Sunday, October 28, 2012
Picha: Angalia UVCCM wakipokeana kwa kuchapana makonde DAR!!
“ Habari tulizozipata hivi punde ni kwamba wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM, wamechapana makonde wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti mpya wa umoja huo.
Tafrani hiyo imetokea leo katika Makao Makuu ya UVCCM, ambapo moja ya makundi ambayo hayakubaliani na ushindi wa Mwenyekiti huyo mpya walikwenda na mabango yanayompinga.
Ndipo kasheshe ikaanza kwa kupigana. Pia indaiwa kuwa mapokezi hao yalidorora kwa vile asilimia kubwa ya viongozi waliomaliza muda hawakujitokeza kumpokea kiongozi huyo mpya. ”
GUMZO LA JIJI BLOG ITAENDELEA KUTAFUTA CHANZO CHA MKASA HUO NA KUKUJULISHA MDAU, ENDELEA KUWA NASI!!!
Weka Maoni yako Hapa
0 comments:
Post a Comment