Mwasiti ameiambia Bongo5 kuwa Sisters ina wasichana/wanawake sita wakiwemo yeye, Shilole, Queen Darleen, Linah, Kajala.
Amedai kuwa mara nyingi huwa pamoja na wanafahamiana ndani na nje na hivyo waliona ni vyema urafiki huo ukazalisha kitu cha msingi kitakachowasaidia wasichana wengine.
Kwa upande wake Shilole amesema anapenda kutumia kampeni hiyo
kuelezea historia yake na jinsi ambavyo maisha yake yaliharibika akiwa
binti baada ya kudanganywa na wanaume.
“Kwahiyo ndio tukasema tuseme na wale mabinti ambao ndio kwanza
watakuja kuwa wanawake wa baadaye, tuwaambie kwamba sisi dada zenu ambao
tulikimbilia hayo maisha ya juu yametuponza kiasi gani, wa kwanza mimi
hebu tujifunze kupitia Shilole,” amesema.
Kwa sasa Sisters wanapita kwenye shule za Dar es Salaam kuzungumza na
wanafunzi wa kike na kuwashauri jinsi ya kujikita kwenye elimu kuandaa
mustakabali unaofaa.
Mwasiti amesema wanatarajia kwenda katika shule sita katika kila mkoa
nchini. Amesema Sisters Movement ina watu wengine ambao ni wataalam wa
masuala mbalimbali ya kijamii kama wanasaikolojia, madaktari, wanasiasa
na wengine ambao huzungumza na wanafunzi.
Kwa upande wake Queen Darleem amesema wanataka kutumia kampeni hiyo
kuwapa wasichana wa leo kile walichokikosa wao wakati wakiwa mabinti
kiasi cha kujikuta wakiingia kwenye maisha makubwa kabla ya wakati.
“Mwisho wa siku sisi ndiyo inabidi tuanze kuongea nao, ambao tayari
yameshatukuta, wazazi wetu hawakupata nafasi ya kuongea na sisi,”
anasema Darleen. “Tumekuja kupata tatizo ndiyo wamekaa chini kuongea na
sisi. Kwahiyo sasa hivi sisi tunajaribu kuongea na hao wanafunzi wajue
kwamba kitu gani kibaya,” ameongeza.
0 comments:
Post a Comment