Friday, March 1, 2013

"SIJAPEWA TALAKA NA MUME WANGU.....WAMBEYA ACHENI MAJUNGU"...SANDRA WA BONGO MUVI AFUNGUKA


SANDRA

Mwigizaji wa kike asiye na skendo nyingi kutoka kiwanda cha Bongomovie maarufu kwa jina Salma salmin a.k.a 'Sandra' ambaye kwa siku kadhaa zilizopita kulizagaa uvumi kuwa amepigwa talaka tatu na mumewe na hivyo kusababisha kutengana kwao, Jioni hii mrembo huyo kupitia kituo cha luninga cha Channel 5 afunguka na kulizungumzia swala hilo ambalo ni binafsia kwake.

Akizungumza kwenye kipindi cha Hot Mix 'Sandra' alisema yeye hakupewa talaka kama inavyosemekana kwenye jamii na wala hajaachana na mumewe mpendwa ambaye amemwagia sifa ya kuwa anampenda kwa dhati, Alisema hakuna marumbano kwenye ndoa yao hiyo ila ni hila za wachache wasiopenda kuona maendeleo yake na mumewe.!!
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger