Showing posts with label SHILOLE. Show all posts
Showing posts with label SHILOLE. Show all posts

Thursday, May 19, 2016

Shilole: Wanaume Suruali Wasio na Pesa Sasa Basi

MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka kuwa kuanzia sasa hataki tena kuwa na mwanaume suruali, bali anahitaji mtu mwenye nazo, ndiyo maana ameamua kufanya kazi kwa bidii.

Akilonga na Risasi Vibes, Shilole alisema kuwa kwa sasa ameamua kukaa singo kwa sababu ameona hakuna faida ya kuwa na mwanaume asiye na kitu.


Kuhusu Nedy Music anayedaiwa kuwa naye mara tu baada ya kumwagana na Nuh Mziwanda, Shishi Baby alisema hana uhusiano naye wa kimapenzi, isipokuwa ni rafiki wa kawaida tu!
Share:

Thursday, May 12, 2016

Shilole: Najua Kuongea Vizuri Kiingereza ila Napenda Kuongea Kingereza Kibovu ili Kuchekesha Watu

Msanii wa Bongo fleva Shilole a.k.a Shishi Baby amekiri kwamba kuzungumza lugha ya kingereza ni kipaji na wala si hivi hivi tu na amesema yeye anajua kuongea vizuri kingereza ila anapenda kuongea kingereza kibovu ili kuchekesha watu tu.

Na hii ni baada yakuonekana katika mitandaoni mbalimbali ya kijamii akijaribu kwa juhudi zote bila mafanikio kuzungumza lugha hiyo huku ikibaki kuwa kama burudani kwa watu wengine.

“Si munaonaga wenyewe muda mwingine nisipoongea kiswangilishi changu watu wanaanza kunitafuta shishi plizi ongea bhana tunataka uongee”,alisema Shilole.

eatv.tv

Share:

Tuesday, May 3, 2016

SHILOLE Afunguka:'Mimi ndio Mwanamke Mzuri Sana Bongofleva'

Msanii Shilole ambaye haishi vituko kwa mashabiki wake amejigamba kuwa kwa Bongo hakuna msanii mzuri kama yeye, kwani ana uzuri wa asili bila vipodozi.

Shilole ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na EATV.

"Mimi ni mwanamke mzuri without make up (bila vipodozi), unaweza ukaniamsha usingizini na nikaenda popote bila makeup, katika Bongofleva mimi ni mwanamke mzuri sana hamna anayebisha,” alisema Shilole.

Pamoja na hayo Shilole amezungumzia suala la kuwa na ukaribu na msanii Nedy Music, na kusema kuwa msanii huyo ni rafiki yake tu na si vinginevyo. “Nedy ni mshkaji wangu tu, ananifanya nismile,” alisema Shilole.
 
Pia Shilole amesema Jumatatu ya wiki ijayo anatarajia kuachia wimbo wake mpya unaoitwa 'Say ma Name'.
Share:

Tuesday, June 9, 2015

Shilole awatolea uvivu wanaojipitisha kwa mpenzi wake


Mwanamuziki nchini Tanzania, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amewatolea uvivu wanawake wanaomshobokea mpenzi wake kwa kuwapa mkwara mzito endapo wataendelea na tabia hiyo kwani hawajui wametoka wapi.
 
Hatua hiyo imefikiwa baada ya mwanamke mmoja kujitokeza katika vyombo vya habari na kudai kuwa ana ujauzito wa Nuh Mziwanda, jambo ambalo Mziwanda, alilikanusha na kudai hana mwanamke wa nje zaidi ya Shilole.

Ameandika “Kutoka picha ya kwanza mpaka ya pili sio kaz ndogo aiseee haraf nashangaaa videm from no where vinaanza shobo mamaeeeee zenu kama mnatumwa kufitinisha mapenz yetu mmefeli mimi ndo ashangedere na mim ndo shishi mtoto wa Tabora nimezoea kula ugali sio wa chipsi mayai sasa mtu ajifanye anshobo na baby wangu aje nimuoneshe jinsi majengo ya serikali yanavyogawanywa watu! nampenda mpenz wangu ndo maana namsapot”
Share:

Sunday, May 19, 2013

VIDEO: MWANGALIE SHILOLE AKIKATA MAUNO MBELE YA MIDUME AKIWA NDANI YA GARI...

 

ANGALIA VIDEO YENYEWE HAPO CHINI...
Share:

Friday, May 3, 2013

"BILA CONDOM HUWEZI KULIFAIDI PENZI LANGU HATA UKINIHONGA MABILIONI"...SHILOLE

Mwigizaji na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Zena Mohamed, maarufu kwa  jina  la   shilole amedai kuwa anaweza kufanya ujinga wowote humu duniani lakini linapokuja suala la mapenzi kamwe hawezi kwenda pekupeku ( bila  condom )  ....

Akiongea kwa  kujiamini ,Shilole  alisema kuwa hata mtu awe vipi, au awe wa dini gani au awe na pesa kiasi gani kamwe hawezi kumvulia nguo kama  hana  kondom  mkononi.....
Msanii  huyo  alienda  mbali  zaidi  na  kuzilaani   kauli   za  baadhi  ya  watu zinazosema eti ukitumia "CONDOM"  ladha ya mapenzi inapungua.Yeye  anadai  kuwa  ni  mdau  wa  "GEMU"  hilo  na  huwa  anatumia  NDOM  kama  kawa  na  hufurahia  kama  kawaida...

" Hata niwe nimelewa kiasi gani huwa nipo makini sana maana najua vijana wengi wa mjini wananimezea  mate....Waje  tu , lakini  bila  KINGA wataambulia  PATUPU!!” Alisisitiza Shilole
Share:

Monday, April 29, 2013

BAADA YA KUTELEKEZWA NA BARNABA COCO BEACH SHILOLE AFUNGUKA NA KUSEMA "HAKUNA WA KUNITENGANISHA NA BARNABA WANGU"...!!

MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa hakuna kinachoweza kumtenganisha na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Elius Barnabas ‘Barnaba’ kwani walikotoka ni mbali.


Shilole na Barnaba hivi karibuni walinaswa maeneo ya Coco Beach wakila bata lakini baada ya kuwaona mapaparazi wakizunguka kutafuta matukio, Barnaba alitimua mbio na kumuacha Shilole ambaye bila hiyana alitiririka:
“Jamani mimi na Barnaba hakuna cha kututenganisha japokuwa watu wanachonga sana hata kuandikwa kwenye magazeti lakini bado tunaendelea tu, hivyo najua hakuna mtu anayeweza kututenganisha.”
Share:

Monday, April 15, 2013

"SHILOLE NI MNAFIKI...MIMI SIKUMBAKA BALI ALINIPA PENZI KWA HIARI YAKE"....MAKALA


MZAZI mwenziye na staa wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Makala Elias amembomoa staa huyo na kumwambia aache kuungopea umma kuwa alibakwa wakati waliishi naye kinyumba.


Akiongea  na  mwandishi wetu, Makala aliweka wazi kuwa anasikitika anapomsikia Shilole akisema kwamba alipata ujauzito baada ya kubakwa wakati walioana na kuachana miaka ya nyuma kabla staa huyo hajawa maarufu.

“Namsihi Shilole aache kusambaza taarifa kwenye vyombo vya habari na kuwafanya Watanzania wamuone mtoto aliyenaye alimpata kwa njia ya kubakwa wakati alikuwa ameolewa na mimi,’’ alisema Makala ambapo Shilole alikataa kuzungumzia juu ya ishu hiyo akidai ameshazungumza mara nyingi.
Share:

Wednesday, April 10, 2013

SHILOLE ANASA KWENYE PENZI LA MZUNGU...!!



SIKU chache baada ya kuripotiwa akijiachia kimalavidavi na ‘lejendari’ wa Bongo Fleva, Aboubakar Katwila, staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa hotelini na bwana Mzungu aliyetajwa kwa jina moja la George, kamera za Risasi Mchanganyiko ni noma.
Kwa mujibu wa shushushu wetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika hoteli moja maarufu jijini hapa ambapo Shilole alikuwa kwenye ziara ya shoo yake.
Ilidaiwa kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara ya shoo, Shilole hakuondoka jijini hapa na badala yake alionekana sehemu tofauti akijivinjari na jamaa huyo ambaye uchunguzi wetu ulibaini kuwa ni bosi wa klabu moja maarufu ya usiku Kanda ya Ziwa.
Kabla ya kuondoka katika jiji hili la sangara na sato, Alhamisi iliyopita na ndege ya jioni, Shilole alinaswa kimalavidavi na Mtasha huyo Jumatano katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere wa Gold Crest kulipokuwa na maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Syria.
Shilole alishuhudiwa akifanyiwa ‘shopping’ ya kufuru na bwana huyo ambapo gazeti hili lilinasa mpango mzima ambapo lilipotaka kujua kama ni wapenzi, Mtasha huyo alijibu kwa kifupi sana: “No comment” (sina la kusema).
Kwa upande wake Shilole alipobanwa mbavu alifunguka: “Nisingependa kuongelea jambo hilo kwani sasa najipanga kimuziki zaidi, shopping ni mambo ya kawaida sana kwa hiyo ni vyema tukaongelea muziki wangu kwani shoo yangu ya Pasaka ilijaa mashabiki wa kufa mtu so nakubalika sana Mwanza na siku moja nitaweka makazi hapa.”
Share:

Thursday, April 4, 2013

SHILOLE, Q-CHILLAH WAWAKERA WATU KWA MABUSU YAO YA HADHARANI....!!!


  
Aibu hiyo ilitokea Machi 29, mwaka huu ambayo ilikuwa Ijumaa Kuu ambapo wasanii hao walikuwa wakitoka Dar kwenda Mwanza kwa ajili ya kufanya shoo siku ya Pasaka.
Akilisimulia gazeti hili, shuhuda wetu aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo (jina tunalo) alisema aliwaona Shilole na Q-Chillah wakiwa katika ‘malovee’ ambapo mara kwa mara walikuwa wakipigana mabusu kitendo kilichowafanya abiria wengine kuwakodolea macho yenye kuwashangaa.



“Tunakubaliana na kazi zao, lakini kusema ule ukweli, sisi abiria wenzao tulishangaa sana, unajua kuonesha vitendo vya mahaba ndani ya ndege si utamaduni wetu Wabongo,” alisema abiria huyo aliyekuwa akienda Mwanza kikazi.
Aliongeza kuwa, ilifika mahali baadhi ya abiria walitaka kuwafungukia ukweli kwamba wanachokifanya si adabu hasa ikizingatiwa kuwa wao wana majina makubwa katika burudani za Bongo.
Kufuatia taarifa hizo na kudakwa kwa picha zao, Amani liliwasaka watuhumiwa hao kila mmoja kwa wakati wake ili kusikia kutoka kwao juu ya kufanya madudu ndani ya ‘pipa’.

Kwa upande wake, Shilole alisema kuwa mabusu ni vitu vya kawaida kwake ikizingatiwa Q-Chillah ni mwanamuziki mwenzake kwa hiyo hakuna tatizo.
“Jamani kwani mabusu yana shida gani, yule (Q-Chillah)  ni mwanamuziki mwenzangu na tumezoeana. Yale yalikuwa ni mambo ya kawaida tu na utani, si vinginevyo,” alisema  Shilole.



Q-Chillah simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita muda mwingi bila kupokelewa, lakini baadhi ya watu wake wa karibu walisema mwanamuziki huyo hana kawaida ya kupokea simu kama namba hazijui. 
Share:

Monday, April 1, 2013

SHILOLE ABANWA KUHUSU KUTONGOZA SERENGETI BOYS...!!



Wiki iliyopita katika safu hii tulimtambulisha kwenu msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, kama kawaida maswali mengi yaliulizwa kama ifuatavyo:
KWELI ALIOLEWA?
Eti ni kweli uliolewa na ulikuwa unaishi Keko? Khatibu, Dar, 0715456296.
SHILOLE: Kweli.
TABIA YA KUTONGOZA SERENGETI BOYS
Shilole acha kutongoza watoto wadogo halafu sauti ya kuimba huna, acha fani za watu. Sister Havinitishi, Dar, 0655196161.
SHILOLE: Mimi kwanza ni mdogo na siwatongozi watoto wadogo, kuhusu kuimba nitajifunza zaidi.
KUHUSU BABA WATOTO WAKE
Dada Shilole uko juu nakupa big up! Ningependa kufahamu hao watoto wako umezaa na baba mmoja au kila mtoto ana baba yake? Angel, Dar, 0714600415.
SHILOLE: Asante, watoto wangu kila mmoja ana baba yake.
HUYU AMEMZIMIA
Shilole naomba namba ya simu maana unanikosha wewe ni mzuri sana. Sangoti, Korogwe, 0654848387
SHILOLE: Asante, nitakutafuta.
KUHUSU MIDUME MCHARUKO MTAANI
Shilole wewe ni msanii mahiri kunako kiwanda cha filamu na muziki Bongo, je, unajiepusha vipi na midume inayokutokea kimapenzi? Salim Liundi, Dar, 0658110395.
SHILOLE: Asante, huwa najiepusha na midume kwa kujiheshimu na kujilinda hivyo siwapi nafasi.
UHUSIANO WAKE NA NGASSA
Shilole nataka kujua eti wewe na kiungo mahiri wa timu ya Simba Mrisho Ngassa mnatoka kimapenzi, mbona kuna tetesi za ajabu kitaani? Msomaji.
SHILOLE: Siyo kweli.
MZAZI MWENZAKE VIPI?
Umesema una watoto wawili, je vipi kuhusu mzazi mwenzio uko naye au ndiyo umemtema baada ya kupata umaarufu? Shariff Juma, Dar, 0713332349.
SHILOLE: Siko naye.
BIFU LAKE NA FLORA
Shilole hongera kwa kazi zako unajitahidi ila nataka kujua kwa nini hupatani na Flora Mvungi.  Silla, Dar, 0718764242.
SHILOLE: Asante, mimi sijagombana na mtu ila mti wenye matunda siku zote lazima upigwe mawe.
KUFICHA WATOTO WAKE
Zamani ulikuwa unaficha kama una watoto wawili mpaka mtu wako wa karibu alipotoa hiyo siri, kwa nini ulifanya hivyo? Cassian, 0655202202.
SHILOLE: Siyo kweli mbona watoto wangu wapo wazi!
KUHUSU MKOROGO
Big up! Shilole napenda muziki wako ushauri wangu kwako acha mkorogo unakuharibu. Tina, Mwanza, 0719747965.
SHILOLE: Siku hizi sipaki mkorogo, nimeacha.
SKENDO YA KUTOKA NA RAY
Dada Shilole unafanya kazi nzuri ila punguza skendo nasikia ulishawahi kutembea na Ray, je ni kweli? Charles Mallya, Mwanza, 0759022399.
SHILOLE: Asante, sijawahi kutembea na Ray.
BARNABA JE?
Shilole hivi ni kweli ulikuwa unatembea na Barnaba na kwa sasa mpenzi wako ni nani? Musa Mbughi, Sumbawanga, 0764021259.
SHILOLE: Siwezi kusema chochote.
UKWELI KUHUSU KUBAKWA
Shilole najua mtoto wako wa kwanza umezaa na Makala wa Igunga Tabora na ulikuwa unaishi naye kwa Tatu Balozi, ilikuwaje ukasema mwanaume aliyekupa mimba ya kwanza alikubaka? Ibrahim Yusuph, Dar, 0719599195.
SHILOLE: Sipendi kurudi nyuma ila ni kweli alinibaka nikapata ujauzito.
HISTORIA YAKE KWA UFUPI
Dada nataka kujua historia yako kiufupi. Sultan, Dar, 0654324222.
SHILOLE: Nimezaliwa Igunga Tabora nikiwa mtoto wa mwisho, sanaa nilianza mwaka 2010.
Share:

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger