Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli (pichani) akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana.
Akitoa hotuba yake katika mji wa Kibaigwa Dk. John Pombe Magufuli
alisema hakuna kitu kinachomuumiza kama mauaji ya wakulima na wafugaji
yanayotokea kati ya wilaya za Kongwa Mkoani Dodoma na Kiteto mkoani
Manyara.
Dkt Magufuli aliahidi kuwa mara baada ya kuchaguliwa na kuunda Serikali yake, jambo hilo atalipa uzito wa juu na kulifanyia kazi kwa umakini mkubwa.
“Yaani mimi Magufuli nimteuwe Waziri na watendaji wengine wa serikali halafu mauaji yatokee watu wafe, Mkuu wa mkoa yupo, Mkuu wa wilaya yupo na Kamanda wa Polisi yupo wabaki wanapunga upepo... wamiliki wa ng’ombe wabaki wanakula maisha... haiwezekani! Nitalala nao mbele na ng’ombe wataliwa msibani kwa uzembe waliousababisha” alisema Magufuli kwa msisitizo mkubwa.

Magufuli amewataka wafugaji na wakulima kuishi kwa amani bila kubaguana, lakini pia akasema atatumia sheria za ardhi na kuhakikisha maeneo ya wafugaji na wakulima yanatengwa, ili wafanye shughuli zao na kukuza kipato na uchumi wao bila kusumbuliwa.

0 comments:
Post a Comment