maumivu kuliko mtu yeyote anaedhani nina maumivu,
ile siku ni maalum kwa taifa au kwa watu wengine lakini kwangu Kanumba
Day ni kila siku‘
‘Kama watu walikwenda siku ile
mimi naweza nikaenda leo, nikaenda kesho… tatizo watu wengi wako-fake
wanataka kuonekana wamefanya, mimi naweza kufanya kitu na mtu yeyote
asijue nimefanya, sidhani kama kumuenzi mtu vinatakiwa kuanza
kutangazwa… hii sio biashara kama natafuta Wateja, najua kiimani kidini
unatakiwa kufanya vitu gani kumuenzi mtu.. hivyo ndivyo ninavyofanya
mimi‘ – Lulu
KUHUSU MAMA KANUMBA:
‘Kuhusu
Mama Kanumba sitotaka kuzungumzia chochote kuhusu yeye kwa sababu
naamini kama iko siku itanilazimu kuongea sanaa nitaongea’
0 comments:
Post a Comment