Friday, April 29, 2016

TID Afunguka 'Nilikuwa Natoka na Wema Sepetu Akanimwaga...Sasa Hivi Akitaka Kurudi Hakuna Nafasi Tena'

Akiwa Katika Kipindi cha Clouds 360 leo,Mwanamuziki TID Amefunguka Kuhusu Kutoka na Wema Sepetu...
"Nilikuwa "namdate" Wema Sepetu akaniambia Sikutaakiiii....tangu kipindi hicho nimekuwa na Wasichana wengi...Ikitokea Wema Sepetu anataka kurudi hakuna nafasi Tena "I'm occupied".

TID amesema katika kipindi hicho aliumizwa sana na jinsi magazeti yalivyokuwa yanamuandika vibaya.

“Wakati huo mitandao ya kijamii haikuwepo lakini wamagazeti walizichukua picha na kufanya yao, it was bad. Mimi nikasema sawa lakini niliumia sana,” alisema TID.

Pia TID Amemuongelea Mwanamuziki Ommy Dimpoz na kusema kuwa yeye ndio aliyemtoa

 "Alikuja studio kwangu akiwa anavaa ndala na kupitia kwangu alijuana na watu muhimu kama Ali Kiba na Ruge Mutahaba". Anasema pia yeye anapenda na ni bora afanye video zake hapahapa Tanzania ili kuitangaza nchi yetu na vivutio vyake zaidi. 

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Confidence’ aliyomshirikisha Joh Makini pamoja na Dully Sykes.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger