
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini
Arusha, Dk Magufuli alisema kama watendaji wa shirika hilo wanamuhujumu
kwa kumzimia umeme, wajiandae kutoka kwenye viti vyao akiingia ofisini
kwani bado siku 18 tu za kuingia Ikulu.
Dk
Magufuli, ambaye amekuwa akisisitiza kwenye mikutano yake kuwa
hatavumilia watendaji wazembe, alisema mawaziri wa Wizara ya Nishati na
Madini na watendaji wajiandae kuachia nafasi zao kwani hataweza
kuwavumilia.
Alisema tatizo la umeme, ambalo linaonekana kuwa sugu, limekosa majibu ya uhakika.
“Ninajua mawaziri wapo kwenye kampeni, lakini nao wajiandae zimebaki siku 18 tu,” alisema Dk Magufuli.
Awali
Tanesco ilisema kuwa tatizo la sasa la umeme lingedumu kwa wiki moja
kwa kuwa ilikuwa ikishughulikia kuunganisha mitambo ya kufulia umeme na
mabomba ya gesi asilia, lakini mapema wiki hii imeeleza kuwa kazi hiyo
inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kutokana na gesi hiyo kuwa na uchafu
uliotokana na uwekaji mabomba, msukumo kuwa mdogo na kusubiri matokeo ya
vipimo vilivyopelekwa nje ya nchi.
Hali kadhalika, uwezekano wa kutumia umeme unaofuliwa kwa kutumia maji, haupo kwa sasa kutokana na mabwawa kukauka.
Awali,
katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema ni jambo ambalo
haliwezekani kwa tatizo la umeme kushindwa kupatiwa ufumbuzi kwa muda
mrefu.
“Hatutaki majibu mapesi kwenye maswali magumu,” alisema Kinana. “Kama wanabadilisha mitambo sasa kutumia gesi, kwanini hawakujiandaa?”
Kinana
alisema viongozi ambao wamekuwa wakitoa majibu kuhusu sakata la umeme
ni wale ambao wanaishi nyumba zenye mashine za jenereta, hivyo hawajui
adha za wananchi.
“Kuna wananchi kazi zao ni vinyozi, sasa wanapokosa umeme ujue unawaathiri sana,” alisema.
Tazama Video
0 comments:
Post a Comment