Monday, May 13, 2013

UPDATE: MAHAKAMA YAMPIGA 'STOP' JAYDEE KUIKASHIFU CLOUDS FM...!!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee(Pichani) muda si mrefu amepokea hati yake ya mashtaka kutoka katika mahakama ya Kinondoni ambapo ameshtakiwa na Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds FM baada ya kuwa na kutofautiana kwa muda.

Jaydee ambaye alikuwa Baraza la Sanaa ambapo alikuwa akiongea katika jukwaa la wasanii, alipata ujumbe wa kuitwa mahakamani na alipofika alikabidhiwa hati hiyo ambayo mwenyewe alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na kusema kwamba anataka kwanza awasiliane na mwanasheria wake.

Kikubwa ambacho aliweza kusema kwa waandishi waliokuwa wameongozana naye ni kwamba, kesi itaanza kuunguruma tar 27 mahakamani hapo
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger