Uzinduzi wa basi la wanawake pekee
katika mji mmoja wa China umewakasirisha wanaume wa taifa hilo na kuzua
mjadala mkali katika mitandao ya kijamii.
Huduma hiyo mpya
itatolewa wakati wa asubuhi na wakati wa shughuli nyingi katika mji wa
mashariki wa Zhengzhou katika juhudi za kupunguza visa vya wanwake
kusumbuliwa na wanaume kulingana na gazeti la Dahe daily.
Kampuni
hiyo ya basi itawalinda wanawake dhidi ya kunyanyaswa wakati wanapovaa
nguo nyepesi huku wanawake wanaonyonyesha wakihisi wapo salama.
Treni
za wanawake na mabasi yameanzishwa katika mataifa mengi na kuonyesha
ufanisi mkubwa ,lakini magari ya uchukuzi ya watu wa jinsia moja ni
swala jipya nchini Uchina.
Wanawake waliohojiwa ndani ya basi hilo
wanasema wanafurahishwa na huduma hiyo huku mmoja akimwambia ripota
kwamba ni heshima kubwa kwa wanawake.Lakini baadhi ya wanaume hawafurahii jambo hilo.
Mmoja aliliambia gazeti la Dahe Daily kwamba unyanyasaji sio jambo la kawaida katika magari ya uchukuzi.Kampuni ya basi hilo imewakejeli wanaume ikisema: Hatua hii itawafedhehesha wanaume.
Mtu
mwengine amelalamika katika kituo cha redio cha Uchina:Nililazimika
kungojea sana kwa basi jingine kuwasili kwa kuwa sikuruhusiwa ndani.
0 comments:
Post a Comment