Hakimu mmoja nchini Brazili amefunga
mawasiliano ya mtandao wa simu kwa njia ya whatsapp kwa saa 72.Hakimu
huyo Marcel Montalvao amesema kampuni inayomiliki mtandao huo imeshindwa
kusaidia kutoa taarifa katika kesi ya uhalifu.
Mwezi
Machi,Montalvao aliamuru kukamatwa kwa afisa mwandamizi wa Facebook
katika nchi za Kilatini bwana Diego Dzoran baada ya kukataa kutoa
ushirikiano katika uchunguzi dhidi ya dawa za kulevya.
Whatsapp
mtandao unaomilikiwa na Facebook umesema umekatishwa tamaa na kitendo
hicho kwa kuwa wamekuwa wakitoa ushirikiano wa kutosha mahakamani.
Mtandao huo umekuwa ukifungiwa mara kadhaa nchini Brazil kwa miezi michache ya karibuni kwa sababu zinazofanana na hizo.
0 comments:
Post a Comment