Prezzo anaonekana akiwa amevaa nguo nyeusi zote, hii ilikua ni ibada ya kumuombea Goldie ambayo ilifanyika siku kadhaa kabla ya Prezzo kuondoka Nigeria kurudi Kenya.
Ni watu wengi wanajiuliza imekuaje CMB Prezzo hajaonekana kwenye msiba wa mpenzi wake ambae walikua na plans za kuoana, Mnigeria Goldie aliefariki muda mfupi tu baada ya kufika Nigeria akitokea Marekani.
Kwa sababu nimeamua kumuacha Prezzo apumzike kwa sasa, ili kujua angalau hata kwa muhtasari niliamua kumtafuta Arthur Samwel ambae ni Dj wake na msimamizi wa kazi nyingi anazofanya Prezzo.
Alichosema Arthur kuhusu Prezzo kutomzika Goldie ni hiki “Prezzo alirudi Nairobi wiki iliyopita, ilikua ni weekend na mpaka anatoka Lagos alikua hajui ni siku gani Goldie atazikwa kwa sababu Wanigeria wanatabia ya kuchelewa kuzika, sasa mtu kama uko ugenini huwezi kukaa muda wote……..
kwa bahati mbaya Prezzo akiwa amesharudi Nairobi alipigiwa simu kwamba Goldie ameshazikwa hivyo ikawa ni ngumu kurudi tena Lagos, sasa hivi yuko Eldoret Kenya kwenye ishu za kampeni”
0 comments:
Post a Comment